MENGI aamua kuwabana wazushi

MENGI aamua kuwabana wazushi

Halisi

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2007
Posts
2,802
Reaction score
614
Nimekutana na taarifa iliyotolewa leo na wakili wa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Reginald Mengi, siku moja baada ya gazeti la Tazama kuandika habari na makala zenye muelekeo wazi wa chuki na jazba za wazi.

TAARIFA YA WAKILI MICHAEL NGALO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KICHWA CHA HABARI KATIKA GAZETI LA TAZAMA TANZANIA “MENGI AKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI – Wananchi wataka Tume ichunguze bilioni 40 za Ukimwi”


Ukurasa wa mbele wa gazeti la Tazama Tanzania toleo Na. 321 la Jumanne 6-113-19,2009 lilichapisha kichwa cha habari “Mengi akumbwa na kashfa ya ufisadi – Wananchi wataka Tume ichunguze bilioni 40 za Ukimwi”.

Gazeti hilo lilichapisha katika ukurasa wa pili habari yenye kichwa cha habari “Mengi na kashfa ya ufisadi”. Habari hiyo inaeleza pamoja na mambo mengine kwamba mwanaharakati mmoja wa ukimwi amedai kwamba:-

• Mengi alikuwa na sakata la akaunti ya zaidi ya bilioni 40 za wafadhili iliyofunguliwa kwa jina lake na ambayo mpaka sasa hakuna maelezo fedha hizo zilitumikaje au zilikwenda wapi, kwa sababu fedha hizo zilizowekwa katika akaunti yake zilichukuliwa na hazikuwafikia walengwa.

• Mengi alifanya njama za udanganyifu kutumia fedha zote peke yake huku akiwaacha waathirika wakifa.

• Uchunguzi wa kina ufanyike ili waliochukua fedha hizo warudishe kama walivyofanya wa EPA na Serikali ikabidhi upelelezi wa fedha hizo za waathirika wa ukimwi kwa ofisi ya Mwanasheria Mkuu ili wahusika waweze kuhojiwa na kuchukuliwa hatua.

Yote yaliyoandikwa katika habari hiyo hayana ukweli wowote, na yanalenga kumkashifu Bw. Mengi. Inasema kwamba Bw. Mengi alifanya njama na udanganyifu kwa kutumia kwa manufaa yake binafsi Shilingi Bilioni 40 alizoomba na kuwekwa katika akaunti yake kwa manufaa ya waathirika wa ukimwi.

Gazeti la Tazama Tanzania linasema Bw. Mengi amekumbwa na ufisadi; linataka achunguzwe na atakiwe kurudisha fedha hizo kama walivyofanya watu waliohusishwa na EPA. Kwa maana ingine, linamwita fisadi na mwizi kama wale wa fedha za EPA.

Inaelekea Mhariri na Mwandishi wa gazeti hilo hawakufuata maadili ya
uandishi wa habari na hawakutaka kuandika ukweli, kwani wangefanya
uchunguzi angalao kwa kumhoji Bw. Mengi wangepata ukweli wa jambo hilo.

Wangefanya hivyo, wangebaini kwamba tarehe 17 Mei,2006 Mwanasheria
Mkuu wa IPP alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba IPP imegundua hati za kugushi za mradi uliopewa jina “Home Based Care Services Centre” na maombi yaliyopelekwa UNAIDS ya Sh. Bilioni 60 kutoka kwa mtu au watu waliojiita “Reginald Mengi Community Services” kama wamiliki wa mradi huo. IPP iligundua pia “Bank Statement” iliyogushiwa yenye jina “Reginald Mengi Community Care” ya NBC Corporate Branch iliyoonyesha kwamba mradi huo wa “Reginald Mengi Community Services” ulikwisha toa kwenye akaunti hiyo jumla ya Sh. 39,939,866,333.00 kutokana na maingizo ya jumla ya Sh. 41,552,733,874.00 ndani ya muda mfupi wa miezi minne tu.

Kwa kuwa IPP au Bw. Mengi hawakuwa na mradi unaoitwa “Reginald Mengi Community Services” au maombi ya msaada wa Sh. Bilioni 60.0 UNAIDS, ilihisiwa kwamba hati hizo ziligushiwa ama kwa makusudi ya kuzitumia kwa njia moja au ingine kuchafua jina la Bw. Mengi au kuzitumia katika vitendo vya jinai au vya udanganyifu mkubwa.

Mwanasheria Mkuu wa IPP aliwaandikia barua UNAIDS na kuwapa nakala za mradi uliogushiwa akitaka kujua kama walipata kupokea maombi ya msaada wa fedha kutoka kwa mradi huo na kuwaomba wawaripoti polisi wahusika kama wakifika ofisini kwao. UNAIDS walijibu kwa maandishi kwamba hawajapata maombi kama hayo na walitoa taarifa kwa vyombo vya habari tarehe 19 Mei,2006 kukanusha upokeaji wa maombi ya msaada kwa mradi huo.

Mwanasheria Mkuu wa IPP aliiandikia pia NBC Corporate Branch kutaka kujua kama wana akaunti ya “Reginald Mengi Community Care” na kama wanayo waeleze ilifunguliwa na nani. NBC ilipatiwa nakala ya picha ya “Bank Statement”. NBC walijibu kwa maandishi kwamba “Bank Statement” hiyo haikuwa ya NBC Limited.

Barua kwa UNAIDS na NBC zilinakiliwa kwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Dar es Salaam.

Majibu ya UNAIDS na NBC yalithibitisha kwamba hati za mradi, maombi ya msaada wa fedha UNAIDS na “Bank Statement” ya NBC zilikuwa za kugushi kama ilivyokuwa imehisiwa.

Kutokana na kashfa za gazeti hili kwa Bw. Mengi, kuna nia ya kupeleka shauri mbele ya Baraza la Habari Tanzania kuliomba waitwe Bw. Mengi au Wakili wake, na Mhariri na Mmiliki wa gazeti la Tazama Tanzania na kusikiliza na kuamua kama Mhariri wa Tazama Tanzania na Mmiliki wake wamemkashifu Bw. Mengi au la, na hatimaye kuchukua hatua au kutoa maagizo inavyopasa na yenye nia ya kumaliza tatizo hili.




¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬¬
_____________________________
Michael Ngalo, Wakili
Ngalo & Company Advocates
14 Januari,2009
 
Last edited by a moderator:
ukitinga kwenye siasa tinga na dhambi zako zote na ujue jinsi ya kujitetea
 
Hili la zamani mbona.. yaani watu hata hawakumbuki habari hiyo iliandikiwa hata magazetini.? well, wanajitahidi kujaribu lakini.
 
Na nakumbuka ilitolewa maelezo ya kutosha kiasi kwamba watu wote walilizika hata waliotoa pesa walilidhika kuwa Bwana Mengi hausiki
 
ukitinga kwenye siasa tinga na dhambi zako zote na ujue jinsi ya kujitetea

Mkuu,

Hapo Mengi ametinga kwenye siasa zipi? Anagombea cheo gani?

Tatizo hapo ni Mengi kupigana dhidi ya ufisadi. Najua Mengi kama mfanyabiashara kuna makosa amefanya lakini bado yeye kwa Tanzania ni nafuu mno ukilinganisha na hao wanaotuibia kila siku.
 
Mafisadi watatafuta kila njia ya kumchafua Reginald Mengi kwa kuwa vyombo vyake vya habari vimewaanika vilivyo. Mwisho wa sikuu uongo unagonga mwamba tu. Pole ndugu yetu Mengi. Tuko nawe katika kukuombea ili wasikudhuru kwa chochote. Mungu akulinde kama tuilindavyo mboni ya jicho.
 
Unless sikuyaelewa vizuri maelezo ya mwanasheria ya Mengi lakini ilivyo ni kwamba hakukuwahi kuwa na hiyo NGO na hata pesa haziwahi kuombwa kutoka UNAIDS na wala benki statement haikuwa ya kweli. Kwa hiyo hapa kila kitu kilikuwa ni cha kupika ili kuharibu jina la Mengi. Cha kushangaza hawa jamaa wa TAZAMA waMeibuka upya na suala ambalo liliwahi kutolewa maelezo na likafungwa.

Ni siri iliyo wazi kuwa hawa wanatumiwa na mafisadi kupunguza kasi ya Mzee kupiga vita UFISADI. Wamekwama na tena kwa aibu kubwa!
 
Kwa kweli nashangaa sana jinsi hiyo makalana habari ilivyoandikwa kishabiki na jinsi walivyosahau hata kwamba suala hilo lilifikishwa hadi polisi kwa dci \manumba baada ya UNAIDS na NBC kukerwa na watu walioghushi
 
Kwa kweli nashangaa sana jinsi hiyo makalana habari ilivyoandikwa kishabiki na jinsi walivyosahau hata kwamba suala hilo lilifikishwa hadi polisi kwa dci \manumba baada ya UNAIDS na NBC kukerwa na watu walioghushi

Hao inabidi wachunguzwe, inaelekea wanawajua waliotekeleza mpango huo
 
Kwa kweli nashangaa sana jinsi hiyo makalana habari ilivyoandikwa kishabiki na jinsi walivyosahau hata kwamba suala hilo lilifikishwa hadi polisi kwa dci \manumba baada ya UNAIDS na NBC kukerwa na watu walioghushi

ebanae! hayo ndo mambo ya Karamagi et al., hilo gazet la TAZAMA TANZANIA linamilikiwa na Karamagi. Mafisadi wameanzisha magazeti haya kwa lengo la kujisafisha na kuwachafua wengine. kazi ipo!
 
Unless sikuyaelewa vizuri maelezo ya mwanasheria ya Mengi lakini ilivyo ni kwamba hakukuwahi kuwa na hiyo NGO na hata pesa haziwahi kuombwa kutoka UNAIDS na wala benki statement haikuwa ya kweli. Kwa hiyo hapa kila kitu kilikuwa ni cha kupika ili kuharibu jina la Mengi. Cha kushangaza hawa jamaa wa TAZAMA waeibuka upya na suala ambalo liliwahi kutolewa maelezo na likafungwa.

Ni siri iliyo wazi kuwa hawa wanatumiwa na mafisadi kupunguza kasi ya Mzee kupiga vita UFISADI. Wamekwama na tena kwa aibu kubwa!!!!!!!!!

Tuko pamoja katika hili.Hizi habari zishatolewa maelezo ya kutosha siku nyingi,inaelekea baadhi ya magazeti yanaanzishwa kwa malengo ya kuwachafulia majini watu.Tazama kila mara wanatoka na habari ya kumchafua Mengi!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
mmh... mimi nadhani kifanyike kikao cha mafisadi ili kuwapa maelezo ya jinsi ya kupambana na wale wanaowaudhi kwani mbinu zao bado ni dhaifu sana. Mengi haitaji kwenye Baraza la Habari yeye awafungulie mashtaka mahakamani, na kuwadai fidia ya Bilioni 30 (akinigawia .005% ya kiasi hicho kwa ushauri huu haitakuwa na ubaya). Pamoja na hayo hilo gazeti pia liandike kwa maandishi makubwa yale yale kuwa "Tumechemsha kuhusu Mengi" ili awasamehe deni hilo!
 
Kwa kweli nashangaa sana jinsi hiyo makalana habari ilivyoandikwa kishabiki na jinsi walivyosahau hata kwamba suala hilo lilifikishwa hadi polisi kwa dci \manumba baada ya UNAIDS na NBC kukerwa na watu walioghushi


Kwa nini asilipeleke mahakamani moja kwa moja kwa kuandika habari ya uongo? huko MCT ni kupotezeana muda tu dawa ya watu kama hao ni kwafikisha kizimbani mara moja na kuomba mahakama ifungie gazeti hadi kesi iishe
 
mmh... mimi nadhani kifanyike kikao cha mafisadi ili kuwapa maelezo ya jinsi ya kupambana na wale wanaowaudhi kwani mbinu zao bado ni dhaifu sana. Mengi haitaji kwenye Baraza la Habari yeye awafungulie mashtaka mahakamani, na kuwadai fidia ya Bilioni 30 (akinigawia .005% ya kiasi hicho kwa ushauri huu haitakuwa na ubaya). Pamoja na hayo hilo gazeti pia liandike kwa maandishi makubwa yale yale kuwa "Tumechemsha kuhusu Mengi" ili awasamehe deni hilo!


Duh...kaka kumbe naona tumefikiri sawa apo!
 
Huyu Mzee anachemsha sasa....anashindana na MWEHU Charles Charles!!! Dawa yao hawa ni kuwadharau tu....kwanza gazeti lenyewe haliuziki na wanunuzi ni wajinga wenzao tu ambao wamejichokea....
 
Cha kusikitisha ni kwamba kiwango cha uandishi kilichoonyeshwa na Tazama kimeanza kuzoeleka, na tunaelekea kwenye udaku na ujinga; hawakufanya upembuzi kabisa kwa wanachokiandika... au labda wameamua kufanya hivyo ili ku-divert public attaention kwa sasa.

On a positive note; Ngalo kafanya cha maana, kaanzia kunakotakiwa (kwenye baraza lao), haya mambo ya mahakama kwa sasa in most cases ni uptezaji wa muda na ishara ya corrupt legal system ambayo everyone can run to (especially kama anajua kuna mwanya fulani). Naamini wataishia hapo maana Tazama wameandika utumbo mtupu.

Kizuri zaidi ni jinsi mafisadi wanavyoshuka hadhi mpaka wanafikia kufukua makaburi kutafuta cha kusema kuhusu Mengi, wanatapatapa na mifano ni mingi... sio wale tuliokuwa tumewazoea wakiwa na confidence, wide smiles everywhere na authority, wamerudi kuwa na kauli kama za watu waliofumaniwa na kukumbushia ya zamani ku-justify upuzi wao

The more these fisadis write utumbo, the better for our nation because they are just reducing themselves to size

"Say No to Fisadis"
 
Back
Top Bottom