Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mbowe aliahidi kuwa mwaka 2023 ungekuwa mwaka wake wa mwisho kuiongoza CHADEMA kama mwenyekiti wa chama. Wengi kama si wote, tuliunga mkono uamuzi wake huo maana kuwa kiongozi haimaanishi kukaa kwenye uongozi kwa miaka nenda rudi, bali kuwa na uwezo wa kuwatengeneza watu wengine kuwa viongozi ambao watahakikisha yale mema uliyoanzisha yanaendelea na kuboreshwa zaidi.
Baada ya vuta nikuvute za sasa, maneno mengi yamekiwa yakisemwa kuhusu Mbowe, na yote yanayosemwa dhidi yake yanasimama kwenye imani kuwa Mbowe atagombea tena nafasi ambayo ameishikilia kwa miaka 20!! Mimi binafsi siamini kama Mbowe atagombea tena. Kwanza ni kwa sababu yeye mwenyewe aliahidi kuwa asingegombea tena nafasi hiyo, pili, akifanya hivyo itaonesha yeye hakuwa kiongozi makini maana ameshindwa kuwatengeneza wengine kuwa viongozi, na sababu ya tatu, chama kinahitaji mtazamo na mbinu mpya kuweza kusonga mbele kwa sababu mbinu zilizotumika kwa miaka 20 ya uongozi wa Mbowe, japo zimesaidia chama kujengeka zaidi, lakini hakujawa na mafanikio makubwa.
Kimachosikitisha zaidi ni kauli za baadhi ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA, kufikia kutoa kauli zisizo na uthibitisho dhidi ya Mbowe, eti agent wa Serikali ya sasa, wengine kusema kuwa eti ni CCM aliyepandikizwa upinzani ili kuipa uhalali CCM kuonesha nchi ina demokrasia!!
Ni kweli kuwa baada ya Mbowe kutolewa mahabusi na kisha kuwa na vikao mfululizo na Rais Samia, Mbiwe amepoa sana, huku chama na wanachama wakipitia magumu mengi, pengine kuliko kipindi chochote, ikiwemo utekwaji na mauaji ya viongozi na wanachama wakosoaji wa serikali.
Hata hivyo kupooza kwake wakati wanachama wake wakidhulumika, haiwezi kuwa ni uthibitisho wa moja kwa moja kuwa amenunulika au amekuwa mamluki wa CCM dhidi ya wanachama wake. Yawezekana, kutokana na yeye kuwekwa mahabusu kwa karibia nusu mwaka, huku wananchi wakishindwa kufanya chochote kuilazimisha Serikali kumtoa huko mahabusu alikowekwa kwa kesi ya kubambikiwa, kulimvunja moyo wa kuendelea kusimama kwenye misimamo mikali. Au yawezekana, kitendo cha Rais Samia kumrudishia mali zake na kumlipa fidia ya rasilimali zake zilizoharibiwa wakati wa utawala wa awamu ya 5, kunamnyima ujasiri wa kufanya chochote dhidi ya Serikali iliyomfanyia wema (kama anaamini kurudishiwa mali zake zilizoporwa ni hisani).
Jambo la muhimu kwa Mbowe kwa sasa, ni kuwaziba midomo wanaomsemea vibaya, na hilo anastahili kufanya kwa vitendo, kwa kusimama katika ahadi yake ya kutogombea tena, na badala yake asimamie uchaguzi kwa uadilifu mkubwa kuhakikisha wanapatikana viongozi ambao wanaaminika kwa kila mtu kuwa hawanunuliki kwa bei yoyote ile. Nje ya hapo, nchi itarudi hatua 100 nyuma, kuweza kujenga chama kingine mpaka kufikia ilipofikia CHADEMA, halafu kiende mbele zaidi.
Kwa uchafu mwingi unaoendelea nchi hii, tunahitaji chama cha upinzani chenye nguvu na kinachoongozwa na watu wenye misimamo thabiti, wasio na uwoga, ambao hata watu wa kuwahonga wanaogopa hata kuwasogelea, na kwa sasa, kwa kipimo chochote kile, kiwe cha ndani au cha kimataifa, mtu pekee anayejulikana kwa hilo kwa sasa, ni Tundu Lisu. Tundu Lisu ni mtu aliyeamua kuyatoa maisha yake kama sadaka kwaajili ya watu wengine. Watu wa namna hiyo si wengi Duniani, sisi angalao tunaye huyu mmoja asiye na mashaka.
Mbowe aridhie kwa moyo wa heri, msaidizi wake akipeleke chama mahali pengine kutoka pale yeye atakapoachia.
Nakutakia Tundu Lisu maandalizi mema ya kutafuta kuchaguliwa, na namtakia mapumziko mema Mh. Mbkwe, baada ya mapambano ya miaka 20, japo nina hakika chama kinaendelea kukutumia kinavyosonga mbele chini ya uongozi mpya.
NOTE: CHADEMA haitakiwi kuwa kama CCM. Kama CHADEMA ikawa unatenda mambo yake yake ambayo CCM inatenda, au inaiga mbinu chafu za CCM, kuna haja gani ya CHADEMA kuwepo, si afadhali watu waendelee na mateao ya miaka yote? Lazima CHADEMA na viongozi wa CHADEMA, waoneshe kwa vitendo ni nini na kwa namna gani CHADEMA inafanya tofauti na CCM, kwenye muelekeo chanya.