Natoa rai kuwa serikali iwakate pembe tembo wetu wote, kama ambavyo ng'ombe hukatwa zihifadhiwe na serikali.
1. Kwa namna hiyo tutaweza kuhifadhi uzao wao, maana hawatawindwa tena na majangili.
2. Serikali Izitumie kama bond kupata mitaji ya shughuli za uzalishaji.
TUJADILIANE!!
Ungepewa wewe tenda hiyo, ungefanyaje? Ungetumia tekinolojia ipi?
Ungepewa wewe tenda hiyo, ungefanyaje? Ungetumia tekinolojia ipi?
Mkuu usiiumize kichwa bure teknolojia ipo rahisi sana kama wakiamua ingawaje siungi mkono hoja!! Iko iv kuna risasi za sindano ndani ya kuna dawa ya usingizi/kulewesha ambayo mnyama akpgwa ndani ya sekunde 25 anasinzia na anaweza kuja kuzinduka ndani ya masaa 5!! Hiyo niliona Animal planet Tv kuna msitu fulani ulaya kuna wanyama fulani ni wakali Afrika hawapo hao watafiti walikuwa wanazunguka na helkopta na kuwasogelea karbu kisha wanawapga risasi then wanawapakia kwenye helkopita baada ya kuwa wamesinzia!!
Vizazi vijavyo wanataka wawaone wakila majani kisha wachukue kinyesi chake wakatengenezee dawa ya pumu.Angewapiga risasi wafe kwanza then anawakata.. Halafu anawakausha wakakae makumbusho, lengo si vizazi vijavyo wawaone?
Kha! Wakati unamkata na yeye katilia tu? Kama vile mtu anatahiriwa????
Hao watafiti wapo Tanzania? Au ndiyo tuandae bajeti ya kuwalipa wazungu? Au tuombe mkopo benki ya dunia?
Mkuu hao watafiti nimewaongelea kama reference tu. Yani ukikabidhiwa hizo zana za kazi hata wewe unamalza mchezo!!