fundibenz
Member
- Jul 31, 2015
- 61
- 67
Salaam Wakuu wangu, natumaini wote mko vema na mnaendelea salama na ujenzi wa Taifa Tanzania.
Natumaini Kama si wote basi baadhi yenu mnauzoefu na ujuzi japo kwa kiasi fulani juu ya vyombo vya moto {hapa nimelenga zaidi magari}
Wandugu mimi ni mpenzi wa Gari aina ya Gari aina ya Mercedes Benz C- Class sasa wakuu naombeni ushauri juu ya hii gari:-
1} Changamoto zake katika uendeshaji/umiliki
2} Utunzaji
3} Utumiaji wa mafuta
Na pia kama kuna kingine tujuzane kwa faida ya wote wenye ndoto hii.
Asanteni wakuu.
C class ni model ya benz ambayo hazina mambo mengi na ni ya mtumiaji wa kawaida hata gharama zake zinakuwa sio juu sana,
Hiyo ni c class W203,zinaanzia 2003 hadi 2006,
Zinakuwa na engine ya 4 petrol,(M111 or M271) cc 1990 hadi 2000,
Kuna zenye engine ya v6(112) c230
Na kuna yenye engine ya diesel
Ila kukushauri chukua ya petrol 4cylinder.
Utuzaji ,inahitaji kuzingatia service na kuonana na fundi kila unapoona tatizo au warning light,
Vilevile spare zake kwa sasa sio ghali maana hii model zipo nyingi
Kwa engine ya 4 hainywi mafuta kabisa,kwa kifupi hii gari iko poa sana
Sent from my iPhone using Tapatalk