Nimesoma mpaka, najisikia amani kwa sababu sasa nina ufahamu, (siyo wa riport ila wa maoni)
Kulipia.
Hili halina mjadala, ni lazima watu walipe. Nashauri copy ziongezwe ili wengi walipie na hela zipatikane za kufuatilia mambo mengine mabaya zaidi juu ya taifa hili. Mbona wananunua magazeti? mbona wanalipa DSTV? mbona wakienda kwenye internet cafe wanalipa? Kazi makini ina gharama kubwa sana, ni resarch gani imefanyika popote duniani bila kufadhiliwa au kulipiwa. Kulipia ni muhimu na si hicho kiwango kidogo cha elfu thelathini nashauri kiwe laki moja.
Ukombozi wa Taifa.
Ukombozi unaletwa na wale wanaoelewa vya kutosha kuwa kuna tatizo, sasa hivi tunapojadiliana hapa, kuna watu wako na shida nyingi sana zinazotokana moja kwa moja na madudu ya watawala wetu lakini hawajui kuwa shida zao zinasababishwa na hawa waheshimiwa. Hawa itawachukua miaka mingi kulelewa maana ya ukombozi na kwa mantiki hiyo tutaonana nao baada ya kazi ngumu. Kulipia ni muhimu
Ufahamu.
Ili uwe na ufahamu ni lazima kuwepo na gharama, hata kama elimu ni ya bure ni lazima unyanyuke na kufunga safari ya kwenda darasani haiwezekani shule ikufuate nyumbani. Sasa wote tuliopo hapa ni watu wenye uelewa angalau wa kufungua anwani ya kutuma e-mail. Iweje tunataka vitu hivi vya gharama kubwa bure. Nashauri tugharimie.
Maoni
Kazi iliyofanyika ni ya kupewa heshima, inastahili kabisa kuwekwa kwenye kumbukumbu za wapigania haki na uhuru wa mawazo nchini mwetu. ni katika haya nawaomba wana JF waone umuhimu wa hawa waliofanya kazi hii na kuwaunga mkono kwa kuchangia hicho kidogo.
Utumwa.
Mimi nafanya kazi kwa muhindi, mshahara anatoa tarehe anayopenda yeye, nilikuwa natamani sana nami niipate nakala yangu, lakini bado sijashika pesa mkononi, mpaka nitakapopata mshahara wangu copy zitakuwa zimeisha, ila silalamiki kwa sababu naamini kuwa kazi ni njema na itazaa matunda muda si mrefu. Ukombozi wa kifikra ukija utanipa masilahi mimi pia.
MWANAKIJIJI.
Nimependezwa na maoni yako nakupongeza binafsi, big up sir.