Meremeta 00:00:00. EXTRA

Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.
Kwa mbali naanza kukumbuka ule msemo wa "Akusaidiaye Kuokota Kuni Asubuhi, Ikifika Jioni Umkumbuke Katika Kuota Moto".

Napata hisia za wazi kuwa kwa wale wahariri na waandishi wa bongo ambao, kwa namna moja au nyingine, walineemeka au kusaidiwa na mafisadi katika kutafuta mfadhili wa njaa zao, kamwe lazima waone aibu na kuingiwa wasiwasi linapokuja suala la kuwaanika mafisadi hao. Hili liko dhahiri kabisa!!

Wanajiona wanalazimika kurudisha fadhila kwa kuwapa kajoto mafisadi wakati wa kipindi hiki cha baridi kali ya Meremeta yenye kuwatetemesha.

Kidogo kidogo tutazidi kuwajua
 
Yawezekana MAGAZETI HAYAJAPATA NAKALA au wanasubiri kuphot*****!
 
Nakala wanazo... Hilo halina shaka.

Tatizo nani wa kulianzisha? Mwenye nia na nguvu ya kufanya hivyo na tumuone.. Mengi ya magazeti haya yanachokoza kwa mbali yakihofia kuchinjiwa baharini
 
Nakala wanazo... Hilo halina shaka.

Tatizo nani wa kulianzisha? Mwenye nia na nguvu ya kufanya hivyo na tumuone.. Mengi ya magazeti haya yanachokoza kwa mbali yakihofia kuchinjiwa baharini
labda wanaipitia maana inahita umakini zaidi badala ya kukurupuka..lkn naona Raia Mwema limeandika
 
Tatizo la nchi yetu,tumegoma kuendelea na viongozi wetu wapo kuhakikisha mgomo unaendelea na unatekelezwa na ndiyo maana kuna kashfa nyingi za ufujaji/uharibifu/uchakavu wa mali na raslimali za Taifa hili changa(ambalo ni kusudio la viongozi wetu hadi sasa hivi).
Na mfano mzuri utashangaa leo linaongelewa hili kesho lile bila ya hata utekelezaji wa makusudi na hata kama kuna utekelezaji basi ujue lazima wataishia njiani na kuja na maelezo kibao yasiyo na msingi.Au inabuliwa issue mpya halafu wafunika ya zamani bila hata kufikia katika hatimisho;yaani ni usanii mtupuuuu!!
 
Magazeti yenye nia njema na nchi yetu yataandika tu.Atakayeshitakiwa atamtaka mshitaki akanushe yaliyoandikwa kuhusu Meremeta.
 
Magazeti ya leo hayajasema lolote juu ya Ripoti ya Meremeta nafikiri wanatafakari nini cha kufanya,ripoti iko so incriminative against the Government.Lazima busara itumike kujua nini cha kuandika vinginevyo kutakuwa na kasheshe kubwa sana serikalini.
 
Kwenye sanaa it is all about timing! Ndio maana kwenye movie wanazo zile sounds effects.. pale mtu ananyemelewa unasikia sauti ya chini, pole polee.. na panapokuwa na impending danger basi sauti inaongezwa na kasi vile vile.. halafu ikitokea kitu basi i "boom"! hadi unaruka kwenye kiti chako.. so everything is abt timing.
 
Mwanajamii,
Unalojambo la kutueleza. Hebu tupe habari kama ulishayajua yote hayo kwamba yalishatajwa kwenye taarifa mbali mbali, hivi hakuna jambo ambalo unakumbuka kwamba labda MKJJ amesahau kulitaja au kuongeza kwenye hii ripoti?? Au umeona yote ni yale tu uliyokuwa unafahamu au uliyokwisha soma, Je hakusahau kitu kweli? Hebu ongezea kidogo basi Mkuu!
 
Next time make it 50,000/= ili 20,000/= iwe donee kwa JF. Kama hili limewezekana, keep thinking big, watu serious always watakuwa nyuma yenu.

Ndivyo haswa inatakiwa iwe! it sounds as if we have uwts ambao hawataki ripoti nyingine itokee hapa kiujanja ujanja tuuu!
 
Hii trust itaanzishwa kwa fedha za nani mwenye moyo mzuri wa kutuanzishia hiyo trust? I would like to explore this idea kwani sina furaha ya kuzuia ripoti muhimu kwa sababu ya michango; safari hii imetulazimu.

May I ask what entails starting the trust?
Haiwezekani kuundwa group hapa hapa JF iliyo na moyo huo wakajiunga na kuahidi/kutoa walicho nacho halafu tukaelezwa imepatikana kiasi gani?
Najiuliza pia server tu imetushinda JF inatishiwa kufungwa, inaweza kuwa ngumu mwanzoni lakini ikafanikiwa as reports start coming out. Tunawaomba wenye mawazo mazuri zaidi na uwezo watupe ushauri zaidi.
 
Nimesoma mpaka, najisikia amani kwa sababu sasa nina ufahamu, (siyo wa riport ila wa maoni)

Kulipia.
Hili halina mjadala, ni lazima watu walipe. Nashauri copy ziongezwe ili wengi walipie na hela zipatikane za kufuatilia mambo mengine mabaya zaidi juu ya taifa hili. Mbona wananunua magazeti? mbona wanalipa DSTV? mbona wakienda kwenye internet cafe wanalipa? Kazi makini ina gharama kubwa sana, ni resarch gani imefanyika popote duniani bila kufadhiliwa au kulipiwa. Kulipia ni muhimu na si hicho kiwango kidogo cha elfu thelathini nashauri kiwe laki moja.

Ukombozi wa Taifa.
Ukombozi unaletwa na wale wanaoelewa vya kutosha kuwa kuna tatizo, sasa hivi tunapojadiliana hapa, kuna watu wako na shida nyingi sana zinazotokana moja kwa moja na madudu ya watawala wetu lakini hawajui kuwa shida zao zinasababishwa na hawa waheshimiwa. Hawa itawachukua miaka mingi kulelewa maana ya ukombozi na kwa mantiki hiyo tutaonana nao baada ya kazi ngumu. Kulipia ni muhimu

Ufahamu.
Ili uwe na ufahamu ni lazima kuwepo na gharama, hata kama elimu ni ya bure ni lazima unyanyuke na kufunga safari ya kwenda darasani haiwezekani shule ikufuate nyumbani. Sasa wote tuliopo hapa ni watu wenye uelewa angalau wa kufungua anwani ya kutuma e-mail. Iweje tunataka vitu hivi vya gharama kubwa bure. Nashauri tugharimie.

Maoni
Kazi iliyofanyika ni ya kupewa heshima, inastahili kabisa kuwekwa kwenye kumbukumbu za wapigania haki na uhuru wa mawazo nchini mwetu. ni katika haya nawaomba wana JF waone umuhimu wa hawa waliofanya kazi hii na kuwaunga mkono kwa kuchangia hicho kidogo.

Utumwa.
Mimi nafanya kazi kwa muhindi, mshahara anatoa tarehe anayopenda yeye, nilikuwa natamani sana nami niipate nakala yangu, lakini bado sijashika pesa mkononi, mpaka nitakapopata mshahara wangu copy zitakuwa zimeisha, ila silalamiki kwa sababu naamini kuwa kazi ni njema na itazaa matunda muda si mrefu. Ukombozi wa kifikra ukija utanipa masilahi mimi pia.

MWANAKIJIJI.
Nimependezwa na maoni yako nakupongeza binafsi, big up sir.
 
- Wakuu tuwajibike japo kidogo tu, copies tunawapatia wananchi wasioweza kuingia hapa JF, lakini kwa wale wote tunaoingia hapa kila siku hakuna excuse ya kutoinunua hii copy toka kwa Mkulu Mwanakijiji, please tupunguze umatonya yaani dola thelathini tu kununua elimu ya taifa lako nayo ni taabu sasa tunaanza kusumbuana huko pembeni, Pleasee! Ahhhgggrrrrr!

Respect.

FMEs!
 
- Wakuu tuwajibike japo kidogo tu, copies tunawapatia wananchi wasioweza kuingia hapa JF, lakini kwa wale wote tunaoingia hapa kila siku hakuna excuse ya kutoinunua hii copy toka kwa Mkulu Mwanakijiji, please tupunguze umatonya yaani dola thelathini tu kununua elimu ya taifa lako nayo ni taabu sasa tunaanza kusumbuana huko pembeni, Pleasee! Ahhhgggrrrrr!

Mkuu ukifuatilia kwa umakini na kiundani hapa JF watu wengi tunatofautiana kwa kipato kama ujuavyo kipato cha kibongo bongo kuna wengine hapa wanafanya kazi mshahara wake hauzidi hata 100,000/= si unajua kazi za wahindi mkuu. Mtu kuchangia anataka sana lakini hali ya uchumi ina mkaba na anataka kupata elimu lakini anashindwa afanyaje ndo anaamua umatonya mbona hata mkuu wa akaya inapo bidi anatembeza bakuri kwa wahisani hali ngumu mkuu na watu tunatofautiana.
Naomba Mwanakijiji baada siku kadhaa kupita tuomba report uianike wazi ili kila raia apate na kufikisha ujumbe kwa ndugu na jamaa. Wakuu twende mbele na kurudi nyuma kipato tunatofautiana kabisaa hili halina ubishi.
 
- Wakuu tuwajibike japo kidogo tu, copies tunawapatia wananchi wasioweza kuingia hapa JF, lakini kwa wale wote tunaoingia hapa kila siku hakuna excuse ya kutoinunua hii copy toka kwa Mkulu Mwanakijiji, please tupunguze umatonya yaani dola thelathini tu kununua elimu ya taifa lako nayo ni taabu sasa tunaanza kusumbuana huko pembeni, Pleasee! Ahhhgggrrrrr!

Respect.

FMEs!

Kweli kabisa Mkuu,

Ushauri kwa Mkuu Invisible/Mwanakijiji,.....
...sina uhakika sana kuhusu uhusiano wa JF na bloggers maarufu kma akina Michuzi et al.........ni vema ikiwa tutashirikiana na bloggers of Michuzi type kusambaza elimu itolewayo hapa JF.......
 
kwa nini kumekuwa na MEDIA BLACK OUT kwenye hili jambo?

maana naona magazeti yote zaidi ya lile RAIA MWEMA halijaripoti

Kulikoni? au imebackfire?
 
kwa nini kumekuwa na MEDIA BLACK OUT kwenye hili jambo?

maana naona magazeti yote zaidi ya lile RAIA MWEMA halijaripoti

Kulikoni? au imebackfire?

Mkuu nimejaribu kuchunguza wanaogopa kutokana hii ishu ni siri lakini pindi MJJ atakapo weka wazi report hiyo na kila mtu adownload basi MEDIA itafanya kazi yake kwa sasa mkuu ni ngumu usitegemee kama wata andika chochote.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom