Meremeta 00:00:00. EXTRA

Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.
umenichekesha.. that is how I felt last night.. we gave a notice a week ago! Ila labda hali ngumu ya uchumi.. and I know wengine watakuja baada ya kupata mshiko wao.


Unajua sisi wakristo tunaamini Yesu atarudi, watu wameambiwa wajiandae kwa maana hawajui muda wala saa, sasa nakuhakikishia ingawa kila jumapili na kila siku wanaambiwa kwenye Internet na TV na Radio.

Bado Yesu atarudi na kukuta wapo watu wengine hawajaJITAYARISHA.

Ndo naona hata hapa JF
 

Ni kweli kabisa, PhD usipende vya bure. Toa pesa upate hiyo report.

tunaozungumzia hii ripoti siyo kwamba hatujalipa ili kuipata, tumelipa 30,000, tumelipa na kuisoma ili kum- support mwanakijiji lakini hiyo haituzuii kuikosoa. Ni bora tuambiwe kwamba baada ya kulipia na kuisoma wanajf haturuhusiwi kuikosoa.
 
tunaozungumzia hii ripoti siyo kwamba hatujalipa ili kuipata, tumelipa 30,000, tumelipa na kuisoma ili kum- support mwanakijiji lakini hiyo haituzuii kuikosoa. Ni bora tuambiwe kwamba baada ya kulipia na kuisoma wanajf haturuhusiwi kuikosoa.
kp_523.jpg
 
Phd umenena nimesikitika sana kwamba ripoti hiyo haina jambo jipya zaidi ya kunukuu taarifa mbalimbali kama zilivyowahi kuripotiwa na vyombo vya habari, vyama vya upinzani na mashirika ya wanaharakati. siyo kwamba napuuza ripoti hii lakini haikustahiriki kuuzwa kwa madai kuwa ni ya uchunguzi kwa kina. MZEE MWANAKIJIJI ni kama umejishushia hadhi kwa kuamua kuuza ripoti hii. Wengi tulisubiri kuona kitu kipya. I beg to differ.
Ndivyo wamekutuma uje uwasemee siyo?
 
tunaozungumzia hii ripoti siyo kwamba hatujalipa ili kuipata, tumelipa 30,000, tumelipa na kuisoma ili kum- support mwanakijiji lakini hiyo haituzuii kuikosoa. Ni bora tuambiwe kwamba baada ya kulipia na kuisoma wanajf haturuhusiwi kuikosoa.

Kwa nini unawaza kukosoa tu? na sio kuongeza inputs zako kama unazo???
 
umenichekesha.. that is how I felt last night.. we gave a notice a week ago! Ila labda hali ngumu ya uchumi.. and I know wengine watakuja baada ya kupata mshiko wao.

Usishangae mimi nitaleta mchango wangu hata kama hii ripoti itakuwa public. The issue sio hela, the issue ni hii move itself.

Naona watu wanaongelea eti hamna jipya. Ndio hata kama hamna jipya lakini mwamsho wa fikra kuhusu ufisadi bado unaendelea. Hicho ndo kitu muhimu. Lazima tuongelee haya maswala hata tukirudia rudia kama sala, hamna shida cha msingi ni kuendelea kusema na kusema kwa njia na style mbalimbali one day tutafanikiwa. I am very sure.
 
Comrade, please if you can afford do me afavour,send me the coppy of this report through my email address[EMAIL="a.scope_full@yahoo.com"].scope_full@yahoo.com.niko[/EMAIL] ktk maeneo ambayo siwezi kwa namna yoyote kutuma fedha kwenda kwa wahusika(remember their dead line).lakini nitasikitika sana kama nitashindwa kuipata.
please just trust me and do me a favour on that.
natanguliza shukrani

The future of our nation is on the hands of patriotic citizens..........
 
Leo kama si kosei ni t+2, na bado sijaona ripoti ikijadiliwa au kama imeleta impact yeyote. Vipi tena, au tusubiri t+7?
 
Sina Uhakika sana kama ni wa kujibiwa, maana wapo ambao hata kama utawajibu unakuwa unatwanga maji kwenye kinu kwani wameshaamua wawe upande gani.

Inawezekana kwa mtazamo wako uko sahihi (hatuwezi jua labda upo kwenye position uliyoweza kuaccess hizi information kabla au hata kufaidi mgao wa Hiyo biashara kwi kwi!). Lakini wengi unatakiwa kutupa nafasi na sisi ya kupima alichotuletea MMM.

Hata kama ni taarifa ambazo wengi walishazisema zimewahi kuwa published kuwa kwenye Document moja? Maana ya report ni nini? Ni kukusanya pamoja ushahidi na kuuweka kwenye mpangilio. Kwa mfano report ya Bw. Utoh (CAG) juu ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo aliyokabidhi jana kwa PM Unadhani itakuwa na jipya?

Itakuwa inajibu hypothesis zetu tulizo nazo, Itakuwa inajaribu kusema hili ni kweli hili si kweli, na itakuwa na mapendekezo. Vivyo hivyo hata report ya Mwanakijiji juu ya Meremeta ni report inayotaka kusema juu ya Hypothesis tulizokuwa nazo. Kuwa na Hypothesis haimaanish umeshakuwa na results, report yako baada ya uchunguzi inaweza ikasema tofauti na hypothesis.

Pia jambo lingine la Msingi ni kuwa kama hakuna kitu, watu hawapati mahali pa kuanzia kujadili Hoja. Si unaona waraka wa Wakatoliki umetukumbusha mambo mengi, umetukumbusha ugawaji wa rasilimali zetu, katiba, madaraka ya Rais na mambo mengine mengi. hata hii Report inategemewa kutoa kianzio cha waTanzania kujadili mstakabali wa nchi yao. Itatuapa nafasi ya kujua wapi tuliteleza, na tukisha kujua tutajua tufanye nini ili tusimame tena.

Sinema ya Darwin Night mare, ilikuwa haina jambo lolote jipya, ilionyesha watu wanakula mapanki (ni kweli) ilionyesha malaya wanajiuza (ni kweli). Unaweza ukaniambia kwanini mh. Rais JK alichachamaa mpaka kufoka sana huko mwanza? Nini Kilimkasirisha kwenye ile documenatary? Kwanini watu walilazimishwa kuandamana? na baadaye kukawa na mjadala mkubwa sio Bongo tu na sehemu zingine Duniani.

Kwa hiyo Vitu kama Darwin night mare huwa hazina kitu kipya lakini zinawafanya watu wafikirie zaidi mbali zaidi ya urefu wa pua yao. Baada ya ile Documentary imewafanya watu kama akina Mwanakijiji na sisi wengine tujiulize kuwa kuna nini nyuma ya hii pazia la samaki na mapanki? kwanini JK amechachawa hivi, hata Ulaya na sehemu zingine duniani kote wanauza K. Sasa amekasirika nini?

Unaona ile katuni ya kipanya akijiuliza kuwa kwanini viwanda vya samaki vipo Mwanza tu na wakati Tanga mpaka Mtwara kuna bahari na hakuna Viwanda? kwanini Kigoma lake Tanganyika hakuna Viwanda? watu makini Tukiona katuni kama ile huwa tunaenda maktaba kujaribu kutafuta majibu, na huko hatutegemei kusema tunayoamini kutoka moyoni mwetu bali kuoona tafiti za wenzetu zinasemaje, kwa hiyo ndizo tunazitumia kutengeneza jibu kwa kuzi-review. (Katika Ulimwengu wa sayansi inakubalika) na baadye kufananisha na majibu ya wakati huu.

Kwa hiyo watu kama Mwanakijiji wamechukua hatua kubwa sana ambayo wasomi wengi Tanzania wameshindwa kufanya, Mashirika mengi yameshindwa kufanya. Tunashindwa kufanya kwasababu tunahesabu gharama kwanza au tunaogopa (sio vibaya)

Kama UWT wangeifanya hii kazi tungewapongeza lakini ikifanywa na raia wenzetu wasio tumia kodi zetu tunapaswa kufanya zaidi ya kuwapongeza, Mwanajamii tunapaswa kuwaunga mkono, Tuwaunge mkono tuwapunguzie gharama za kukusanya hizi data na kuziweka in a presentable form, tuwaunge mkono kwa kuanza kujadili na kusema wazi, tuwaunge mkono kwa kuwaambia wengine wasio jua kweli waijue, na kusimama na kusema sasa inatosha, Enafu iz Enafu! INATOSHA.

Tumedanganywa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha, sasa ni wakati wetu wa kuwa na taifa la watu walio sawa na Huru, ni wakati wa kila aitwaye Mtanzania kupata nafasi ya kujadili mstakabali wa nchi yake, ni wakati wa kila mbongo kupata nafasi kuvuna kilichopandwa shambani mwetu, kwenye shamba letu la familia ya watanzania. Tusikatishane tamaa, kama huwezi kuwa upande wetu lakini unaamini kuwa hupo upande wao, basi tulia, tuache tuvipige vita, tukishinda tutakualika kwenye karamu ya kufaidi matunda ya nchi.

Ijueni Kweli nayo Kweli Itawaweka Huru.

Mbogela; Hapo umenena, wasipokuelewa ukilaza unawasumbua, lakini umefunga kazi. thanks
 
I wish we could discuss this document lakini mie siwezi na sababu wahusika wanazijua

..anyway

kuna mtu ame scan magazeti ya Leo? wanasemaje kuhusu hii ripoti?
 
I am trying ku scan magazeti yalivyoripoti on Meremeta lakini sioni kitu jamani hebu leteni news articles ili tuweze kuscan tuone walivyoripoti on this report ...na lengo kuu ni kuona magazeti yepi ambayo hayatoi credit to JF

THIS SHOULD BE INTERESTING
 
Nani aandike magazeti ya Bongo? Wengi wanaogopa kubambikiwa wizi wa siri za serikali!
 
Nani aandike magazeti ya Bongo? Wengi wanaogopa kubambikiwa wizi wa siri za serikali!
Mwoga ataikomboaje nchi yake, au ni mshirika unaogapa kuumbuliwa na wanamtandao wenzio.
Waulize Manyerere, Rweyemamu (Salva), Rweyemamu (Mihingo) na Balile; hoi na ndani ya tope la ufisadi!
 
Kweli wote wanojifanya wana habari nyeti na moto safaro hii wameloa kabisa au kuna memo imepita ya mkwara??maana si kawaida kabisa hata udaku kimya?maana nina hakika wana copy tayari....kila mhariri anasikiliZia...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom