Sina Uhakika sana kama ni wa kujibiwa, maana wapo ambao hata kama utawajibu unakuwa unatwanga maji kwenye kinu kwani wameshaamua wawe upande gani.
Inawezekana kwa mtazamo wako uko sahihi (hatuwezi jua labda upo kwenye position uliyoweza kuaccess hizi information kabla au hata kufaidi mgao wa Hiyo biashara kwi kwi!). Lakini wengi unatakiwa kutupa nafasi na sisi ya kupima alichotuletea MMM.
Hata kama ni taarifa ambazo wengi walishazisema zimewahi kuwa published kuwa kwenye Document moja? Maana ya report ni nini? Ni kukusanya pamoja ushahidi na kuuweka kwenye mpangilio. Kwa mfano report ya Bw. Utoh (CAG) juu ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo aliyokabidhi jana kwa PM Unadhani itakuwa na jipya?
Itakuwa inajibu hypothesis zetu tulizo nazo, Itakuwa inajaribu kusema hili ni kweli hili si kweli, na itakuwa na mapendekezo. Vivyo hivyo hata report ya Mwanakijiji juu ya Meremeta ni report inayotaka kusema juu ya Hypothesis tulizokuwa nazo. Kuwa na Hypothesis haimaanish umeshakuwa na results, report yako baada ya uchunguzi inaweza ikasema tofauti na hypothesis.
Pia jambo lingine la Msingi ni kuwa kama hakuna kitu, watu hawapati mahali pa kuanzia kujadili Hoja. Si unaona waraka wa Wakatoliki umetukumbusha mambo mengi, umetukumbusha ugawaji wa rasilimali zetu, katiba, madaraka ya Rais na mambo mengine mengi. hata hii Report inategemewa kutoa kianzio cha waTanzania kujadili mstakabali wa nchi yao. Itatuapa nafasi ya kujua wapi tuliteleza, na tukisha kujua tutajua tufanye nini ili tusimame tena.
Sinema ya Darwin Night mare, ilikuwa haina jambo lolote jipya, ilionyesha watu wanakula mapanki (ni kweli) ilionyesha malaya wanajiuza (ni kweli). Unaweza ukaniambia kwanini mh. Rais JK alichachamaa mpaka kufoka sana huko mwanza? Nini Kilimkasirisha kwenye ile documenatary? Kwanini watu walilazimishwa kuandamana? na baadaye kukawa na mjadala mkubwa sio Bongo tu na sehemu zingine Duniani.
Kwa hiyo Vitu kama Darwin night mare huwa hazina kitu kipya lakini zinawafanya watu wafikirie zaidi mbali zaidi ya urefu wa pua yao. Baada ya ile Documentary imewafanya watu kama akina Mwanakijiji na sisi wengine tujiulize kuwa kuna nini nyuma ya hii pazia la samaki na mapanki? kwanini JK amechachawa hivi, hata Ulaya na sehemu zingine duniani kote wanauza K. Sasa amekasirika nini?
Unaona ile katuni ya kipanya akijiuliza kuwa kwanini viwanda vya samaki vipo Mwanza tu na wakati Tanga mpaka Mtwara kuna bahari na hakuna Viwanda? kwanini Kigoma lake Tanganyika hakuna Viwanda? watu makini Tukiona katuni kama ile huwa tunaenda maktaba kujaribu kutafuta majibu, na huko hatutegemei kusema tunayoamini kutoka moyoni mwetu bali kuoona tafiti za wenzetu zinasemaje, kwa hiyo ndizo tunazitumia kutengeneza jibu kwa kuzi-review. (Katika Ulimwengu wa sayansi inakubalika) na baadye kufananisha na majibu ya wakati huu.
Kwa hiyo watu kama Mwanakijiji wamechukua hatua kubwa sana ambayo wasomi wengi Tanzania wameshindwa kufanya, Mashirika mengi yameshindwa kufanya. Tunashindwa kufanya kwasababu tunahesabu gharama kwanza au tunaogopa (sio vibaya)
Kama UWT wangeifanya hii kazi tungewapongeza lakini ikifanywa na raia wenzetu wasio tumia kodi zetu tunapaswa kufanya zaidi ya kuwapongeza, Mwanajamii tunapaswa kuwaunga mkono, Tuwaunge mkono tuwapunguzie gharama za kukusanya hizi data na kuziweka in a presentable form, tuwaunge mkono kwa kuanza kujadili na kusema wazi, tuwaunge mkono kwa kuwaambia wengine wasio jua kweli waijue, na kusimama na kusema sasa inatosha, Enafu iz Enafu! INATOSHA.
Tumedanganywa kiasi cha kutosha, tumedharauliwa kiasi cha kutosha, sasa ni wakati wetu wa kuwa na taifa la watu walio sawa na Huru, ni wakati wa kila aitwaye Mtanzania kupata nafasi ya kujadili mstakabali wa nchi yake, ni wakati wa kila mbongo kupata nafasi kuvuna kilichopandwa shambani mwetu, kwenye shamba letu la familia ya watanzania. Tusikatishane tamaa, kama huwezi kuwa upande wetu lakini unaamini kuwa hupo upande wao, basi tulia, tuache tuvipige vita, tukishinda tutakualika kwenye karamu ya kufaidi matunda ya nchi.
Ijueni Kweli nayo Kweli Itawaweka Huru.