A
Anonymous
Guest
Habari za kwenu?
Kuna mwalimu wa kiume wa sekondari ya Nkoasenga anaitwa Alb.... (jina limefupishwa) katika kijiji cha Nkoasenga wilaya ya Meru, kata ya Leguruki mkoa wa Arusha anafanya biashara haramu ya kuuza bangi kwenye baa yake.
Wanafunzi wa sekondari nao huenda katika baa hiyo kununua bangi.
Tabia zake hizo zimekuwa zinaathiri wakazi na watoto wa kijiji hiki kwa kuuza bangi kwenye baa yake kwa wanafunzi na vijana wetu.
Pili vijana wengi wa kijiji hiki wameathirika na bangi anazouza huyu mwalimu. Sisi tukiwa ni wakazi wa kijiji hiki tumechoka na tabia zake zisizo na maadili na kuondoa maadili ya jamii yetu ya watu wa Meru.Tunaomba sheria ichukue mkondo wake na ahamishwe kijini kwetu.
Tunaomba mamlaka za kupambana na dawa za kulevya na idara ya elimu wafanye uchunguzi kubaini suala hili.
Wazazi tumechoka na tabia yake ya uuzaji wa bangi.
Meru bila bangi inawezekana.
Mwalimu ni maadili na haiba.