DOKEZO Meru, Arusha: Kuna Mwalimu ni mvuta bangi na anauzia wanafunzi Bangi

DOKEZO Meru, Arusha: Kuna Mwalimu ni mvuta bangi na anauzia wanafunzi Bangi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Huko Meru si ndiko wanalima bangi? Zuieni kwanza kilimo cha bangi, mkiweza kudhibiti uzalishaji basi hakutakuwa na wauzaji, sasa utadili na muuzaji wakati kiwanda kipo na kinaendelea kuzalisha? Mwalimu endelea kupiga kazi, Mambo ya kufuatilia yapo mengi sana......
 
Ma ticha wa kizazi kipya ni VITUKO!
Mara ubakaji, mara kuwatia mimba wanafunzi, mara adhabu Kali, mara kuweka kinyumba wanafunzi, mara.
......
Inatisha.....

...
 
Ma ticha wa kizazi kipya ni VITUKO!
Mara ubakaji, mara kuwatia mimba wanafunzi, mara adhabu Kali, mara kuweka kinyumba wanafunzi, mara.
......
Inatisha.....

...
Mnawaandama maticha badala muwaandame watekaji na mafisadi...

Hiloooo lione kwanza
 
Habari za kwenu?

Kuna mwalimu wa kiume wa sekondari ya Nkoasenga anaitwa Alb.... (jina limefupishwa) katika kijiji cha Nkoasenga wilaya ya Meru, kata ya Leguruki mkoa wa Arusha anafanya biashara haramu ya kuuza bangi kwenye baa yake.

Wanafunzi wa sekondari nao huenda katika baa hiyo kununua bangi.

Tabia zake hizo zimekuwa zinaathiri wakazi na watoto wa kijiji hiki kwa kuuza bangi kwenye baa yake kwa wanafunzi na vijana wetu.

Pili vijana wengi wa kijiji hiki wameathirika na bangi anazouza huyu mwalimu. Sisi tukiwa ni wakazi wa kijiji hiki tumechoka na tabia zake zisizo na maadili na kuondoa maadili ya jamii yetu ya watu wa Meru.Tunaomba sheria ichukue mkondo wake na ahamishwe kijini kwetu.

Tunaomba mamlaka za kupambana na dawa za kulevya na idara ya elimu wafanye uchunguzi kubaini suala hili.
Wazazi tumechoka na tabia yake ya uuzaji wa bangi.

Meru bila bangi inawezekana.

Mwalimu ni maadili na haiba.
Mmea umebarikiwa hata Jah alipoongea na Mosses alijifanya mmea
 
Unaripoti kama Anonymous na bado unaogopa kutaja jina lake kamili, uoga wa namna gani huu??!! Dkt. Gwajima D
Hiyo hapo namba 119 ya mamlaka ya kudhibiti dawa za kulevya wapige haraka ili akutwe na ushahidi mubashara. šŸ‘‡
 

Attachments

  • IMG-20250825-WA0032.jpg
    IMG-20250825-WA0032.jpg
    79.8 KB · Views: 28
Back
Top Bottom