Message za tume ya uchunguzi wa mauwaji ya 29/10/2025 - 3/11/2025

Message za tume ya uchunguzi wa mauwaji ya 29/10/2025 - 3/11/2025

Nimepokea messages kwa namba zote ninazotumia

Wanataka nitoe/tutoe maelezo au ushauri, juu ya kilichotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi, kuisaidia tume.

Sina tatizo na massages hizo.
Shida yangu, ni,, je wako tayari kuupokea ukweli na watauandika ulivyo, watauwakilisha ulivyo na wataufanyia kazi ?? Nikiamua kwenda mwenyewe mbele ya tume watanisomea maelezo yangu jinsi nilivyowaeleza ndivyo walivyoandika.

Kwa wenye ushahidi wa picha na video, wako tayari kuvipokea kama vielelezo ?

Nawasilisha.

Tume imfuate Larry Madowo wakamjibu Yale maswali ambayo Semaji alishindwa kujibu. Kwanini Semaji alishindwa kujibu Maswali yake na kwanini kwenye Press yake hakumualika????

Makabuli ya Halaiki pale nyuma ya Mwananyamala Hospitali na kule Kondo - Bahari Beach ni kweli yapo???
 
Hata Mimi nimepokea nilichofanya ni kuwablock kanisa, kwanza aliyeunda tume ni rais batili wasiniharibie mood
 
Yani haya maccm wanadhani watu ni wajinga kiasi hicho.
Watu waliingiwa na nyongo mapema sana. Mmefunga wapinzani wote makini mkafanya siasa peke yenu kabla ya hapo mmeteka sana watu matukio ya KIBAO mdude na sativa yaliumua hasira ya taifa Leo mnatusumbua na mameseji yenu mbwa nyie.
 
Tutegemee report kuandika chanzo cha zile vurugu ni
-Taasisi na watu binafsi waishiyo nje ya TZ kuwalipa hela vijana kufanya vurugu.
-vyama vya siasa kuchochea uchaguzi usifanyike NRNE
- kukodisha watu kutoka nchi jiran kuhusika kwenye maandamano nk

Report haitandika haya
- Ukandamizwaji wa haki za binadamu hasa uhuru wa kuongea, Kutoa maoni binafsi na kujishughulisha na Siasa za upinzani kama katiba inavyosema.

- Utekaji na mauaji ya Raia wanaongea kuhusu udhaifu wa Serikali. (Wako weng sana wamepotezwa)

- kufungwa kwa vyombo vya habari (online TV), mitandao ya kijamii (twitter na JF) na watu binafsi (wanaHarakat na wanasiasa ) ambao wametoa maoni binafsi kuhusu uwajibikaji wa Serikali.

- kuminywa Haki kwa wanasiasa waliokubali kushiriki Uchaguzi wa Oct 29. ( Mpina , Sheikh Ponda na wengne weng).
Kutokuwepo kwa mazingira sawa huru kwa wanasiasa kipind cha kampeni.

Nk

Ripoti yao ni TAKATAKA...Judicial rubbish.
 
Tume haitafuti idadi ya wahanga, bali kwanini yametokea ,na way foward ...

Exactly.

Ni uchunguzi wa kwann vurugu zimetokea na sio uchunguzi wa Raia wangap wamefariki.

Sasa ukijua hii. Haikupi shida kujua namna Siasa inavyofanywa.
 
Nimepokea messages kwa namba zote ninazotumia

Wanataka nitoe/tutoe maelezo au ushauri, juu ya kilichotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi, kuisaidia tume.

Sina tatizo na massages hizo.
Shida yangu, ni,, je wako tayari kuupokea ukweli na watauandika ulivyo, watauwakilisha ulivyo na wataufanyia kazi ?? Nikiamua kwenda mwenyewe mbele ya tume watanisomea maelezo yangu jinsi nilivyowaeleza ndivyo walivyoandika.

Kwa wenye ushahidi wa picha na video, wako tayari kuvipokea kama vielelezo ?

Nawasilisha.
Achana nao. Lengo lao linajulikana,ni kupoteza ushahidi utakaohitajika ICC
 
Back
Top Bottom