Hahahaa kaka Saul aka Paul kawa mfalme lini!?Soul kazaliwa Jerusalem wakati wa utawalawa wa Rumi(Roman Empire),Saul alikuwa mnyapara kazi yake ilikuwa kuwasaidia warumi kuwasaka wafuasi wa Yesu na kuwauwa,...kwani Solomon(Suleiman) alikuwa anaishi Israel!
Ha ha ha mkuu Chabuso, soma hiki kitabu kikusaidie..
Masikini waislam, yaani hujui Saul ndiye mfalme wa kwanza wa Israel? Siyo kila Saul ndiye Paul, Paul ni mtoto mdogo sana, alikuwepo Saul wa enzi hizo.
Ngoja nikupe andiko.
1Samwel 8:4 Ndipo wazee wote wa Israeli wakakutana pamoja, wakamwendea Samweli huko Rama;
5 wakamwambia, Angalia, wewe umekuwa mzee, na wanao hawaendi katika njia zako; basi, tufanyie mfalme atuamue, mfano wa mataifa yote.
1Samwel 9:16 Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikilia.
17 Hata Samweli alipomwona Sauli, BWANA akamwambia, Huyu ndiye niliyekuambia habari zake; huyu ndiye atakayewamiliki watu wangu.
1Samwel 10:1 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.
17 Basi Samweli akawakusanya watu mbele za BWANA huko Mispa
18 akawaambia wana wa Israeli, BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Naliwatoa Israeli kutoka Misri, nami naliwaokoa ninyi na mikono ya Wamisri, na ya falme zote zilizowaonea;
19 lakini leo mmemkataa Mungu wenu, naye ndiye awaponyaye katika misiba yenu yote na shida zenu; nanyi mmemwambia, Sivyo, lakini weka mfalme juu yetu. Basi, sasa, hudhurieni mbele za BWANA, kwa kabila zenu na kwa elfu zenu.
20 Basi Samweli akawaleta kabila zote za Israeli karibu; na kabila ya Benyamini ikatwaliwa.
24 Samweli akawaambia watu wote, Mnamwona mtu huyu aliyechaguliwa na BWANA, ya kuwa hakuna mtu mfano wake katika watu wote. Ndipo watu wote wakapiga kelele, wakasema, Mfalme na aishi!