Messi anacheza ligi bora kuliko zote duniani! Ahame aende wapi?

Sijui Kala maharage ya wapi huyu[emoji15]
Nimegundua nafanya convo na MTU asiyefatilia mpira

Nimekupa takwimu hapo juu
Kwanini messi hawezi kuhama laliga alafu unaleta mambo ya Simba

Sorry brother
 
Ninajiuliza kwani huyo mviziaji yeye ameleta Kombe la dunia pale ureno
 
Heshimu watu na wewe utaheshimika

Kumitwa messi anduje inaonyesha jinsi gani usivyostaarabika

MTU mweusi ni wa kwanza kulilia anabaguliwa ila nyue ubaguzi mbele foot ball is love bro

Sa unalia au

Huyo ni overatted na timu anayochezea tu,nje ya hapo ni sakala tu na ndio maana anaogopa kutoka nje ya barca na masakala wenzake hamlioni hilo mnajifanya sio kitu muhimu ila kwetu sisi ni muhimu sana,hata akipewa ushindi mara tilioni moja,bila kutoka nje ya barca kwetu sisi si kitu
 
Nimegundua nafanya convo na MTU asiyefatilia mpira

Nimekupa takwimu hapo juu
Kwanini messi hawezi kuhama laliga alafu unaleta mambo ya Simba

Sorry brother
Kuwa na mahaba na Messi hakukufanyi usijishushe, jishushe ujadili mada uliyoiweka mezani vizuri kwa hoja na uthibitisho.

Mchezaji kuwa bora lazima atimize vigezo mbalimbali vya kuthibitisha kuwa yeye ni bora katika mipaka fulani( kiligi, kitimu, kitaifa, kidunia ).

Messi amekuwa bora mara 6 kidunia hadi sasa kwa kutwaa tuzo ya Ballon d'or ambapo hii tuzo inaangaziwa katika nyanja za vilabu, tena barani Ulaya pekee.

Ukija kwenye nyanja ya kitaifa katika nchi yake ya Argentina, kuna ukakasi mwingi wa kuthibitisha kuwa huyu ni bora Duniani, jambo ambalo ndio linazua mjadala namna hii.

Malegends kama akina Pele, Maradona, Zidane walikuwa bora kuanzia kwenye timu zao za Vilabu hadi timu za Taifa na walizisaidia nchi zao kutwaa mataji ya Kidunia. Hao vigezo vya kuwa bora vilitimia vizuri kuliko Messi ambapo vigezo vipo upande mmoja(wa kilabu yake ya Barca).

Sasa kinachohitajika, ni takwimu sahihi za Messi katika timu ya Taifa ili vithibitishe umwamba wake. Tuwekee takwimu.
 

Hao mkuu ni viroja juu ya viroja na hata wanaompaga ushindi huyo andunje nadhani wana mtindio wa ubongo,haiwezekani mtu yupo hapo hapo milele hajawahi kwenda kwingine na kudeliver halafu useme eti ni mkali,huo ni uzwazwa uliopitiliza
 
Mbona hamuelewi sio kwamba aende timu gani,Messi nje ya Barcelona hana tofauti na Molinga,Mfano akiwa nje ya Barcelona ni Argentina ameshafanya kitu gani cha maana.
Amefika,robo na nusu fainali za world cup...hapo ni padogo?
 
Messi kama mwanaume kweli atoke hapo Barkalona, sote tumejionea amefanya nini akiwa Argentina
Nawe kama mwanaume kweli uhame hiyo nyumba uhamie nyumba ingine tuone kama utashindwa maishai!.....hoja dhaifu sana hiyo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Acha kukosoa spelling unaona ulichoandika wewe
Hahahaaaaaa... Aiseee

Nimecheka kweli,

Yaani nimechapia kiwango cha lami
 
Kwanini hicho kipaji chake kimeshindwa kuisaidia Argentina miaka nenda Rudi kila mara yenye ndio amekuwa mtu wa kujiliza kama mtoto mdogo.
Ameshindwa kuisaidia Argentina? Leo hii tu umeshasahau alivyoisaidia kufuzu World Cup Russia kwa stunning goal ilhali Argentina ilikuwa inapumulia mashine? kufikia Argentina kuwa mshindi wa 2 kwenye World Cup pale South Africa unaona ni jambo dogo siyo? Labda kama una kichwa cha panzi.

Halafu tusikariri kuwa mchezaji ili awe mchezaji bora ni lazima awe ameshinda taji na timu yake ya taifa. Ingekuwa hivyo George Weah wala asingeitwa mchezaji bora wa dunia enzi zile, maana kila mtu anajua ile Liberia yake ni kichwa cha mwendawazimu kuliko Stars yetu. Na hata alipokuja Dar na Liberia yake kucheza na Taifa Stars hakuna lolote la maana alilolifanya katikati ya 1990s (sana sana ni yule mchezaji wa Mliberia aliyekuwa akiichezea Simba SC, William Fahnbuller, alionekana akiwasumbua akina Mtwa Kihwelu na wenzake).
 
Real Madrid ndio bora zaidi imechukua mataji mengi kuliko Barca..hivi mara ya mwisho Barca kuchukua klabu bingwa Ulaya ni lini???
 
Real Madrid ndio bora zaidi imechukua mataji mengi kuliko Barca..hivi mara ya mwisho Barca kuchukua klabu bingwa Ulaya ni lini???
Mkuu kwani Real madrid haipo La liga? umemuelewa mleta mada lakini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…