Kuwa na mahaba na Messi hakukufanyi usijishushe, jishushe ujadili mada uliyoiweka mezani vizuri kwa hoja na uthibitisho.
Mchezaji kuwa bora lazima atimize vigezo mbalimbali vya kuthibitisha kuwa yeye ni bora katika mipaka fulani( kiligi, kitimu, kitaifa, kidunia ).
Messi amekuwa bora mara 6 kidunia hadi sasa kwa kutwaa tuzo ya Ballon d'or ambapo hii tuzo inaangaziwa katika nyanja za vilabu, tena barani Ulaya pekee.
Ukija kwenye nyanja ya kitaifa katika nchi yake ya Argentina, kuna ukakasi mwingi wa kuthibitisha kuwa huyu ni bora Duniani, jambo ambalo ndio linazua mjadala namna hii.
Malegends kama akina Pele, Maradona, Zidane walikuwa bora kuanzia kwenye timu zao za Vilabu hadi timu za Taifa na walizisaidia nchi zao kutwaa mataji ya Kidunia. Hao vigezo vya kuwa bora vilitimia vizuri kuliko Messi ambapo vigezo vipo upande mmoja(wa kilabu yake ya Barca).
Sasa kinachohitajika, ni takwimu sahihi za Messi katika timu ya Taifa ili vithibitishe umwamba wake. Tuwekee takwimu.