Messi Vs Pele

Ukiona mjadala wanauhamishia kwa pele kutoka kwa ronaldo ujue wamekwishwa[emoji16]

Tutajie timu alizochezea pele

kwanza ligi ya USA na brazil km messi angecheza akiwa kijana angefunga goli alfu tatu na kuendelea

Namkubali pele km mfungaji mzuri ila hajamfkia messi
 
Mkuu mbona unakuwa mvivu ? Ulishawahi kujiuliza na kufanya Research kwanini Pele hakwenda Juventus, Real n.k. Tafuta sababu alafu utaelewa...

Ila kama watu wenye uwezo wa kuchambua ngoja tupime like for like..., yaani makombe / mashindano aliyocheza Pele na ambayo kacheza Messi (like for like) ambayo ni World Cup.., Hapo Stats zipo vipi naomba unijibu...
 
AHSANTE MKUU KeyserSoze kama ni hivyo kuwa enzi za pele offside zilikuwepo ila hakukuwa na faulo au penalt za mchongo kama sasa basi hakuna kama PELE.
 
Huna akili

Kombe la dunia ni mechi saba, mechi za ligi 30+

Messi hata asingechukua kombe lw dunia hakuna mchezaji wa kulinganishwa naye kwa kweli

Ni kweli pele alifanya vizuri enzi za mpira wa giza lkn kaachwa mbali na messi
 
Mpira si magoli tu, Ingekuwa hivyo basi viungo wasingeingia ktk list ya wachezaji bora duniani.

By the way, Messi alianza kama Winger, lazima ufungaji wake uwe mdogo kuliko forward. Hata hivyo mpaka sasa Messi keshamzidi Pele idadi ya Magoli na Assists. Lakini ukiacha yote hayo, Messi ana uwezo mkubwa wa kukusanya kijiji kuliko Pele. Pele alikuwa mwepesi wa kupoteza mpira kuliko Messi
 
Huna akili

Kombe la dunia ni mechi saba, mechi za ligi 30+

Messi hata asingechukua kombe lw dunia hakuna mchezaji wa kulinganishwa naye kwa kweli

Ni kweli pele alifanya vizuri enzi za mpira wa giza lkn kaachwa mbali na messi
Sasa unataka kulinganisha nini ? Au nikutajie wachezaji ambao waliweza kucheza vizuri La Liga wakarudi huko makwao wakashindwa kucheza au unadhani River Plate, Santos n.k. ni timu za vijiweni ?

Au unadhani kuna timu duniani ilikuwa haimtaki au kumfuata Pele ? Kama haujui ni kwamba Timu zote za ulaya zilikuja kumtafuta na nchi / Bunge kulazimika kubadilisha Sheria ili asiweze kuuzwa nje.....
 
Narudia huna akili

Kombe la Dunia ni mechi saba ligi ni mechi 30+
Messi hapimwi kwa kuchukua kombe la mechi saba tu japo amechukua

Pele aliogopa kwenda uropa kwasababu ushindani ni mkubwa kuliko huko kwao markani

River plate au bocca ingekuwa bora ingekuwa inachukua klabu bingwa wa dunia

Tunaona kila msimu klabu bingwa ya dunia inaenda ulaya
 
Mpira si magoli tu, Ingekuwa hivyo basi viungo wasingeingia ktk list ya wachezaji bora duniani.
Nani kasema ni Magoli ? Na unadhani Pele alikuwa na Magoli Pekee kuna kitu kinaitwa clinical ambacho Pele alikuwa nacho na Messi hana....
By the way, Messi alianza kama Winger, lazima ufungaji wake uwe mdogo kuliko forward.
kuanza kama winger hata kina Henry, Ronaldo n.k. walianza hivyo mpira wa sasa wale original number 9 / 10 hawapo tena..., na Pele pamoja na kuwa forward alikuwa anashuka na kutafuta mipira na ku-take on defenders....
Hata hivyo mpaka sasa Messi keshamzidi Pele idadi ya Magoli na Assists.
Yaani ucheze mechi nyingi zaidi alafu ujifananishe na mtu aliyecheza mechi chache...., ndio maana kuna kitu kinaitwa ratio....,
Lakini ukiacha yote hayo, Messi ana uwezo mkubwa wa kukusanya kijiji kuliko Pele. Pele alikuwa mwepesi wa kupoteza mpira kuliko Messi
Kukusanya kijiji ili waende wapi..., Pele alikuwa anazungukwa na madefender pia na sio kuzungukwa na kumwangalia bali kuzungukwa na kupigwa kiatu huku refa anapeta...., (sasa unadhani hapo mpira hautapotea) alafu hizo stats za pele kupoteza mipira umezitoa wapi ? Una stats ya Pass Completion ya Pele ?

Na tukijka kwenye chenga hatuwezi kumchukua Messi tukamuacha Garrincha ingawa na vyenga pia Pele anavyo...., pili kuna chenga constructive na ugumu wa kumyanganya mpira stricker nitamuangalia Ronaldo De Lima kabla ya Messi....,

By the way Pele hakuwa playmaker ila nikitaka playmaker effective tamchukua Pirlo na kumuweka Messi Bench kwahio mambo ya kukusanya vijiji is immaterial....
 
Pele ni muongo muongo Ronaldo alivyomfikia idadi ya magoli aliyo funga aka update bio ya insta kuongeza magoli ili aonekane bado anaongoza wakati mwanzo bio yake ilikua inasoma idadi ya magoli ambayo Ronaldo kayafikia.

Kwangu Mimi Messi ndo mchezaji Bora zaidi kwanza anacheza nyakati ngumu sana hakuna magoli ya offside Kama enzi ya kina pele na maradona waliokua wanafunga hadi na mkono
 
Wanaokoteza ili wamlinganishe na mbuzi Messi [emoji16]

Bahati nzuri sisi hatutumii nguvu takwimu za messi zinaongea tukianza kuleta messi anavyobeba vijiji [emoji16]
Sasa hii chenga ni ngumu kabisa hadi iwe kigezo cha kuwa the Greatest? ina maajabu gani?
 
Sasa mbona hapo anachezewa rafu na refa anasimamisha mpira kuonesha ni faulo? Tafuteni vigezo ndugu zangu otherwise Messi ni bora kuliko huyo pele.

Ngoja niseme jambo la uongo kwako ,
Umesema enzi hizo asist zilikuwa hazihesabiwi ila umetuandikia kwamba Pele ana 0.83 za asist huku Messi akiwa na 0.79
Huu ni uongo maana kama takwimu hazikuchukuliwa wewe umezitoa wapi?

Kuna kipengele cha Offside ambacho umekisemea mi naona cha wakati wa Pele kilikuwa soft maana enzi za sasa ambazo Messi kafunga sana hata tshirt ikizidi tu tayari ni offside that means Messi kafunga magoli huku wachezaji wengi ikilazimika awapite kwanza ndo akafunge.

Huyu Pele anaweza kuwa alikuwa bora sana ila Messi kamfunika kwa vingi sana kiuchezaji.
 
Sahihi
Messi kafunga kwenye ligi bora kabisa na ulimwengu ulioadvance kwenye soka kupita kawaida so he is the best
 
Kama ni World cup hata Messi 3 angekuwa nazo timu ilikuwa haijitambui tu eg 2014 ile fainal Argentina alishindwa mwenyewe kisa ujinga wa other strikers huwezi kumlaumu Messi hapo
 
Narudia huna akili

Kombe la Dunia ni mechi saba ligi ni mechi 30+
Messi hapimwi kwa kuchukua kombe la mechi saba tu japo amechukua
Okay kwahio cup competition haina maana ? Sawa.... ngoja nifuate logic yako ili uone kwamba hata wewe mwenyewe hujui unaongea nini au unasimamia nini ?
Pele aliogopa kwenda uropa kwasababu ushindani ni mkubwa kuliko huko kwao markani
Hivi unashindwa hata kufanya research kidogo ndugu yangu.... unaongelea kwamba Europe ndio kuna mpira kipindi cha Pele wangapi walikuwa wanatoka kwao kucheza Europe ? Na kipindi hicho ambacho Brazil ilikuwa inachukua makombe huku na kule wale wachezaji walikuwa wanacheza timu gani ? Pili unajua 1961 pele alifanywa nyara ya Serikali ili asichukuliwe ?

Unajua mambo ya ubaguzi ? Eusebio alikuwa the Best Footballer in Europe mara kadhaa ila unajua walivyokutana na timu ya Pele ilkuwaje ? Kuna kombe lilikuwa linaitwa Intercontinental Cup na hili zilicheza timu za Ulaya na South America... unajua ilikuwaje kipindi cha Pele ?

Having already won the World Cup with Brazil, he became a world champion at club level as Santos defeated Benfica to win the Intercontinental Cup in 1962, repeating the feat the following year against AC Milan. In addition to two Intercontinental Cups, Pele's Santos won the shortlived Intercontinental Supercup in 1968.


River plate au bocca ingekuwa bora ingekuwa inachukua klabu bingwa wa dunia

Tunaona kila msimu klabu bingwa ya dunia inaenda ulaya
Club Bingwa ya dunia ilianza lini ? Mkuu cheki hapo continental cup ambayo ilikuwa ni European and South American Cup kipindi cha Pele...

Pia nimekwambia hata wewe mwenyewe unajipinga..., hapo juu umesema world cup (cup competition sio kipimo) sasa club bingwa ni nini ?
 
Fact
 
Pele ni muongo muongo Ronaldo alivyofikiwa idadi ya magoli aliyo funga aka update bio ya insta kuongeza magoli ili aonekane bado anaongoza wakati mwanzo bio yake ilikua inasoma idadi ya magoli ambayo Ronaldo kayafikia.
Kwahio unadhani watu na akili zao wanatafuta stats za kina Pele kwa kutumia Instagram ya Pele ? Yaani FIFA Officially verified Stats ni Insta ya Pele ?
Kwangu Mimi Messi ndo mchezaji Bora zaidi kwanza anacheza nyakati ngumu sana hakuna magoli ya offside Kama enzi ya kina pele na maradona waliokua wanafunga hadi na mkono
Hii nishajibu mara kibao hata kwenye Post hapo juu acheni kudanganyana Offside rule imeanza tangia 1800's na pia haikuwa marginally onside bali lazima awepo jamaa kabisa mbele yako achana na sasa kwamba upo nae sambamba
 
Hiyo tu ilinifanya nimwone ni mwoga kufunikwa hahaha
 
Mnaosema eti Pele ana Worldcup tatu. Mwaka 1962 Pele aliumia kwenye Mechi ya pili na kushindwa kumalizia tournament, akina Garincha wakaibeba timu mpaka kutwaa ndoo halafu unakuja hapa kumsifu kwa Worldcup Tatu?.

Messi katwaa Copa America na alikuwa mchezaji bora wa mashindano hayo!, Pele hajawahi kutwaa Copa America!.

Messi amekuwa mchezaji bora wa mashindano ya Worldcup mbili, ya mwaka 2014 na 2022 , Pele amekuwa mchezaji bora wa Worldcup ya mwaka 1970 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…