Messi vs Ronaldo: Nani zaidi?

hilo jukumu la messi uwanjani kwamba ni kufunga magoli tu wewe nio umempa jukumu hilo? Wewe ni kocha wa barcelona?
wewe ndio unadefine jukumu la mchezaji uwanjani.

kama wewe umemua kudefine mchezji bora kwa kigezo kimoja kwamba amefunga magoli mangapi hiyo ni juu yako.
watu wanaojua wmpira hawako so closed-minded na wanaangalia vigezo vingi na wanapendelea kuangalia mpira na kuuanalyze n sio kuchukua list ya wfungaji na kuanza kupigia wtu kelele
 


Mkuu kama hujui bora upige kimya, Angalia kwenye La Liga ni nani mwenye assist nyingi zaidi?
 
Messi amechezea Barcelona misimu 11 ba CR amechezea Real Madrid misimu 6 halafu mnalinganisha magoli ya kufunga na hat trick bila kutofautisha misimu waliyocheza, CR he's the best.


Wakati mwingine ni heri ukae kimya tuu!
 

Well said Mkuu. Messi hana mfano wake. Nashukuru nimeishi katika zama za Messi, nimemuona bila kuhadithiwa.
 

Unaumwa ww,fikiria kw kutumia akili uctumie hisia kufikiria
 
unawezaje kubeza mtu mwenye assist 27!?
 
Haya sasa hivi nawawekea sttistics kutoka squawka zinazowalinganisha messi na ronaldo katika nyanja zot za mpira
sources
squawka.com na whoscored.com
 

Hivyo vigezo vingine vya kumpima striker objectively ni vipi?
 
Hivyo vigezo vingine vya kumpima striker objectively ni vipi?
Nakuletea statistics muda si mrefu kutoka whoscored, a world-renowned football statistics site n nkuonyesha vigezo vyote vinavyotumika kuanalyze wachezaji
 
unawezaje kubeza mtu mwenye assist 27!?

Assist si jukumu la msingi kwa striker, ni kitu cha ziada. Viungo ndio wanaopimwa kwa assist pamoja pass accuracy. Haiwezekani ukaacha kumpima mshambuliaji kwa kutumia kigezo cha jinsi anavyotimiza majukumu yake na badala yake ukampima kwa kutumia vitu vya ziada.

Hata hivyo kwa taarifa yako ni kwamba hata hizo assist kwa msimu huu Messi ana assist 18 na SIYO 27! na Ronaldo ana assist 16. (search hapa: La liga stats 2014-2015: Top Scorers, Assist, Clear sheets). Kwa hiyo hata kama mtu akaamua kuwa na kichwa kama cha mwendawazimu na akaziita hizo assist kuwa ni magoli basi Messi atakuwa na magoli 59 (yaani magoli 41na assist 18), na Ronaldo atakuwa na magoli 61 (yaani magoli 45 na assist 16).
Kwa hiyo hata kwa kigezo hicho cha kiwendawazimu bado RONALDO yuko juu ya Messi!
 
Hiyo inakuonyesha rankings za wachezaji msimu huu based on statistics peke yake according to whoscored.com. Tambua kuwa kila kigezo kinapewa alama sawa kwa kila mchezaji. Mfano kufunga goli inaweza ikawa inachukua 4/10, pasi ya mwisho (assist) laba 2/10 na vitu kama hivyo na average inatfutwa kwa msimu mzima. Hao nimechukua sita wa kwanza kama screen yangu ilivyoruhusu.


Kigezo cha kuwalinganisha messi na ronaldo kama mastriker na hivyo kulinganisha magoli kuwa si sawa. Hizi ni namba walizocheza messi na ronaldo, sio strikers.
Wamecheza namba tofauti sana. Hivyo kigezo cha magoli pekee hakitoshi
wamewezaje kupata hizi positions? Wamechukua heat maps. Ramani ya mchezaji alipocheza mechi nzima na kwa kila mechi wmeweza kupata average position ya mchezaji. Hivyo huwezi sema messi ni striker wakati msimu mzima amecheza namba hiyo mara nne tu kwa mfano
kama unaona hapo messi amecheza kama attacking midfielder, kiungo mshambuliaji kulia na forward wa kulia. Wakti ronaldo amechez forward na winga pia. Hivyo magoli pekee hayatoshi.
Kama unataka kutumia magoli peke yake yatumie kuwalinganisha mastriker kama aguero costa torres n falcao wanaocheza namba tisa throughout lakini si attackin midfielder/right forward kama messi




Tukitumi kigezo cha position ya forward peke yke hizi hapa chini ndizo statistics zao









.Hapa ukiachana na magoli (ronaldo anaongoza kwa magoli tu)
Messi anakimbiza statistics nyingine zote especially chances created kwamba ameweza kufunga kama yeye na ameweza kutengeneza chances kwa wenzake (neymar suarez n.k) hivyo basi kama forward ameweza kufunga magoli mengi na pia ameweza kutengeneza nafasi nyingi kwa wenzake kufunga akiwa kama attacking midfielder na nadhani ndio anongoza ulaya kwa kutengeneza key passes na nafasi za kufunga nyingi kama sikosei.

Sijaweza kuichukua hii statistic ila assist nyingi za ronaldo ni ndani ya box,(wametoa na distance from goal) wakati nyingi za messi ni za mbali zaidi na goli na ni throughballs/defence splitting passes hivyo ameweza kuonyesha uwezo wake wake wa pasi. Unaweza kucheki youtube kuhakikisha hizo assists bila tatizo.
Ukijudge messi n ronaldo kama mastriker unakosea kwa sababu asilimia kubwa wanacheza position nyingine kabisa ambpo kuna majukumu mengi zaidi n hyo inbidi ulinganishe pia
Kwa haraka haraka ronaldo anaongoza idaadi ya magoli peke yake

Messi anongoza dribbling na tena amemwacha ronaldo mbali sana na hii imeweza kumpatia . Anajaribu more dribbles per game, na anafanikiwa asilimia kubwa ya hizo dribbles na pia anaongoza kwa successful dribbles ulaya nzima akifuatiwa na hazard.

messi anaongoza kwa kutengeneza chance nyingi zaidi per game na key passes.
pia ni mmoja ya wachezaji wanaoongoza kw kutoa pass za mwisho (aidha wa kwanza au wa pili ulaya). Pia ikumbukwe mchezaji anaweza kuongoza kutengeneza chance nyingi (kama messi kombe la dunia) na kushindwa kuongoza assist kutokana na umaliziaji wa anayepokea na hilo lilikuwa tatizo first half ya msimu ambapo suarez hakuwa amerudi kiwango chake cha ufungaji.

messi anaongoza kwa kufanya tackling, angalia picha
messi anaongoza kwa magoli kupitia direct freekicks

Ronaldo anapiga more shots golini ukilinganisha magoli anayofunga kwa hivyo anahitaji shots nyingi zaidi kuweza kufunga goli moja wakati messi anahitaji shots chache, hivyo messi ana higher conversion rate kama uonavyo kwenye picha
na vingine kama utakavyoona kwenye picha

achana na hiyo, messi ameibeba barcelona hadi sasa wana nafasi kubwa kushinda makombe 3 wakati ronaldo na madrid wanaondoka bila makombe. Najua utasema neymar (japo neymar amepitwa kila kitu na messi) lakini angalia magoli mngapi ya neymr ymepatikana kutoka key passes za messi?

Halafu unafikiri wenzako kwenye kupiga kura wanasumbuka kuangalia sijui una magoli mangapi?
Wanaangalia umeibeba timu yako mpaka wapi? Umeonyesha mchezo gani. Nadhani umeona comments juu ya messi toka kwa wachezaji na wote hao ambao ndio wapiga kura wenyewe, watu wameona tangu vs man city anavyopiga watu matobo na kuwaibisha akina kompany, david luiz, boateng n.k hadi kufika fainali na kuonyesha kiwango bora kabisa (maneno ya wachezaji wenzake).

Ndio maana muda mwingne statistics hazifai kabisa. Mpira unatakiwa uuangalie na uuenjoy kwa kuona na sio kusoma idad ya magoli ni kigezo finyu sana.
Mi nna rafiki zangu kibao ambao hawamkubali messi lakini wamecheki mpira na wameona kazi yake na wamecompare na ronaldo na wameona ubora wa messi. Hiki ni kigezo muhimu sana "eye-test" na statistics huwa zinakuja kusadifu ulichokiona kwa macho

Ndio maana ukimzungumzia messi hatuzungumzii magoli kwani messi ni playmaker mkuu wa barcelona (attackin mid) kwa nini uache vigezo vyote vya uchezaji uchukue kimoja.

Halafu pia sijaweza kuchukua statistics juu ya uzito wa magoli na assists zenyewe, airtel inasumbua kukamata,
Ila wanastatistics za mpira wameweza kucount magoli muhimu.
Kwa mfano
Goli linaloipa timu ushindi, goli linalofungua scores yani toka 0-0 kwenda 1-0 n.k messi pia ameongoza hapa anyways tuachane na hizo ntazipost nikiziona tena

Hivyo ronaldo anaongoza magoli ila messi anaongoza vigezo vyote vilivyobaki na makombe juu

Ila pamoja na kuandika vyote hivi najua hautakubaliana na yote niliyoyasema na utang'ang'ania kigezo chako cha magoli sitashangaa na mimi kwa kweli sidhani kama nitapenda kuendelea kuzungumzia mpira na wewe baada ya kusumbuka sana na kuandika hii post na ile nyingine. Hivyo kila la heri katika utazamaji wako wa mpira
 
Nakuletea statistics muda si mrefu kutoka whoscored, a world-renowned football statistics site n nkuonyesha vigezo vyote vinavyotumika kuanalyze wachezaji

Kwa taarifa yako hizo statistics za ratings siyo za kisayansi na ziko too subjective. Kwa mfano mtu mmoja anaweza kutoa uzito mwingi (pointi nyingi) kwenye pass accuracy maana yeye binafsi anavutiwa na hicho, na mwingine akatoa uzito uzito mwingi kwenye tackling maana ni mshabiki wa hicho, mwingine ataegemea kwenye dribbling maana hicho ndicho kinachomkuna! Hivyo mwisho wa siku watu kumi tofauti wataalam wa mpira ukiwapa jukumu la kuwafanyia wachezaji comprehensive ratings, kila mmoja atatoka na pointi tofauti na mwenzake kwa kuwa always ratings are heavily subjective! Hata mtu akitumia kompyuta ili iwe rahisi kwake kimahesabu lakini program aliyo-feed kwenye kompyuta itakuwa subjective according to his own test which may be different from that of another expert!

Mwisho wa siku inabidi watu wakubali tu kuwa kwa striker kigezo cha magoli ndicho kigezo pekee cha kisayansi ambacho kipo totally objective! hasa kinapotumika kuwapima washambuliaji wanaocheza katika mazingira yaliyosawa kama Ronaldo na Messi. Wote wawili wanapambana na timu zile zile, na wanachangamoto ya mabeki wale wale na wakiwafunga makipa wale wale! Mtu akishindwa kwa kigezo hiki itabidi tu akubali matokeo. Itabidi tu Messi asubiri labda msimu ujao panapo majaliwa!

Ndio maana hata ballon D'Or ya FIFA iko extremly subjective! Can you image, wanaopiga kura mwisho wa siku ni makocha na ma captain wa timu za taifa! Watu wataalam kabisa wa mpira wa miguu. Kaliningrad hawajawahi kutupatia mchezaji bora aliyewahi kufikisha asilimia hamsini (50%) ya kura za wataalam hao wa soka! Kwa nini? Hivyo kimsingi hakuna mwaka ambao watu wote waliridhika na huyo aliyechaguliwa! kwa nini? Jibu ni rahisi, kigezo kinachotumika siyo cha kisayansi, kiko very subjective! Kila mpiga kura anaathiriwa na hisia zake binafsi, zikiwakilishwa na ladha binafsi, pendo binafsi, chuki bidhaa binafsi etc!

Lakini dunia haijawahi kutofautiana kuhusu nani anastahili kupata kiatu cha dhahabu! kwa nini?, jibu ni rahisi! ndicho kigezo pekee cha kisayansi ambacho kiko very objective! Hakitoi nafasi kwa hisia binafsi, pendo binafsi, chuki binafsi etc!

Hitimisho: Kwa Kuwa Messi na Ronaldo wote ni washambuliaji, wote wanacheza ligi moja- la liga, na kwa kiasi kikubwa wanatimiza majukumu yao katika mazingira yanayofanana, hawawezi kukwepa kupimwa ubora wao kwa magoli waliyofunga la liga maana hilo ndilo jukumu la msingi la striker! Zaidi ya hapo Labda mtu aende kwa mganga wa kienyeji akaulize ni nani aliye bora kati yao! Maana waganga wa kienyeji huwa hawana vigezo vinavyopimika kuthibitisha maadai yao!
 
Wanavipimo vya kitoto mashabiki wa Ronaldo, utasikia anafunga mogor ya vichwa, miguu yote anapiga…!!! Leo ukisikia Sergio Ramos kafunga gori kwa halakahalaka tu utajua kafunga gori la kichwa lakin sijui wao walikia mchezaji bora anapimwa miguu anayoitumia uwanjan…!!!! Yaan patupu kbsa
 
Japokuwa mada inazungumzia kuhusu ubora wa Ronaldo na Messi. Kwa msimu huu Barcelona naona Neymar kaisaidia timu kwa kiasi kikubwa
 

Hata magoli yapo subjective pia kwa sababu messi na ronaldo sio mastriker kama unavyotaka watu waamini.
Messi anacheza positions hizi msimu huu: right forward, attacking midfielder, center forward na sio striker. Nimeangalia mechi zote za barcelona na suarez ndio anacheza nafasi hiyo sometimes neymar, messi anacheza nyuma zaidi. Cheki heat map yake halafu linganisha na ya striker kama costa halafu uone unavyozingua kuwaita wote strikers ili na wewe upate nafasi ya kuongea.
Strikers chukua hao akina costa, sijui drogba aguerro benzema suarez, hawa ndio wanaocheza kama strikers na tunawalinganisha kwa magoli tu kwa sababu ndicho pekee wanachofanya uwanjan.
Lakini messi anacheza kama attackin midfielder anayeanzia kulia au kati na ndiyo maana tunampima kwa magoli,dribbling, chances created, key passes, n.k

Ronaldo anacheza left of a forward, left wing forward au centerforward depending na match. Kwa hiyo tusahau kabisa kama kutokana na kuwa wing forward pia anatategemewa atengeneze nafasi za kufunga?
Mpira hauko shallow hivyo, positions haziko fixed kama unavyosema.
Kwangu mimi vigezo vya magoli,assists, dribbles, chances created, number of touches, key passes, throughballs kwa sababu naangalia mpira, naona roles ambazo ronaldo na messi wanaplay uwanjani

Na sidhani kama umesoma post yangu yote hapo juu, sijui ndio uvivu wa watanzania kusoma ukaishia kusoma paragraph moja tu. Hiyo inayozungumzia statistics zote kwa hiyo inaonesha kabisa hmna haja ya kuwa na a pointful discussion ila wewe lengo ni kuja hapa kutuaminisha hizo propaganda zako na huna lengo la kusikiliza mtu yoyote kujua wao wao wanaonaje.
So mkuu umeingia kwenye my ignore list kiroho safi tu
 
Japokuwa mada inazungumzia kuhusu ubora wa Ronaldo na Messi. Kwa msimu huu Barcelona naona Neymar kaisaidia timu kwa kiasi kikubwa

Neymar magoli mengi anayofunga unakuta source ni Messi. Sio Neymar tuu hata nafasi nyingi za kufunga kwa Barca wanazofunga ni Messi ndiye anayetengeneza hizi Nafasi.
 

Mkuu, mimi nimeshaongea muda kuwa Messi na Ronaldo sio mastriker. Na katika hili jamaa kajidhihirisha kuwa hana lolote analofahamu kuhusu mengi ya uwanjani.
Messi ni kiungo, na Ronaldo pia ni kiungo. Hakuna Striker yoyote atakaeenda Madrid na akawika endapo Ronaldo atakuwepo pale, Ronaldo ndiye aliyepewa jukumu la kufunga pale. Madrid wanafanya usajili wa sehemu zingine ila sehemu ya Striker ni tatizo. Striker mwenye akili timamu hawezi kwenda Madrid, sababu wanahofia ubinafsi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…