
Hiyo inakuonyesha rankings za wachezaji msimu huu based on statistics peke yake according to whoscored.com. Tambua kuwa kila kigezo kinapewa alama sawa kwa kila mchezaji. Mfano kufunga goli inaweza ikawa inachukua 4/10, pasi ya mwisho (assist) laba 2/10 na vitu kama hivyo na average inatfutwa kwa msimu mzima. Hao nimechukua sita wa kwanza kama screen yangu ilivyoruhusu.



Kigezo cha kuwalinganisha messi na ronaldo kama mastriker na hivyo kulinganisha magoli kuwa si sawa. Hizi ni namba walizocheza messi na ronaldo, sio strikers.
Wamecheza namba tofauti sana. Hivyo kigezo cha magoli pekee hakitoshi
wamewezaje kupata hizi positions? Wamechukua heat maps. Ramani ya mchezaji alipocheza mechi nzima na kwa kila mechi wmeweza kupata average position ya mchezaji. Hivyo huwezi sema messi ni striker wakati msimu mzima amecheza namba hiyo mara nne tu kwa mfano
kama unaona hapo messi amecheza kama attacking midfielder, kiungo mshambuliaji kulia na forward wa kulia. Wakti ronaldo amechez forward na winga pia. Hivyo magoli pekee hayatoshi.
Kama unataka kutumia magoli peke yake yatumie kuwalinganisha mastriker kama aguero costa torres n falcao wanaocheza namba tisa throughout lakini si attackin midfielder/right forward kama messi
Tukitumi kigezo cha position ya forward peke yke hizi hapa chini ndizo statistics zao



.Hapa ukiachana na magoli (ronaldo anaongoza kwa magoli tu)
Messi anakimbiza statistics nyingine zote especially chances created kwamba ameweza kufunga kama yeye na ameweza kutengeneza chances kwa wenzake (neymar suarez n.k) hivyo basi kama forward ameweza kufunga magoli mengi na pia ameweza kutengeneza nafasi nyingi kwa wenzake kufunga akiwa kama attacking midfielder na nadhani ndio anongoza ulaya kwa kutengeneza key passes na nafasi za kufunga nyingi kama sikosei.
Sijaweza kuichukua hii statistic ila assist nyingi za ronaldo ni ndani ya box,(wametoa na distance from goal) wakati nyingi za messi ni za mbali zaidi na goli na ni throughballs/defence splitting passes hivyo ameweza kuonyesha uwezo wake wake wa pasi. Unaweza kucheki youtube kuhakikisha hizo assists bila tatizo.
Ukijudge messi n ronaldo kama mastriker unakosea kwa sababu asilimia kubwa wanacheza position nyingine kabisa ambpo kuna majukumu mengi zaidi n hyo inbidi ulinganishe pia
Kwa haraka haraka ronaldo anaongoza idaadi ya magoli peke yake
Messi anongoza dribbling na tena amemwacha ronaldo mbali sana na hii imeweza kumpatia . Anajaribu more dribbles per game, na anafanikiwa asilimia kubwa ya hizo dribbles na pia anaongoza kwa successful dribbles ulaya nzima akifuatiwa na hazard.
messi anaongoza kwa kutengeneza chance nyingi zaidi per game na key passes.
pia ni mmoja ya wachezaji wanaoongoza kw kutoa pass za mwisho (aidha wa kwanza au wa pili ulaya). Pia ikumbukwe mchezaji anaweza kuongoza kutengeneza chance nyingi (kama messi kombe la dunia) na kushindwa kuongoza assist kutokana na umaliziaji wa anayepokea na hilo lilikuwa tatizo first half ya msimu ambapo suarez hakuwa amerudi kiwango chake cha ufungaji.
messi anaongoza kwa kufanya tackling, angalia picha
messi anaongoza kwa magoli kupitia direct freekicks
Ronaldo anapiga more shots golini ukilinganisha magoli anayofunga kwa hivyo anahitaji shots nyingi zaidi kuweza kufunga goli moja wakati messi anahitaji shots chache, hivyo messi ana higher conversion rate kama uonavyo kwenye picha
na vingine kama utakavyoona kwenye picha
achana na hiyo, messi ameibeba barcelona hadi sasa wana nafasi kubwa kushinda makombe 3 wakati ronaldo na madrid wanaondoka bila makombe. Najua utasema neymar (japo neymar amepitwa kila kitu na messi) lakini angalia magoli mngapi ya neymr ymepatikana kutoka key passes za messi?
Halafu unafikiri wenzako kwenye kupiga kura wanasumbuka kuangalia sijui una magoli mangapi?
Wanaangalia umeibeba timu yako mpaka wapi? Umeonyesha mchezo gani. Nadhani umeona comments juu ya messi toka kwa wachezaji na wote hao ambao ndio wapiga kura wenyewe, watu wameona tangu vs man city anavyopiga watu matobo na kuwaibisha akina kompany, david luiz, boateng n.k hadi kufika fainali na kuonyesha kiwango bora kabisa (maneno ya wachezaji wenzake).
Ndio maana muda mwingne statistics hazifai kabisa. Mpira unatakiwa uuangalie na uuenjoy kwa kuona na sio kusoma idad ya magoli ni kigezo finyu sana.
Mi nna rafiki zangu kibao ambao hawamkubali messi lakini wamecheki mpira na wameona kazi yake na wamecompare na ronaldo na wameona ubora wa messi. Hiki ni kigezo muhimu sana "eye-test" na statistics huwa zinakuja kusadifu ulichokiona kwa macho
Ndio maana ukimzungumzia messi hatuzungumzii magoli kwani messi ni playmaker mkuu wa barcelona (attackin mid) kwa nini uache vigezo vyote vya uchezaji uchukue kimoja.
Halafu pia sijaweza kuchukua statistics juu ya uzito wa magoli na assists zenyewe, airtel inasumbua kukamata,
Ila wanastatistics za mpira wameweza kucount magoli muhimu.
Kwa mfano
Goli linaloipa timu ushindi, goli linalofungua scores yani toka 0-0 kwenda 1-0 n.k messi pia ameongoza hapa anyways tuachane na hizo ntazipost nikiziona tena
Hivyo ronaldo anaongoza magoli ila messi anaongoza vigezo vyote vilivyobaki na makombe juu
Ila pamoja na kuandika vyote hivi najua hautakubaliana na yote niliyoyasema na utang'ang'ania kigezo chako cha magoli sitashangaa na mimi kwa kweli sidhani kama nitapenda kuendelea kuzungumzia mpira na wewe baada ya kusumbuka sana na kuandika hii post na ile nyingine. Hivyo kila la heri katika utazamaji wako wa mpira