Messi vs Ronaldo: Nani zaidi?


Uko deep mkuu
 

Ni kweli kabisa.
Huyo jamaa hapo juu sijui anaitwa mbingunikwetu
Hawezi kutofautisha kato ya forward, attacking midfielder, false nine na striker.
Anaona kila anayefunga magoli mengi ni striker.
Anawalinganisha eti messi ronaldo kuwa wanacheza role sawa na wachezaji kama costa, aguerro, mario gomez, lewandowski role ya striker ambayo si kweli, nimemwekea stats kuhusu player positions, kuhusu heat maps lakini bado mtanzania hataki kuzisoma ili ajiweke informed maana anajiaibisha na kionesha jinsi asivyojua mpira lakini as any other fool hataki kujifunza labda aone kwa nini natofautiana kimawazo na kundi kubwa la watu.
Mi nimeamua kumuignore maana hamna namna nyingine, nangoja nikiweka bundle kwenye tablet
 
Nashukuru mkuu lakini it's all for nothing unatumia muda kukusanya statistics lakini wala mtu hasomi.
Eti messi na ronaldo ni mastriker, labda mnisaidie nyie wenzangu mnaoangali mpira

While using your mind argue some people using their chests so wazoee mkuu ndo hali zao
 
hizo ni assists za season yote hadi uefa na makombe mengine. ambapo messi ana 27 na cr7 22. kuwa na vitu vya ziada ndiyo hufanya mchezaji kuwa bora. dani alves ni beki lakini mda fulani unaweza dhani ni winga.
 
Mtu yeyote wa mpira ukimuangalia Messi anavyocheza walahai unaburudika.
 

Wachezaji ndani ya uwanja wanaweza kugawanywa katika makundi makubwa matatu kulingana na majukumu yao 😀efenders, midfielders na strikers. Japo katika kila kundi kuna sub-classification, kwa mfano, midfielders wanagawika kama defensive midfielder, attacking midfielder, holding midfielder kulingana na uwezo wa mchezaji. Hali kadhalika kwa washambuliaji, wanagawika kama central striker ambaye hushambulia kutokea katikat na kuna washambuliaji wa pembeni wenye uwezo wa kushambulia kutokea pembeni. Lakini Kwa soka la kisasa wote ni washambuliaji! Jinsi washambuliaji watakavyojipanga hiyo inategemea formation aliyochagua kocha kulingana na game plan ya siku husika. Anaweza kuamua kutanguliza striker mmoja na wengine wakawa nyuma yake. Kwamba wako nyuma ya mwingine haijawafanya wasiwe strikers bali kocha ameona kwa kuwapanga hivyo watafanikiwa kutimiza malengo waliyojipangia kwa game husika. Hebu angalia jinsi wachezaji huwa wanatambulishwa kwenye tv kabla ya kila mechi, wanatambulishwa kwa category hizo tatu, na messi hutambulishwa kwenye category ya strikers sambamba na suarez na neymar! bisha na hilo! kama umesahau subiri mechi ya barca na Juventus ujionee! Soka la kisasa ni tofauti na la kizamani ambapo ukisikia striker maana yake ni centre forward! Hata hivyo hoja yetu ya msingi siyo hiyo!
 
Ronaldo hawezi shindana na messi...ashindane na akina Bale,Teves,Van persi,Diego costa,Torres,Muller nk,watu wazito katika soka duniani wote wanamkubali messi hata kwa kuwaangalia tu on the pitch..Pep guardiola anaamini messi anaweza linganishwa na ma Greatest yaani akina Pelle na Diego maradonna...
 

Naona bado haujanielewa! Sitachoka kujieleza!
Kwanza kwa dhati kabisa nikushukuru kwa jinsi ulivyoshiriki mjadala huu ulioanza siku nyingi, hivyo uko kwenye rekodi ya wachangiani makini.
Pili naomba nieleweke kuwa sisemi kwenye mpira hakuna vigezo vingine vya kuangalia uhodari wa mchezaji zaidi ya magoli kwa wachezaji hususani strikers! Data ulizoweka si tu kwamba nimezisoma sambamba na post yako, lakini pia nimeingia mwenyewe kwenye website uliyotumia nikajisomea kwa hamu! Nikajiridhisha kuwa ulichopost ndicho hicho.
Suala ambalo ninasema ni kwamba vipengele vingine vya uchezaji japo vipo, namna yake ya kuvipima inaathiriwa na subjectivity! Kwa manufaa ya wale ambao wanaweza kuwa hawafahamu ninamaanisha nini kusema hiyo subjectivity japo nafahamu Kuwa hakuna hilo tatizo kwako.
Tuchukuwe kipengere kimoja cha dribbles kama mfano. Ili upime kipengere hiki lazima kusi-asign point weight na ukadirie mchezaji anafikisha pointi ngapi kati ya zile ambazo umeasign! Hiyo ndiyo falsafa ya ratings. Kipimo hicho kitatoa pointi tofauti kulingangana na mtu anayefanya hiyo rating! Kipimo kinachotoa majibu tofauti kulingana na watu tofauti wanaokitumia, kipimo hicho kipo subjective, hakiwezi kupima kwa haki bila kuathiriwa na vionjo tofauti vya wapimaji! hakiwezi kuwatendea haki wapimwaji. Ni sawa na kutumia mzani unaotoa uzito tofauti kwa watu tofauti wanaoutumia kupimia! Hakuna atakayepimwa na mzani huo akaweza kutendewa haki!
Hivyo pamoja na uzuri wa dribbling kwenye soka, hakuna namna ya kukipima kipengere hicho Kiasi ambacho wapimaji 100 wote watoke na figure moja. Mmoja aweza kumpa mchezaji 8/10, na mwingine 7/10, mwingine 9/10 nk. Maana hakuna namna ya kukiweka kipengere hiki kwenye mzani na ukapata uzito mmoja bila kujali kama huyo mchezaji unampenda au vinginevyo! Kama unaweza njoo hapa ueleze nami nitakushukuru.
Data nyingi ulizotoa kutoka tovuti uliyotumia zilipatikana kwa njia hiyo, na summary yake ikatoa ratings kwa wachezaji mbalimbali. Wala hawajaficha, wanaziita ratings! Ten raters comes up with ten different ratings!

Lakini pia umenishangaza kwa mambo mawili: 1. Unasema Messi siyo mshambuliaji wakati hizo chati ulizopost zinaainisha pia position ya wachezaji husika! Messi ameainishwa kama forward - right, yaani mshambuliaji wa kulia na Ronaldo ameainishwa kama forward - left! yaani mshambuliaji wa kulia. Zisome tena! 2. Umesema hata kigezo cha magoli ni subjective! Kama ni hivyo maana yake ni kwamba watu 10 waliomtazama Messi mechi yake iliyopita ukiwauliza Messi alifunga magoli mangapi, kila mtu atatoa jibu tofauti na mwenzake!
Tunasema kigezo cha magoli ni objective tukimaanisha kuwa wote tutakuwa na jibu moja kuwa Messi alifunga goli moja na Ronaldo alifunga magoli matatu mechi Iliyopita bila kujali kama tunawapenda au vinginevyo! Kigezo cha magoli kinatenda haki!
 
Mtu yeyote wa mpira ukimuangalia Messi anavyocheza walahai unaburudika.

Ni sawa unaburudika, lakini huko kuburudika hakupimiki, kiasi cha kuja na kiwango cha kuwalinganisha wachezaji wawili! Mwingine anaburudishwa zaidi na vitu vya mchezaji mwingine kuliko huyo wa kwako! Hii inatokana na watu kutofautiana vitu vinavyotuburudisha kutokana na mpira wa miguu na hilo halipingiki.
Ndiyo maana ni vigumu kuwalinganisha wachezaji wawili kwa kutumia vigezo vya hisa binafsi isiyopimika!
Hoja yangu ya msingi siyo Messi haburudidhi lakini ni kuwa huko kuburudisha ambayo hakuwezi kupimika hakuwezi kutumika kama kigezo cha kuwalinganisha wachezaji wawili kwa haki bila kuathiriwa na hisia binafsi za mtu anayepima!
Magoli ndio kipimo sahihi kisichokuwa na upendeleo na hakiathiriwi na hisia zetu binafsi zinazotofautiana sana! Mawazo yako tutayaheshimu kama mawazo binafsi, kama na wengine walivyo na mawazo binafsi tofauti na ya kwako.
Lakini kwenye magoli hakuna mawazo binafsi! mtu apende asipende atalazimika kukubali magoli Ya mchezaji husika hata kama hapendi!
Kama striker ana stadi za ziada basi tuone zikimsaidia kufumania nyavu!
 
Nadhani. Sikueleza vizuri baadhi ya statistics ndio maaana umepata maana tofauti


tuanze hpo kwenye dribbling, hizo sio marks wlizotoa wenye site. Hizo ni statistics ya number of dribbles ambazo messi/ronldo hujaribu per match, idadi ya hizo dribbles ambazo mwisho wa dribbles mchezji anakuw meweza kuretain mpira au kutoa pasi bila kuupoteza (successful dribble/take-on) Na asilimia y hizo dribbles ambazo zilifanikiwa. Kwa hiyo km unvyooona hiki sio kipimo ch mtu kukaa na kuamu n kusema ngoja tumpe messi 8 u ngpi, ni actual idadi ya dribble anachocheza kwenye mechi. Kwa hiki ni kipimo objective kabisa.
Kama messi anajaribu more dribbles, anafanikiwa katika nyingi zaidi na asilimia kubwa na tuna idadi ya namba za hizo dribbles kwa nini tusizitumie kumpima mchezaj


Kigezo cha magoli kinaeleweka
Kigezo cha assist kinaelewek
Kiigezo cha key passes na secondary assists na chances created per game ndhani kipo clear, ni idadi y nafasi zaa kufunga ambazo mchezaji anatengeneza per match na hizi zinahesabiwa pia per mtch hivyo ni objective kbisa na wala unachoona hapo siyo marks za mwandishi, balo ni statistics za uwanjani


Sijasem messi siyo mshambuliaji. Nimesema messi siyo striker.
Messi ni mshmbuliaji=attackers, na kigezo cha kuwa mshambuliaji kinahusisha attacking midfielders, wing forwards, centre forwards n strikers. Strikers unaosema wewe ni nmb tisa n hao ndio kazi yao ni kufunga magoli
Cheki description yake wikipedia
Association football positions - Wikipedia, the free encyclopedia
Ona hapa kwenye forward wanasema hivi "Forwards (or strikers) are the players who are positioned nearest to the opposing team's goal. The primary responsibility of forwards is to score goals and to create scoring chances for other players. Forwards may also contribute defensively by harrying opposition defenders and goalkeepers whilst not in possession. The most common modern formations include between one and three forwards; for example, a lone striker in a 4–2–3–1, paired strikers in a 4–4–2 or a striker and two wingers in a 4–3–3"
Kazi za forward "kufunga magoli, kutengeneza chances, na pia defensively ndio mana unaona nimeweka pia tackles per game". Hapo ronldo anongoza kigezo kimoja tu kati ya hivyo.


Lkini pia kama umeangalia vizuri hapo utaona kuwa messi na ronaldo wamekuwa outlined kama attacking midfielders kwenye zile picha.
Kazi zao kama attacking midfielders kulingana na article na messi anaangukia katika role ya "false nine"/trequartista ambapo mara kwa mara anarudi nyuma na kucheza nyuma ya suarez n neymar n yeye huwa kiungo kulink viungo waliopo nyuma yake na maforward walio mbele yake. Kama umeangalia mechi z barcelon utakubalina na hili


Kazi za trequartista kama quote yao ni "Some attacking midfielders are called trequartistas or fantasisti (Italian: three-quarter specialist, i.e. a playmaker between the forwards and the midfield), known for their deft touch, vision, ability to shoot from range, and passing prowess; however, not all attacking midfielders are trequartistas – some attacking midfielders are very vertical and are essentially auxiliary attackers. Where a creative attacking midfielder is regularly utilised, he is commonly the team's star player, and often wears the number 10 shirt. As such, a team is often constructed so as to allow their attacking midfielder to roam free and create as the situation demands. "
Ona jinsi maelezo haya yanavyosadifu uchezji wa messi uwanjani.


Tuje kwa false nine ambayo ni role ya messi pale barca misimu. Mingi iliyopita hii ni two in one, yani kama centre forward na attacking midfielder
"


A false nine is a player who appears to be playing as a centre-forward (traditionally a number nine shirt), but drops deeps or pulls wide disrupting the opposing team's marking. Usually the centre forward will be marked by one of the centre-backs but the false nine will often move away into a grey area causing a dilemma on whether the centre-back follows, isolating them from the other centre-back or stays where they are, making themselves redundant"


Nadhani umeona role anayocheza messi. Messi ni mshambuliajji (attacker), ni forward ila siyo striker ambayo hutumika kumwelezea (traditional centre forward ila ni false nine centre forward


Hivyo naomba utambue kuwa vigezo vya
1. Assist ni objective, zinahesabika na statistics zipo. Messi anaongoza hapa
2. dribbles ni objjective na ina statistics zake per game, per season,
Kukuonyesha kuwa ni objective
Kwa haraka haraka mechi ya barca vs atletico camp nou messi aliattempt dibbles 15 na kucomplete 12 hivyo 75% percent, na unaweza kupata kwa msimu mzima. Messi amemwach ronaldo mbli kwa hili


3 chances created, key passes zote zinahesabika kama watu wanvyohesabu pasi au magoli kwenye mechi.


4. Tackles nazo zinapimwa kwa mechi n messi amemuaacha ronaldo hapo pia
5 vision ya mchezaji inapimwa kwa throughballs, uwezo wa kupiga pasi zinazoweza kugawa walinzi wa mpinzani. Ingia whoscored wamekupimia throughballs ambazo mchezaji anapiga kwa mechi na hizo huwa zinahesabiwa pia ndani ya mechi


Mkuu hapo whoscored kigezo pekee ambacho wanatoa marks wao ni hicho cha rating na wanatoaje marks. Mfano ukiweza kufunga goli unapewa point moja, hivyo messi kifunga 5 napewa tano, ukiweza kucomplete one dribble unapewa point 0.5 hivyo messi akicomplete 4 anapewa point 2, ronldo akicomplete mbili anapewa point 1. Hizo ni ratings pekee.


Kama ronaldo amemshinda messi ni kwa kigezo cha goals scored pekee na kama unavyoona hapo messi anakimbiza karibu vigezo vyote, tumia whoscored au squawka.
Na vigezo vyote vinapimika vizuri katika mechi.


Lakini achana na yote hayo, messi yupo on course kushinda makombe 3 wakati ronaldo hajafanikiwa kupata kombe hata moja
Huku messi akionyesha kiwango kizuri vs team ngumu


Pia usisahau
mshambuliaji ni attacker
attacker=forwards+attacking midfielders+strikers
Ni hayo tu
 
mkuu,unajua kila kitu au mtu lazima awe na mshindani hata shetani mshindani wake ni mwenyezi mungu bt kama tujuavyo lazima atakuwepo mwingine bora zaidi.

hata ukitumia simple analysis tu,kwa kutambua idadi ya magoli mengi na tuzo nyingi toka wameanza soka huyo CR7 hajawahi na hata kuja kumzidi mess. kingine ni namna ya magoli wanavyofunga,faulo,penalty chenga huyo CR7 hamfikii mess hata kidogo.

labda uniambie CR7 anamzidi mess kwa kitu gani??????,kinacho msaidia CR7 mpaka wanajaribu ku mlinganisha na mess ni idadi ya magoli aliyo yafunga misimu ya karibuni hamna kingine.

na bado tuzo ya mchezaji bora wa ballon d`or ya mwaka kesho anachukua kirahisi sana. CR7 HANA TOFAUTI NA BALE,ROONEY anacho wazidi ni magoli tu.hata James rodrigues ni bora kuliko huyo CR7 wako
 
kaka wanabishana tu,hayo magoli ambayo CR7 anamzidi mess in baadhi ya misimu tu.tena ukianza kufany analysis kupitia takwimu za soka huyo ronaldo hamfikii mess hata kidogo kwa chochote ronaldo anamzidi mess mbio tu za kukimbia na mpira akiwa anakwenda kufunga na magoli ya vichwa hamna kingine.
 
neymar kaisaidia timu ni kweli,ila neyma kasaidiwa sana na mess kuisaidia timu
 
Cristiano ronaldo level zake ni neymar jr, if u'r sound mind u can compare messi from cr7, coz messi is a magic person. Me ntamuelewa mtu anaesema cr7 vs neymar jr.
 

Nikushukuru tena kwa kuendelea kuchangia kwa hoja. Uungwana ni kujibu hoja kwa hoja.
Kwa hiyo nami nichukue fursa hii kujibu hoja zako: Naona nianze kwa kutumia mfano ili wadau wanipate vizuri zaidi. Kuna watu wawili ambao ni wafugaji wa mifugo mbali mbali. Mmoja (A) ana kuku 6, bata 3, mbuzi 4, na kondoo 6. Mwingine (B) ana kuku 2, bata 7, mbuzi 8, na kondoo 1. Ukatokea ubishi nani ni tajiri zaidi kati ya A na B. Watu wakaanza mjadala. Mmoja akasema tujumlishe hiyo mifugo tuone nani ana mifugo mingi. Mwingine akamjibu kuwa kanuni ya hesabu hairuhusu kujumlisha kuku na mbuzi nk kwa sababu hivyo vina thamani tofauti. Mwingine akasema kama ni hivyo tuvithamanishe kwa fedha ili tupate jumla ya thamani ya mifugo ya kila mmoja. Yule atakayekuwa na thamani kubwa ya kifedha kwa mifugo yake huyo ndiye tajiri zaidi!. Mwingine akajibu ni wazo zuri lakini tatizo watu tofauti wanathamanisha tofauti kwa aina moja ya mifugo. Mtu mmoja anaona bata ana thamani zaidi kuliko kuku kulingana na jinsi anavyoifurahia nyuma ya bata mpaka kuna msemo wa "naona unakula bata". Kwa mwingine anaona hata kama ukimpa bata wa bure, atachukua tu kwa kukuheshimu lakini hawezi kutoa pesa yake kununua bata hata kama bei ni karibu na bure! yuko tayari kununua kuku mmoja kuliko kununua bata kumi kwa pesa hizo hizo alizonunulia kuku mmoja! Hapo kwenye kuthamanisha mifugo ili tupate kigezo cha Kulinganisha utajiri wa A na B ndipo pameshindikana kutokana na subjectivity! Idadi ya kila aina ya mfugo kwa kila mmoja haina tatizo maana idadi hiyo inapatikana objectively! Lakini idadi hiyo haitoshi kujibu swali letu la nani ni tajiri zaidi ya mwenzake kwa sababu ya hisia tofauti kwa watu tofauti juu ya thamani ya kila mfugo. Na tofauti hizo hazikwepeki kwenye jamii! Swali linakuja, je katika mazingira haya swali la nani ni tajiri zaidi ya mwenzake kwa kigezo cha mifugo yao halijibiki? Kwangu mimi mbingunikwetu linajibika bila utata, kwa vipi? nasema ni kama ifuatavyo: Kwanza tuangalie wahusika wenyewe wanaitumiaje hiyo mifugo, kama matumizi yao ni sawa tuangalie tija ya mifugo ya kila mmoja kwenye hayo matumizi. Hawa watu tukagundua kila mmoja ana akaunti ya benki ambapo huwa anaweka pesa zitokanazo na mauzo ya mifugo yao wanayouza wenyewe kwa bei WALIYOPANGA WENYEWE! Sisi tutaamua nani tajiri kwa mujibu wa SALIO la BENKI la kila mmoja,. Mwenye salio kidogo hawezi kulalamika kwa sababu aliuza mwenyewe kwa bei aliyopanga mwenyewe!

Hali kadhalika messi na Ronaldo ni kama hao wafugaji wawili, wanafuga mifugo ile ile ila kwa idadi inayotofautiana! Yaani wote wana football skills mbali mbali kwa viwango tofauti! Mmoja ana skill fulani kwa kiwango kikubwa kuliko mwenzake. Lakini huyo mwenzake pia ana vitu(skills) fulani kumzidi huyo wa kwanza! Kila mmoja ana haki ya kuona skills anazozidi zina thamani zaidi kuliko zilizopungua.
Hizi skills mbali mbali nakubaliana na wewe kuwa zinapimika objectively kama vile ambavyo kila aina ya mfugo inapimika objectively! Tatizo linakuja kwamba ili hizi skills mbali mbali ziweze kutumika kutupa jibu la swali kwenye uzi huu la nani ni zaidi kati ya messi na Ronaldo ni lazima tupate namna fulani ya kupata jumla ya thamani ya skills hizi kwa kila mmoja! Hapo ndipo subjectivity kwenye suala zima linapoingia! Hizi skills japo idadi yake inapatikana objectively, thamani ya kila skill haiwezi kupatikana objectively! HOJA yangu iko hapo ndugu yangu gasgas! Huwezi kujumlisha skills mbali mbali ili upate kigezo cha kulinganisha kama vile ambavyo huwezi kujumlisha kuku na mbuzi maana kwa hakika vina thamani tofauti! Swali linakuja, je katika mazingira haya hatuwezi kujibu swali la nani ni zaidi? Kwangu mimi mbingunikwetu swali linaweza kujibika bila utata! Kwa vipi?, ni kama ifuatavyo: Kama tulivyofanya kwenye mifugo, tuangalie wao wenyewe messi na Ronaldo kama forwards kwenye timu zao hizi skills wanazitumia ili iweje? Zinawapa tija ipi? Bila ubishi wachezaji wote wawili ni wafungaji wazuri wa magoli. Je wanatumia nini kufunga magoli? Jibu ni rahisi, wanatumia hizi football skills zao! Kama kuna mtu anabisha kuwa wanatumia football skills aje hapa atuambie wanatumia nini! Kumbe football skills hasa kwa forwards kama messi na Ronaldo zaweza kupata thamani na tija inayopimika kwa njia ya magoli! Kama yeyote kati ya messi na Ronaldo anaona skills zake zina thamani zaidi ya zile za mwenzake basi aziuze skills hizo MWENYEWE kwenye MECHI kwa gharama ya magoli nasi tutaona na kukubali hata kama hatupendi thamani ya skills hizo kwenye score bord! Zikipata thamani kidogo kuliko za mwenzake asilalamike maana aliziuza MWENYEWE kwenye mechi kwa bei aliyojipangia mwenyewe!
Vinginevyo hakuna njia nyingine ya kuthaminisha skills kama dribbles, tackles, shots accuracy, passing accuracy etc objectively japo idadi yake yawezekana kupatikana objectively! Hata kwenye hiyo website uliyopata statistics za wachezaji hawa, wametumia ratings kupata nani aweze kuwa juu ya mwenzake, na ratings zote tunakubaliana zinapatikana subjectively, ndiyo maana utasikia maneno kama "mchezaji fulani yuko over-rated". Halafu skills zingine zote kila skill iko peke yake na idadi yake, kama vile idadi ya mifugo. Ndiyo maana kuna chati nyingi kila chati ikionyesha skill moja! Sina tatizo na chati hizo.

Hitimisho: Kigezo cha magoli ndicho kigezo pekee ambacho tunaweza kuwapima messi na Ronaldo kwa kuwa wote ni fowards kwenye timu zao na wote hutumia skills zao kufunga magoli! Na kwa sasa mwenye magoli mengi la liga ni Ronaldo, Hivyo kwa sasa Ronaldo ni zaidi ya Messi, hitimisho ambalo ni very Objective! Mwenye kigezo kingine kilicho "objective" yaani hakitegemei hisia na utashi binafsi tuletee hapa!
 

uko sahihi mkuu hao wengine wanaomsifia ronado wanatapatapa MESSI KAMA MAJI USIPOYANYWA UTAYAOGA USIPOYAOGA UTAYAFULIA N.K
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…