Kuna namna mbili za maoni ulimwenguni: subjective na objective. Objective ni yale ambayo usahihi wake ni mmoja tu; kama kuna kauli mbili tofauti juu ya jambo hilohilo moja, basi angalau mojawapo (au hata zote) lazima itakuwa sio sahihi. Ni objective kwa sababu object ya maoni hayo ni moja tu. Mfano, 2x2=4. Yeyote anaydhani jawabu sio nne, amekosea. Lakini subjective opinion ni ile ambayo kunaweza kuwa na maoni hata alfu juu ya jambo hilohilo moja, na yote yakawa sahihi kulingana na hoja zilizojengwa. Ni subjective kwa sababu kila subject wa hoja hiyo anaweza kuwa na maoni tofauti. Kwa mfano, ni kipi chakula kitamu baina ya sembe na biriani. Kila mmoja anaweza kutoa maoni tofauti yaliyo sahihi kwa mujibu wa atavyojenga hoja yake. Hili la Messi na Ronaldo ni subjective, ingawa kuna kasoro kidogo kwenye ujenzi wa hoja husika. Sawa mmoja kafunga magoli mengi zaidi ya mwenzake au katoa pasi za mwisho nyingi zaidi ya mwenzake. Lakini wanachezea timu tofauti! Jaalia Messi angekuwa akichezea Madrid, angefanya vyema kama anavyofanya Ronaldo huko? Na kinyume chake je? Huyu mmoja ameshaonyesha uwezo akiwa na klabu mbili za nchi mbili tofauti. Je na huyu aliyechezea klabu moja ya nchi hiyohiyo moja akihamia klabu ya nchi nyingine atafanya kama alivyofanya mwenzake? n.k. Sina upande kwenye hili, ila ni kusaidia tu kutoa tanbihi (tahadhari) ya kuliangalia swala lenyewe (na malumbano yote mengine kwenye nyanja zote nyingine) kwa mtizamo ulio sahihi zaidi.