Mkuu so unazungumzia mfungaji na mchezaji bora au? Maana leo nikikuambia unipe record ya Zidane kama alishawah chukua kiati cha dhahabu ila kwann alichukua uchezaji bora?
Mess magori anayofunga yana akil kuliko anayofunga Ronaldo, Ronaldo anafunga magori easy kabisa ambayo ata Sergio Ramos ila angalia anavochukua mpira Mess na kwenda kiweka kimiani utaona utofauti wa Mess na Ronaldo.
Jana nilikuwa na angalia mpira na mshabiki mkubwa wa Ronaldo lakin alikubali kuwa Mess ni zaid ya Ronaldo huku akitumia neno la utani (Mess kweli yule jamaa Zombie) na kunalizia kuwa Ronaldo amepata bahati ya kufunga tu lakin kimsingi hamfikii Ronaldo
Unapolinganisha wachezaji wawili lazima kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Utumie kigezo kinachopimika ili kuondoa subjectivity!
2. Wachezaji wawe na majukumu yanayolingana.
3. Wachezaji wawe katika mazingira yanayofanana kwa Kiasi kikubwa.
Ni halali kuwalinganisha Messi na Ronaldo kwa kutumia magoli kwa sababu ndicho kigezo pekee kinachopimika na ndiyo majukumu ya wote wawili kama washambuliaji ambayo ni kufunga magoli! Na pia wako katika mazingira yanayofanana kwa Kiasi kikubwa maana wote wanacheza ligi moja (la liga), na magoli yao wanayapata kwa kucheza na timu zile zile, wakipambana na mabeki wale wale!
Zaidi ya kutumia magoli huwezi kupata kigezo kingine ambacho ni objective! Vinginevyo watu tunatofautiana kuhusu ladha tunayopenda, usipotumia objective criteria kila mtu atakuja na hisia zake anazoziamini yeye!
Ndiyo maana timu inayoondoka na pointi tatu muhimu ni ile iliyopata magoli mengi kuliko timu pinzani na hakuna ubishi katika hilo maana kila timu iliingia uwanjani ikiwa na jukumu moja la msingi ni Ushindi kwa kigezo cha magoli. Vigezo vingine vyote havipimiki hivyo havina msaada katika kumpata mshindi pasipo ubishi!
Kwa hiyo kwa sasa Ronaldo ni bora kuliko Messi, Messi ana magoli 41 katika mechi 37, wakati Ronaldo ana magoli 45 katika mechi 34!
Habari ingekuwa nyingine kabisa kama Ronaldo angefanikiwa kucheza mechi zote!
Ndio maana mashabiki wa Messi kwa kuzidiwa hoja na vigezo vya kitaalam wanaishia kutoa kejeli na matusi!
Kuhusu
Kuhusu Zidane si haki kumlinganisha Zidane na hawa wengine maana majukumu yao ni tofauti, na hawajacheza katika mazingira sawa, Hivyo huwezi Kupata kigezo kinachopimika kitakachowatendea haki wote.
Ndiyo maana hakuna mchezaji wa dunia aliyewahi kuchaguliwa kwa asilimia inayofikia asilimia 50%. Kwa maneno mengine dunia haijawahi kukubaliana ni nani aliye mchezaji bora wa dunia maana wanatumia kura hivyo zoezi zima kuingiliwa na subjectivity! Huwezi kuwalinganisha kwa haki golikipa, defender, midfielder, na strikers!
Ndiyo maana mtu akichukua kiatu cha dhahabu kama anavyotarajia Ronaldo mwaka huu ni wa kuheshimiwa maana kigezo kinachotumika kinapimika (magoli), na kinawahusisha wachezaji wenye majukumu yanayolingana (strikers)! Ukilikataa hili huwezi kubisha kuwa vigezo unavyotumia havipimiki hivyo kutumia hoja ya nguvu (kulazimisha interest zako binafsi), Badala ya nguvu ya hoja (objectivity).