Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Takriban watu 23 wamefariki dunia baada ya sehemu ya barabara ya juu kuporomoka na kupelekea treni ya abiria kuanguka katika barabara ya chini iliyokuwa na watu wengi wakati wa jioni siku ya Jumatatu.
Waokoaji walilazimika kushikilia kwa kreni sehemu ya treni hiyo iliyokuwa imebaki ikining’inia ili kuwaokoa abiria waliokuwa wamekwama ndani ya kifusi cha barabara hiyo iliyokatika na mabaki ya treni, na kufanikiwa kumwokoa dereva wa pikipiki akiwa hai. Watu wengine 70 wamejeruhiwa na 49 kati yao wapo katika hali mahututi.
Meya wa mji wa Mexico City, Claudia Sheinbaum amesema watoto ni pamoja na watu waliofariki baada ya nguzo inayoshikilia barabara hiyo ya juu yenye urefu wa futi 16 (mita 5) kutoka barabara ya chini kukatika wakati treni ilipokuwa ikipita juu yake na kupelekea barabara hiyo kuporomoka.
Shughuli za uokoaji zilitatizwa usiku kutokana na wasiwasi wa kuporomoka kwa kipande cha treni kilichokuwa kikining’inia, huku kukiwa na wasiwasi kuwa watu wengine wanaweza kupatikana wakiwa hai ndani ya treni hiyo.
Barabara hiyo ya juu imewahi kulalamikiwa kwa kujengwa chini ya kiwango baada ya kukamilika kwake mwaka 2013, huku wataalamu wakihofia kuwa tetemeko lenye ukubwa wa 7.1 kipimo cha rikta kilichotokea mwaka 2017 kikichangia kuharibika kwa barabara hiyo.