BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mashuhuda waliripoti kuona majengo yanatikisika ingawa bado hakukuwa na ripoti za haraka za madhara kwa binadamu, huku meya wa Mexico City akiripoti kuwa hakuna uharibifu mkubwa.
Licha ya kutotangazwa madhara, agizo la kuhama kwenye maeneo ya hatari limetolewa.
Mamlaka ya Hali ya Hewa imesema tetemeko hilo lilikuwa na kipimo cha 6.8 huku uchunguzi wa Jiolojia wa Marekani ukiiweka takwimu hiyo kuwa 7.5 na kusema kuna uwezekano wa Tsunami kutokea.
Tetemeko hilo linakuja katika kumbukumbu za tetemeko kubwa zaidi la ardhi lililorekodiwa nchini Mexico, ambapo zaidi ya vifo 5,000 viliripotiwa baada ya mji mkuu kukumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.1 mnamo Septemba 19, 1985.