Jana nimesikia Waitara akimkoromea Mbowe kutokutumia pesa huko Hai na akampa madaraka mkuu wa wilaya kuzitumia pesa za mfuko wa jimbo hilo.
Tuliona Ofisi ya Bunge ikimpa rais Mipesa kibao kwamba haikutumika, tumeona Dr. Mpango akiyakoromea makampuni yasiyoleta gawio, viongozi wa hayo makampuni watafute kazi zingine.
Tumemsikia na kumuona Dr. Mpango akilalamikia Tanzania kupunguziwa misaada ya wahisani, hadi kusababisha baadhi ya miradi kutokutekelezeka na mingine kusuasua.
Na mara kadhaa tumemsikia rais Magufuli akitafuat pesa kokote humu ndani hadi kuwakumbusha wakurugenzi kubuni njia zingine za mapato.
Sasa leo nimeshangaa, Eti moja ya makosa ya Meya Mwita ni kutokutumia Bil 5.8 zilizotoka kwa Kisena.
Ikiwa tunashida na tunatafuta pesa kila kona kwanini hilo liwe kosa kwa Meya badala ya kumpongeza na kuzichukua zikafanye kazi kwingine?
Tatizo liko wapi hadi iwe hivyo kwa Meya Mwita?
Mgogoro wa UDA na jiji uliisha au bado upo, na kama upo au kesi iko mahakamani kwanini hiyo pesa itumike? na kama mgogoro uliisha kwanini haikutumika?