Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Meya anyang’anywa gari, ofisi yafungwa. Adai kuwa yeye bado ni Meya halali

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita Meya anyang’anywa gari, ofisi yafungwa. Adai kuwa yeye bado ni Meya halali

Ccm ni wajinga sana,hapa namuona Paul Makonda (Bashite) akitaka kumpokonya Boniface umeya wa jiji kwa kuwa Boniface alishawahi kuligangamalia suala la vyeti vya Bashite!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alipo haribu ni kusema raisi Alingilie Kati hilo swala ngoja nisiseme chochote nisikilizie tu nini kitatokea Mara baada ya hapo
 
Hizo bilioni 5.8 zingejenga madarasa mengi sana na kufanya watoto zaidi ya 5000 kuingia masomoni hapo Dar.Huyo meya ni wa kufurushwa mapema
Aliyelipa hizo pesa anafanya nini gerezani?
 
Dar ni mali ya upinzani tangu 2015 na huo ni ukweli. Kazi ya kuirudisha kwa mmiiki wa kabla ya 2015 inaambatana na baadhi ya mambo ya machafu.
 
Namshangaa Neya anapoomba Raia aingilie kati.... Hivi anafikiri haya yanafanyika bila kupata Baraka toka juu.....!!
 
Kutokutumia pesa za wananchi ni kuwanyima wananchi maendeleo,kuwanyima wananchi maendeleo ni kosa. Mengine sijui mkuu.

macson
Duuuh,basi tukakwapue hazina yote tubaki weupe!
 
Magufuri atakuwa alielekeza kuhakikisha wakati anarudi Dar hilo jiji lisiwe na MEYA wa Upinzani.

Ambacho anashindwa kukumbuka huyu meya alichaguliwa kwa ridhaa ya wananchi baada ya kuchaguwa madiwani wengi kutoka upinzani.

sisi wananchi tunafuatilia kwa karibu sana, kiwango cha dharau anachoonyesha Magufuri dhidi ya maamuzi yetu ya kikatiba.
Na ajue, tunajua, analiongoza Taifa hili kwa njia za ukwapuaji. hakushinda uchaguzi wa mwaka 2015.

Na kama anachokifanya kinatokana na kiburi cha kuliongoza Taifa japo hakushinda uchaguzi, tunampa salamu. haya mambo yana mwisho, aombe Mungu mwisho usiwe wakati wake.

Jiheshimu uheshimiwe
 
Amani ni kama afya ya mwili. Ni lazima itunzwe ila ukiamua kuibomoa unaweza mfano kwa kunywa viroba. Naona watu wameamua kinywa voroba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Meya Jiji la Dar es Salaam, nchini Tanzania Isaya Mwita amejikuta njia panda baada ya kunyang’anywa gari alilokuwa akilitumia ambalo linamilikiwa na halmashauri hiyo muda mchache baada ya uamuzi wa mkutano mkuu kutoa uamuzi dhidi ya tuhuma dhidi yake.

Mkutano huo umefanyika leo Alhamisi Januari 9,2019 katika ukumbi wa mikutano wa Karimjee wilayani Ilala, Dar es Salaam chini ya ulinzi wa Polisi.

Akisoma matokeo ya azimio la wajumbe waliopiga kura ya kutokuwa na imani na Mwita, Naibu meya Abdallah Mtinika aliyekuwa akiongoza kikao hicho idadi ya waliopigwa kura kwa kusimama kwenye viti vyao ni 16.

"Naomba nisome uamuzi wa mwanasheria wetu wa jiji la Dar es Salaam, kuhusu uamuzi wa kutokuwa na imani ya meya.”

“Kura zilizopigwa ni 16 na mjumbe mmoja ameomba udhuru na wawili hawakupiga kura, uamuzi wenu umepitishwa, baada ya hapo nafunga kikao," amesema Mtinika

Hata hivyo, Mtinika hakusema kama Mwita ameondolewa katika nafasi badala yake alisema uamuzi wa wajumbe 16 ambao ni CCM. Hata hivyo baada ya kutoa uamuzi huo wajumbe wa Chadema walionekana wakishangilia na kusema kuwa bado Mwita ni meya wa jiji hilo.”

Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amesema kwa mujibu kanuni ili Mwita aondolewa ilitakiwa ipatikane theluthi mbili ambao ni wajumbe 17, lakini CCM walikuwa 16.

Baada ya kutoka nje ya ukumbi Mwita alikwenda moja kwa moja katika maegesho ya magari ambako hakulikuta gari aina Prado alilokuwa akilitumia katika shughuli zake za kila za nafasi hiyo.

Hata hivyo, Mwita amesisitiza yeye bado meya wa jiji hilo kwa kuwa kikao hicho hakijatimiza akidi ya kumuondoa katika wadhifa huo kwa mujibu wa kanuni.

"Nashangaa nimenyang' nywa gari na bendera imeshushwa nawaambia mimi bado ni meya. Namuomba Rais John Magufuli aingilie kati suala hili kwa sababu wakati naingia madarakani ilikuwa hivi hivi.”

"Sio gari tu hadi ofisi imefungwa sielewi kinachoendelea dhidi ya wadhifa wangu. Nasisitiza mimi bado meya wa jiji hili," amesema Mwita

Kikao hicho kilikuwa na lengo la kupokea taarifa ya uchunguzi dhidi ya tuhuma za Mwita baada ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuchunguza tuhuma ambazo zinamkabili.

Miongoni mwa tuhuma anazokabiliana nazo Mwita ni kutotumia Sh5.8 bilioni za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda). Fedha hizo ni asilimia 51 ya hisa zilizotolewa na kampuni ya Simon Group kama sehemu ya ununuzi wa asilimia 51 ya hisa za Uda.

Tuhuma nyingine ni kutumia vibaya gari ya ofisi ambayo alipata nalo ajali, kushindwa kuongoza kikao cha baraza la madiwani na kusababisha meya wa Ubun-go Boniface Jacob kugombana na meya wa Temeke, Abdallah Chaurembo na kudaiwa kuwapendelea baadhi ya mameya kuingia kwenye kamati za fedha.

Hata hivyo, Mwita ambaye pia mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, alishajibu tuhuma hizo akisisitiza hahusiki na jambo hilo bali ni za kutengenezwa ili kuondolewa katika kiti hicho alichokitumikia kwa miaka minne
Mbona hizo tuhuma nyepesi hata kama ni kweli????
 
Hili lilishajulikana mapema sana, ccm kama hawakutaki watakuondoa hata kwa lazima,huko mahakamani alipokwenda kuzuia hilo sijui imekuaje..

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilishangaa sana jana eti Hakima anasema alikuwa amepanga kutoa uamuzi wake leo (tar 10/01/20) kwa sababu alikuwa hajamaliza kuandika, wakati yeye anapanga kutoa uamuzi juu ya shauri hilo huku kikao knaendelea cha kumuondoa meya madarakani as if hakuna issue yeyote imepelekwa mahakamani
 
Social Political Dimensional barriers will not be easily overcome d, It's a central and highly complex impediment of progress, especially if you do not recognise them as such!

Ufanyeje sasa;

Self identification as part of a Global community ndo dawa! wana JF!
 
Magufuri atakuwa alielekeza kuhakikisha wakati anarudi Dar hilo jiji lisiwe na MEYA wa Upinzani.

Ambacho anashindwa kukumbuka huyu meya alichaguliwa kwa ridhaa ya wananchi baada ya kuchaguwa madiwani wengi kutoka upinzani.

sisi wananchi tunafuatilia kwa karibu sana, kiwango cha dharau anachoonyesha Magufuri dhidi ya maamuzi yetu ya kikatiba.
Na ajue, tunajua, analiongoza Taifa hili kwa njia za ukwapuaji. hakushinda uchaguzi wa mwaka 2015.

Na kama anachokifanya kinatokana na kiburi cha kuliongoza Taifa japo hakushinda uchaguzi, tunampa salamu. haya mambo yana mwisho, aombe Mungu mwisho usiwe wakati wake.

Jiheshimu uheshimiwe
Wapo wapi akina Iddy Amin dada na yule msaidizi wake mnyama mwenye Roho mbaya kama ya Daud Bashite alijulikana kwa jina la Maliyamungu , wapo wapi alina Sadam Hussein, Gadafi, Bokasa, Abacha, Mabutu, chiluba, Allbashiri na wenzao wenye Tabia kama zao?
 
Back
Top Bottom