Meya wa Moshi kuingia darasani kufundisha wanafunzi na kumsifia Rais Samia mbele ya wanafunzi ni sahihi?

Wizara ya Elimu popote mlipo , NAOMBA MKEMEE HIKI KITENDO HARAKA SANA KWANI NI KUDHALILISHA TASNIA YA UALIMU. HIVI KWANINI TUNARUHUSU HUU UJINGA UTAMALAKI? WIZARA YA ELIMU TOENI KAULI JUU YA HUU UJINGA.

Ukienda popote na ukafanya chochote hata nje ya utaratibu, ili mradi unamsifia rais basi ujue uko salama, hakuna yoyote wa kukugusa.
 
Wizara ya Elimu popote mlipo , NAOMBA MKEMEE HIKI KITENDO HARAKA SANA KWANI NI KUDHALILISHA TASNIA YA UALIMU. HIVI KWANINI TUNARUHUSU HUU UJINGA UTAMALAKI? WIZARA YA ELIMU TOENI KAULI JUU YA HUU UJINGA.
CCM ndivyo inavyoendelea kutuharibia nchi. Hayo yote kiherehere ili Rais amuone kama mchapakazi. Kupongeza kila kitu na kukihusisha na Rais. Mbatis emetwambia tuna tatizo la viongozi wengi kuwa mapunguani ktk nchi hii.
 
Huyu Meya dizaini namwonaga kama ana wenge flani.. Hivi hali msuba kweli?
 
Biology is a study of living things.
-Binamu
-Animal
-Mimea

Kupatwa kwa elimu.
Angalia alivyo jidhalilisha, hivi ndivyo siasa inavyoingilia shughuli za kitaalamu na kusababisha uharibifu. Mfano tu mwanafunzi akiulizwa swali: With examples what do you understand by the term biology? Halafu kwenye majibu ya mwanafunzi unakutana na mifano Kama:
-Binamu
-Animal
-Mimea
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
Huyu ni opportunist mkubwa kama nakumbuka alichangia kuongeza maambukizi ya uviko19 wakati wa Jiwe kwa kuzuia watu kuvaa barakoa ili kumfurahisha Jiwe. Anaalingalia upepo upande wenye maslahi kwake kisiasa.
 
Sio hivyo tu mkuu,biology haihusiki na living things but also non living things, hapo meya kapotosha Sana,na mtoto huenda amekalili hivyo, mwisho wa siku lawama zinaenda kwa mwalimu
 
Hivi lile sakata lake na mkuu wa wilaya la milioni 25 za limo liliishaje
 
Huyu ana tuhuma kubwa akishirikiana na Sabaya zipo wazi

Anacho kifanya hapo ni kufukia kupata huruma litakapokuja kusanuka
 
Kwa nini afundishe? Alikuwa na lesson plan?
 
Ndio Maana nilisema, Watoto wangu kusoma hizi shule za Umma kwa level ya Primary na Sekondari ndani ya Tanzania hii.
Big No!! Oneni jinsi watoto wanaonewa.

Kwanza limsururu la watu wazima hivyo kuingia Darasani ni kuharibu tension ya Watoto na Walimu.

Na hautasikia popote Wizara ya Elimu au Tamisemi wakikemea hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…