Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Katika historia ya ujasusi wa kimataifa, kuna sura ambazo hazikuwahi kuvalia sare za kijeshi wala kuwa na vitambulisho rasmi, lakini walikuwa silaha kubwa katika operesheni za kificho. Mmoja wao ni Meyer Lansky, kamaria mmoja hatari na mfanyabiashara wa kamari haramu, mafia hatari, na kiungo namba nane katika operesheni ya CIA dhidi ya kiongozi wa Cuba, Fidel Castro.
Lansky, mzaliwa wa familia ya Wayahudi waliokimbia Ulaya Mashariki, alikulia katika mitaa ya New York hadi kuwa mmoja wa mafioso maarufu na hatari zaidi wa karne ya 20. Alijenga mtandao mkubwa wa kamari haramu ndani ya Las Vegas, Cuba kabla ya mapinduzi, pamoja na Bahamas. Lakini kile watu wengi hawajui ni kwamba shughuli zake za kihalifu ziliwavutia sana idara ya ujasusi ya Marekani — CIA.
Mnamo miaka ya 1960, punde tu baada ya Mapinduzi ya Cuba na kuingia kwa Castro madarakani, Marekani ilijikuta ikihitaji mbinu mbadala za kumdhoofisha na kumuondoa kiongozi huyo wa Kikomunisti. Ndivyo Operesheni Mongoose ilipozaliwa — mpango wa siri wa kumuua Fidel Castro na kusababisha machafuko nchini humo.
Lakini CIA haikuwa na watu wengi wa aina ya Lansky, sampuli ya watu waliokuwa na mitandao, fedha, na uwezo wa kuua pasipo kujulikana kirahisi. Majina mengi yakaletwa mezani, Sam Giancana, Santo Trafficante Jr, Johnny Roselli, ila lilipofika jina la Meyer Lansky mwamba hatari sana na ndipo wakaona ndo suluhu ya operesheni yao.
Vitabu kama “Mafia Spies” kilichoandikwa na Thomas Maier pamoja na kitabu cha “Legacy of Ashes: The History of the CIA” cha Tim Weiner, vinaeleza kwa kina jinsi CIA ilivyoshirikiana kwa umakini na wahalifu wa Marekani kama Sam Giancana, Johnny Roselli, na kwa kiasi kikubwa, Meyer Lansky. Hawa walikuwa na maslahi ya moja kwa moja dhidi ya Castro, kwani mapinduzi ya Cuba yalifuta kabisa himaya yao ya kamari haswa ndani ya mji wa Havana. Ni kama vile Castro aliwanyima ugali wao.
Kabla ya mapinduzi ya 1959, Lansky alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya utawala wa Dikteta Fulgencio Batista. Alimiliki na kuendesha majumba ya kasino mengi pamoja na nyumba za starehe kama vile, Hotel Nacional de Cuba pamoja na Riviera Hotel, sehemu ambazo zilitumika mara kadhaa kama vituo vya utakatishaji fedha na mikutano ya mafia.
Ndani ya kumbi hizi zilikuwa maarufu sana kwa muziki wa kuvutia wa jazz, pamoja na mambo, na ilikuwa ni kawaida kusikia sauti za wasanii kama Nat King Cole, Frank Sinatra, na Benny Moré waliopiga nyimbo maarufu kama “Autumn Leaves”, “Fly Me to the Moon”, na “Bonito y Sabroso” zilizoleta haiba ya kifahari na raha sana kwa watu waliokuwa makini kucheza kamari.
Uchumi wa kumbi hizi ulikuwa mkubwa sana — baadhi zilikuwa zikikusanya zaidi ya $500,000 kwa wiki katika mapato ya kamari na burudani, zaidi ya bilioni 1.3 ndani ya wiki moja pekee kwa pesa za Kitanzania, kiasi hiki kiligawanywa baina ya mafia na viongozi wa serikali ya Batista.
Hii ilimfanya Lansky awe mtu muhimu sana kwa CIA — alikuwa na uelewa wa ndani wa siasa, uhalifu, na uchumi kivuli ndani ya Cuba.
CIA ilielewa kuwa Lansky alikuwa na uwezo wa kuandaa mashambulizi ya kisiri dhidi ya Castro kupitia mitandao yake pasipo CIA kuhusika moja kwa moja.
Ingawa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha Lansky alihusika moja kwa moja katika njama ya mauaji, nyaraka mbalimbali zinaonyesha kuwa alikubali kushirikiana na CIA kwa sharti la kurejeshewa biashara zake endapo Fidel Castro angeondolewa madarakani.
Kwa mujibu wa kitabu “The Game of Nations” cha Miles Copeland, ambaye alikuwa afisa wa CIA, ujasusi wa kimataifa mara nyingi hutegemea watu walioko “nje ya mfumo” wengi ambao huwa ni wahalifu, wafanyabiashara wa silaha, na wakati mwingine watangazaji wa habari.
Sio ajabu hata kidogo kuona utendaji kazi wa *Joseph Alsop alivyokuwa akipigia chapuo sera za kigeni za Marekani ndani ya bara la Asia.
Hata Ben Bradlee ambaye alikuwa shushusu wa CIA, watu kama Carl Berstein, Walter Cronkite, Howard Hughes, pamoja na George Plimpton. Kwa CIA, kushirikiana na mafia ilikuwa njia ya kupata matokeo bila kujihusisha moja kwa moja. Kwa Lansky, ilikuwa ni njia ya kulinda maslahi ya kifedha, hivyo ilikuwa ni WIN-WIN kwa pande zote.
Kitabu cha “Confessions of an Economic Hit Man” kilichoandikwa na John Perkins pia kinaeleza jinsi mashirika mengi ya kijasusi yanavyotumia mashirika au watu wa kawaida kufanya kazi chafu kwa niaba ya mataifa makubwa. Lansky aliingia kwenye muktadha huu kama mchezaji kwa mkataba wa muda tu— akitoa msaada wa mtandao na rasilimali kwa ujasusi wa kimataifa.
Operesheni dhidi ya Castro hazikufanikiwa, lakini zilifichua na kuanika wazi jinsi Marekani ilivyokuwa tayari kutumia mbinu zozote — hata kushirikiana na watu waliokuwa wakitafutwa na sheria. Zipo ripoti zinazoelezea kuwa Fidel Castro alipona zaidi ya hatari 638 za kutaka kumtoa uhai.
Lansky aliendelea kuwa tajiri, lakini aliepuka kushtakiwa mara nyingi sana. Hili linaongeza mashaka kuwa aliendelea kuwa “mjasusi asiye rasmi” kwa mashirika ya serikali kama vile, NSA pamoja na IRS kwa kupewa vibarua kadhaa.
Wakati Roselli na Giancana wanakufa katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuchunguzwa na Kamati ya Seneta Frank Church kuhusu uhusiano wa CIA na mafia, Lansky aliishi hadi uzeeni na kufa mwaka 1983.
Meyer Lansky anabaki kuwa mfano bora wa jinsi ujasusi unaweza kushirikiana na wahalifu kwa ajili ya maslahi ya taifa. Alikuwa mhalifu, lakini pia alikuwa rasilimali mtu. CIA ilimtumia katika vita ya kivuli dhidi ya Castro, na ingawa hakuwahi kusimama jukwaani kama jasusi, mchango wake ulisababisha miongo kadhaa ya mvutano kati ya Marekani na Cuba.
WIKI HII NITALETA UZI MAALUMU KUHUSU KISA CHA DADA YAKE FIDEL CASTRO AMBAYE ALIFANYA KAZI KWA UKARIBU NA CIA.