Mfahamu Abby Chams, mtoto mwenye kipaji cha kutisha


Kuishi Tanzania sio lazima ujue Kiswahili

Kuna watu Tandahimba,Kigoma hata Moshi milimani kabisa huko lugha yake kuu ni ya Kienyeji

Hivi mnaona kila mtu ni lazima Kiswahili akijue?

Majitu yapo biased sana na mnataka dunia nzima Kiswahili ndio iwe standard...mwingine akitaka kuzungumza lugha ingine anayotaka yeye,then mnamshambulia??!

Hii tabia ya Kiswahili supremacists ni ya kipumbavu sana...nikitaka kuzungumza Kichagga niache ni changu,sijui kwanini mpo butt hurt namna hii?!
 

Mzee hata civics ya form 1 hukusoma kuwa lugha ni part ya culture?

Slave mentality inakuja hivi kipindi kile cha ukoloni manamba walijifunza lugha za wakoloni ili watumike kama walanguzi na wasimamiaji wa kutafuta na kuuza watumwa.
Walifanya hivi ili wajipendekeze kwa hao wakoloni ili wasiwe pamoja na watumwa.

Dunia nzima mlikaa mkapitisha kiingereza lini??mbona mimi sikusikia? Au mlikutana nyumbani kwenu?

Sichukii mtu anayeongea lugha tofauti na yangu ila namdharau anayeisahau/kuichukia lugha yake Katika mazingira anayoishi.
Hao kina Abby wangezaliwa marekani na kukulia huko basi sawa hata kutojua kiswahili.
 

Sawa ila ukiishi tandahimba kijijini na umezungukwa na wamakonde tu maisha yako yote halafu kwasababu unataka kuonekana mjanja wa mjini wewe ukawa hujui kimakonde unajua kiswahili tu..hilo nalo litakuwa tatizo.

Ishu sio kiswahili tu ishu ni kuwa watu tunajidharau utamaduni wetu na lugha zetu na kuabudu tamaduni na lugha za wengine.
Sio dhambi kuzijua lugha nyingine ila ni dhambi kuzisahau lugha mama.
 
Huyu binti kajaliwa vipaji vingi na katoka familia tajiri /yenye uwezo na anatumia fursa anazozipata vizuri. Anajielewa na ametengemezewa mazingira ya kujielewa. All the best to her she is inspiring. If you are blessed with certain talents you are blessed haijalishi ni maskini /tajiri juhudi zako ndio zinazomatter.Anaonekana anapenda kile anachofanya kutoka moyoni na anajuhudi. Really inspiring. ...!
 
Kuna watu wana vipaji mara mia ila hawajulikani kwasabab ya umasikini...hata wewe ungekulia yale mazingira ungekuwa na kitu fulani unique.
Kama mbwa marekani wanapiga mpaka piano unashangaa nini mshua mmoja kucheza violin bongo??
 

Huyu si ndio aliefanya nyimbo na ben paul kabla ben paul hajaenda kenya kwa Anerlisa?
Alianza game kwa kupiga violin!!!
 
Kuna watu wana vipaji mara mia ila hawajulikani kwasabab ya umasikini...hata wewe ungekulia yale mazingira ungekuwa na kitu fulani unique.
Kama mbwa marekani wanapiga mpaka piano unashangaa nini mshua mmoja kucheza violin bongo??
Shida ni kuwa watu wengi mnaingiza utajiri wa kwao na kipaji chake. Nahisi asingekuwa na kipaji tusingemdiscuss hapa na hamna mtu ambaye angeshughulika nae
 
Shida ni kuwa watu wengi mnaingiza utajiri wa kwao na kipaji chake. Nahisi asingekuwa na kipaji tusingemdiscuss hapa na hamna mtu ambaye angeshughulika nae
Shida ni kuwa hatuoni haja ya kumdiscuss mtu ambaye haoni thamani ya utanzania.
Ni sawa na kuanza kumsifia baba ako aliyekukana akaikimbia familia eti ana akili hata kama ni professor kwasababu hakuhusu na hakutaki.
Huyo dogo ni moja ya wale wabongo wasiopenda kuwa wabongo.
 
Hivi lugha inamclassfy mtu? Maana angengea kilugha mngesema ni mkabila.Hiyo ni priority tu ya mtu kiingereza ni lugha kama lugha zingine maisha yamebadilika badilisha Fikra.Jinsi alivyo inatokana na maisha/malezi aliyokulia.Kwanza haringi,anajipenda she loves her black natural colour,anavaa kwa staha,anajiremba kwa wastan that's enough to classify her as a Tanzanian girl
 
Okay bi mkubwa. Wewe utakuwa dada yake maana ningesema utakuwa yeye ningesokea maana yeye hajui kiswahili.
Unamfahamu mzungu aliyezaliwa na anayeishi states au UK halafu hajui kiingereza yeye anajua kiswahili?

Kama lugha sio priority ya kuidentify utaifa wa mtu bali ni mavazi na kujiremba ndo vya muhimu basi mwalimu wako wa uraia anajilaumu sana.
 
nyie majamaa Mcqueenen na Wyatt Mathewson mmeharibu kabisa huu uzi... si mpeleke mabishano yenu jukwaa la lugha?

kwanza majina yenu hayana uzalendo afu mnateteana lugha humu kwanini msingejiita MAKWININI na mwingine WATU MATESONI?

Tena majina hayo uliyowapa ni ya Kingereza,ingefaa mmoja tumuite Tutumfye na mwingine Mwakaleli ...🤣🤣🤣🤣🤣🤣...

Nakubaliana na Wyatt,Kingereza ni lugha inayounganisha mataifa mengi,ukiimudu ni kitu cha ziada...so hongera kwa mdada wetu..
. Mcqueenen mbona unaongea kiswahili..na huongei lugha ya kabila lako?? huo uindigneous sidhani aisee.
 
Ukiimudu ni vizuri namimi sishangai dogo kujua kiingereza kwasbabu hata kingereza chake cha kawaida mno.
ishu ni kuwa eti unakua mTz halafu hujui kiswahili does it come come?
Mimi kilugha nakitwanga ng'wadila ng'waguku.

Na hata mtu anayekulia mazingira ambayo wanaongea lugha fulani na kwasababu zake aamue kutoipenda hiyo lugha na kuchagua ya kigeni huo ni ufala na usaliti.

Wewe unamjua mzungu aliyekulia USA au UK hakui kiingereza?
 
Mnaopiga kelele watu kuongea kiingereza wakati ndio lugha ya kufundishia kuanzia form one mpaka chuo kikuu mi nawaona wanaafiki tu. Hata hao wabunge wenu wanaowawakalisha huko kijijini kwenu wakiwa Dodoma tunawasikia wakiongea broken zao. Tanzania ni nchi huru kila mtu kwa mpango wake, acheni hizo.
 
Ishu sio kuongea kiingeleza,kijaruo au kijapan ishu ni kuwa unaishi Tz na hujui lugha ya nchi yako.Sio kwasababu ya msingi ila tu unapenda lugha ya kigeni ili uonekane mjanja
Hao wabunge wasipojua kiswahili hatuwachagui walahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…