Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa barabara Dar (Bamaga - Urafiki) kutambua mchango wake kwa Taifa

mbona shule ya msingi na sekondari hilo linafundishwa sana, wewe hukuhudhuria?
Kwa hii mitaala ambayo kila shule inajichagulia kitabu cha kufundishia unategemea shule zote mtasoma kitu kimoja kwa aina moja?
 
mbona shule ya msingi na sekondari hilo linafundishwa sana, wewe hukuhudhuria?
Historia ya kweli haiko shuleni, mambo mengi tuliyosoma ni yale yaliyowapa sifa watawala tu, chini kuna mengi zaidi. Mimi sio kilaza kuandika hivyo. We utaamininkila unalofundishwa shuleni?
 
Aisee nilikuwa sijui chochote kuhusu hilo.
 
T
Historia ya kweli haiko shuleni,mambo mengi tuliyosoma ni yale yaliyowapa sifa watawala tu,chini kuna mengi zaidi.Mm sio kilaza kuandika hivyo.We utaamininkila unalofundishwa shuleni??.
Uwekee hizo historia za kweli.
 
Daah Story nzuri. We never hear these stories at school. Na mwenye story ya Bibi Titi Mohamed
 
Last edited:
Nisaidieni kumuita hapa mzee Mohamed Said
 
Good piece of history, ila ningependa na askari waliofariki wakiwa na Shekilango nao wakumbukwe.
 
Shukran sana kwa rekodi hii kumbukumbu ya heshima ambayo inaweza kuwa sehemu ya historia. Ningependa kuongezea yafuatayo:

Kwanza, ningependa kuhakikishiwa kama ile ndege iliyoanguka kwenye Mlima Meru ikiwa na Waziri Shekilango, wakati ule, ilikuwa ya Jeshi au ya kukodi?

Pili, katika ndege hiyo pia alikuwepo Bw. Chilumanga ambaye alikuwa Ofisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Tanzania. Huyu ndiye alikuwa Msaidizi Mkuu wa Waziri.

Tatu, baada ya muda kidogo, Ojok naye alifariki nchini Uganda kwa njia hiyo hiyo. Helikopta ya Jeshi aliyopanda ilianguka. Katika helikopta hiyo pia alifariki askari wa Tanzania aliyekuwa mlinzi wake akiitwa Friday. Nakumbuka Friday alikuwa Mnyakyusa smart na mcheshi lakini sikujua majina yake mengine wala maskani yake au wazazi wake walikuwa mji gani hapa Tanzania!

MWENYEZI MUNGU AZIPE FARAJA ROHO ZA MAREHEMU HAO.
 
Hili jina She nilikuea nikihisi ni mtanga ila sikuwa na uhakika, nakushukuru mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…