Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa barabara Dar (Bamaga - Urafiki) kutambua mchango wake kwa Taifa

Mfahamu Hussein Shekilango, aliyepewa barabara Dar (Bamaga - Urafiki) kutambua mchango wake kwa Taifa

Nadhani shekilango mwenyewe anasikitika sana huko aliko barabara yenye jina lake kutumiwa na wauza papuchi
 
JINA SHEKILANGO

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA
Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Ngudu Godfrey Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) Ndugu David Oyite Ojok na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe.

Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kamapala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wanakorogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Hussein Ramadhani Shekilango
 
Asante sana! RIP Shekilango na Kilumanga!
 
Kifo chake kinashabihiana sana na kifo cha John Garang.
 
Hey The Boss,
My mom is msambaa and my daddy is half Irish half dutch.

Taarifa yako sio ya kweli.
Wako watu wanaitwa Lukindo mpaka leo, and what I can remember is that, Lukindo is called Ukindo in Kisambaa
Wako watu wanaoitwa Kilango mpaka leo.

She in kisambaa is [ a son of ]

See this, Maukindo
A daughter of Ukindo.
You are right Darwin
Nadhani jamaa kateleza kidogo kuingia ukurasa huu kwa makusudi au kutokujua
Kuna maneno mengi ya majina kujaribu kuelezea mtoto wa
Mfano wamasai Ole----Sendeka
wanyakyusa Mwa-----kipesile
Wasambaa She------lukindo
waingereza Mac-----kenzie
makaburu Van-----Niekerk
wadachi Von-bunchenroder
wasukuma Mwana-----kachungwa
 
HUSSEIN RAMADHANI SHEKILANGO, SHUJAA ALIYEKUFA AKIIJENGA UGANDA

Jijini Dar es salaam kuna Barabara Mashuhuri kama 'Shekilango Road', ikianzia maungio ya Barabara ya Morogoro eneo la Nyumba za NHC mkabala na Kiwanda cha Urafiki, ikipitia Mitaa yote ya Sinza na kuishia Maungio ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi kituo cha Bamaga.

Ni watanzania wachache wajuao kuwa Barabara hiyo ya Shekilango imepewa jina Maalum kwaajili ya heshima ya Ndugu Hussein Ramadhani Shekilango, aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu, akishughulika zaidi na mambo ya Utawala, wakati wa Uongozi wa Rais Julius Nyerere na Makamo wake Aboud Jumbe Mwinyi.

Hussein Shekilango alichaguliwa na Wananchi wa kwao kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Jimbo la Korogwe Mjini, Mkoani Tanga katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1975, akiachia nafasi yake ya Zamani ya Meneja Mkuu wa Shirika la Usagishaji Nchini (NATIONAL MILLING CORPORATION).

Mwaka huo huo akachaguliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Utawala) akiwa chini ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu, ndugu Rashid Mfaume Kawawa.

Mwaka 1977 yalifanyika Mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri Nchini, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kulinda Taifa, Ndugu Edward Moringe Sokoine aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Kawawa, Shekilango akabakishwa katika nafasi yake lakini akiwa na bosi mpya.

MATATIZO YA UGANDA

Mara baada ya Mapambano ya Vita vya Kagera, Mwanzoni mwa mwaka 1979 Vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania vilifanikiwa kumng'oa Madarakani Dikteta Amin wa Uganda na kumpachika Ndugu Yusufu Lule kama Rais wa Muda wa Taifa hilo Jirani. Lule hakudumu sana madarakani kwa kuwa mwezi Juni, 1979 naye aling'olewa madarakani kwa kutofautiana na Baraza la Ushauri la Taifa la Nchi hiyo juu ya uteuzi wa nafasi za Mawaziri, na nafasi yake kuchukuliwa na Godfrey Lukongwa Binaisa.

Miezi kadhaa baada ya kuchukua madaraka kwa Binaisa katika Serikali ya Uganda bado mambo ya kuendesha nchi hiyo hayakuonekana kwenda vizuri, Changamoto za kujenga upya nchi hiyo iliyoharibiwa na vita zilikuwa kubwa, huku Jeshi jipya la nchi hiyo likiwa na kashfa ya kufanya ukatili kwa wananchi na pia kushiriki kwenye uhalifu na uporaji. Ili kuimarisha mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo ilimbidi Rais Nyerere ambaye bado vikosi vya Jeshi lake vilikuwa havijaondoka Uganda, ampeleke Waziri Hussein Ramadhani Shekilango kwenda kusaidia mambo ya Kiutawala ya Nchi hiyo.

Mwezi Mei, 1980 ilizuka sintofahamu kubwa katika Utawala wa Uganda, Rais Godfrey Binaisa alimuondoa Jeshini Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Nchi hiyo (zamani akiitwa Chief of Staff) David Oyite Ojok sasa marehemu na kumteua kuwa Balozi wa Uganda Nchini Algeria, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni nidhamu mbaya ya Jeshi la nchi hiyo hasa kwenye masuala ya Ukatili kwa wananchi na Uporaji.

Uamuzi huo wa Rais Binaisa haukumfurahisha Kiongozi huyo Namba 2 wa Jeshi la Nchi hiyo, hivyo alikataa Uteuzi mpya, na wanajeshi waliokuwa Watiifu kwake wakatangaza kumuondoa Madarakani Rais Binaisa aliyekuwa akilindwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika Hekalu la Rais la Entebbe. Misururu mirefu ya Magari ikaonekana katika Jiji la Kampala, ambapo Wanajeshi watiifu kwa David Oyite Ojok walikuwa wakiyapekuwa magari yote yaliyokuwa yakitoka na kuingia ndani ya jiji hilo ili kuhakikisha hakuna silaha, huku pia wakikiteka Kituo cha Redio cha Taifa cha Nchi hiyo.

Wanajeshi wafuasi wa Ojok waliweka vizuizi katika barabara zote za Jiji la Kampala na kuamua kuyalinda majengo yote nyeti ya Serikali likiwemo Jengo la Nile Mansion Hotel ambalo ndilo lililokuwa na Ofisi nyingi za Wizara nyeti za Serikali ya Nchi hiyo.

Kung'olewa kwa Binaisa kulifanywa na Tume maalum ya Watu sita, ambayo ilikuwa ni sehemu ya Baraza la Ushauri la Taifa lililomng'oa Rais Lule, huku matendo ya Tume hiyo pamoja na Ojok kwenye wiki hiyo yakihusishwa zaidi na Rais Milton Obote aliyekuwa ughaibuni, ambaye aling'olewa Madarakani na Amin mwaka 1971. Obote alikanusha kuhusika na matendo hayo ya Ojok yaliyokuwa yakiteteresha hali ya ustawi wa nchi hiyo japo haikubadili ukweli kuwa marafiki hao lao lilikuwa moja.

katika hali ya matatizo yote hayo, Waziri Hussein Ramadhani Shekilango pamoja na Balozi Kilumanga waliamua kupanda Ndege kwenda kumpa habari za namna hali halisi ya mambo ilivyo nchini humo Rais Nyerere ambaye alikuwa kwenye Ziara ya Kiserikali Mkoani Arusha. Safari hiyo ndiyo ikawa mwisho wa maisha yao.Kwa kuongezea hapa kuna mwanajeshi mmoja naye alikuwa aende siku hiyo kuambatana nao lakini akapata udhuru wa kuuguliwa familia yake siku hiyo hakwenda ndio ikawa pona yake mipango ya mungu jina limenitoka kidogo.

Ilikuwa siku ya huzuni mno kwa kumpoteza Waziri huyo damu changa, Tarehe 11 Mei, 1980, ndege ya Kijeshi iliyowachukua Shekilango, Balozi Kilumanga pamoja na Wanajeshi wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ilianguka katika vilima vya Jiji la Arusha na Abiria wote kupoteza Maisha, wakiacha huzuni na majonzi mazito kwa Watanzania.

Msafara wa Rais ukakatisha ziara na shughuli ya Mapokezi ya Miili ya Mashujaa wetu hao ndiyo ikawa Ratiba rasmi, huku Rais Nyerere akionyesha kwa dhati namna alivyohuzunishwa kwa kumpoteza Waziri huyo Mchapa Kazi kwa Taifa. Majonzi zaidi yakiwa kwa Wana korogwe waliopoteza Kijana wao Msomi wa Makerere aliyejitolea kuwatumikia kwa dhati.

Shekilango alizikwa Kijijini kwao Jitengeni, Korogwe, Mkoani Tanga, huku akisindikizwa na umati mkubwa wa watu, mpaka leo akibaki Mbunge kipenzi cha watu wa Korogwe na akisifika Serikalini kwa hatua yake ya kurudisha Madaraka Mikoani. Kwa kumuenzi kuna Shule yenye jina lake Jimboni Korogwe.

Mamlaka za Uongozi wa Jiji la Dar es salaam kwa kutambua mchango wa Shekilango kwa Taifa, ikaamua kuipa Barabara mpya iliyokuwa inajengwa wakati huo jina la Shekilango ili kumuenzi shujaa huyu.

Mola amlaze Pema Shujaa Hussein Ramadhani Shekilango
 
David Oyite Ojok mungu ailaze roho yake mahala pema peponi. Nitamkubuka kama rafiki/schoolmate mkakamavu na zaidi sana mtu mdadisi mwenye ukorofi uliokithiri pale tu uanapoingilia haki zake za msingi.
 
Jamii forum ni kisiwa cha habari na uchambuzi. Ndo mana nimekuja hapa. Ilikua jumamosi nimetoka zangu sehemu nikaingia mahali nipate chai. Nafika nikakutana na mhudumu na Brother mmoja hivi yuko miaka 40s. Wakawa wanapiga story, yule brother anamwambia mhudumu mi sijawahi kupiga kula na siji kupiga kula.

Mi nikatega masikio huku nikatabasamu kuonesha na Mimi nataka kushiriki kwenye hiyo mada.
Badae akaniambia mdogo angu mbona unacheka? Nikamjibu natamani nijifunze kwa nini unasema uwezi kupiga kura wakati ni haki yako kikatiba kumchagua kiongozi anayefaa, akanipa sababu nyingi ambazo hata mi ndo zinanifanya nisipige kura.

Lakini kilichonifanya kuja kuomba msaada kujua historia ya Shekilango ni baada ya kua interested sana na hiyo habari ili niupate ukweli zaidi.

Wakati anaendelea kunihabarisha akaniuliza unaijua barabara ya Shekilango nikamwambia ndio, akasema, yule alikua waziri wakati wa Nyerere, lakini alidunguliwa alivyokua ametoka Uganda na waziri mwenzie kufanya uchunguzi wa baadhi ya mambo ambayo yalikua yanaonesha uchafu wa Nyerere ndo akaamuru wauawe. Akasema ndo mana uwezi kuona mahari popote huyu waziri ameandikwa. Akanitajia wengi wanaharakati waliouawa, akiwepo Kigoma Malima, Mwaikambo, Kamishna mkuu wa usalama, komandoo aliyetoroka na kwenye kujengewa mnara wa shujaa wa msubiji baada ya mwalimu kuamuru auawe. Niishie hapo.

Naombeni kujue hiyo history vizr ya hiyo Shekilango, Je maelezo ya hapo juu yanaukweli wowote?
 
Mambo ya Nyerere muulize Tundu Lissu ila ccm watakupotosha uone upande mweupe tu
 
Kumbe inaelekea siku za nyuma mpaka sehemu, barabara, jengo kupewa jina la mtu kulikuwa na maana kwa kujitolea kwa ajili ya taifa. Je, hii inafanyika hivyo siku hizi?
... Mfugale bridge sijui flyover pale Tazara imezingatia sana hilo.
 
Hizi ndio History tunazopaswa kuzifahamu,
Naomba siku nyingine mtuletee ya watu walioanzisha na waliokua mstari wa mbele kudai uhuru wa Tanganyika
Sheikh na mwalimu maarufu al-Ustaadh Mohamed Said amekuwa akikuleteeni khabari hizi toka enzi lakini mmeghairi kabisa kuamini khabari zake enyi umma usioamini! Je, shingo zenu na kizazi chenu zikatwe ndipo muamini?
 
Asante kwa kuniongezea kitu kichwani maana nilikiwa sijui lolote kuhusu Shekilango zaid ya kufahamu ni jina la mtaa tu na Barbara yake.
Zaidi ya 85% watanzania walipata ufahamu baada ya Shekilango kufariki.
 
Sheikh na mwalimu maarufu al-Ustaadh Mohamed Said amekuwa akikuleteeni khabari hizi toka enzi lakini mmeghairi kabisa kuamini khabari zake enyi umma usioamini! Je, shingo zenu na kizazi chenu zikatwe ndipo muamini?
Atuletee habari za kimbea tukubali tu?

Huyo anayesema Bungeni 86% ni wakristo?

Hahaha.
 
Back
Top Bottom