Yamakagashi,
Kama kunivunjia adabu hilo ushalifanya na ndiyo imetufikisha hapa kwa mimi
kukuonyesha kuwa nayaweza pia.
Kuhusu Shakespeare labda nikutahadharisha jambo.
Nimefanya fasihi Cambridge Examination 1970 na katika hayo ya Kiingereza
ikutoshe kuwa nimetoka na First Class Merit Pass English Oral yaani mtihani
wa kuzungumza Kiingereza.
Katika moja ya vitabu nilivyotahiniwa ni Shakespeare.
Sasa acha hayo maneno ya Shakespeare wa kutishwa na Shakespeare si mimi.
Nimefanya English Elocution ''passage,'' yangu kutoka kwa Shakespeare ''Julius
Caesar.''
''Into what dangers would you lead me Cassius...''
Malizia wewe...
Hili la kwanza la pili mimi niko katika jopo la waandishi wa Oxford University
Press wanaoshughulika na usomeshaji wa lugha ya Kiingereza kwa shule za
msingi Afrika ya Mashariki.
Nishaandika vitabu viwili katika mradi huo kimoja kwa shule za msingi na kingine
kwa ajili ya shule za sekondari na vitabu vyote viko katika mtaala Kenya.
Nakuwekea hapo chini toleo la kwanza na la pili la moja ya kitabu changu:
Mohamed Said: OXFORD UNIVERSITY PRESS WATOA TOLEO LA PILI LA "THE TORCH ON KILIMANJARO" KITABU CHA WATOTO CHA MWANDISHI MOHAMED SAID
Kwa hiyo mimi si wa kutishwa na mambo ya Shakespeare tafuta mtu mwingine lakini
si
Mohamed Said.
Njoo na hiyo unayoita personal nakukaribisha.
Ungekuwa wewe mama yako kakufunza adabu hiyo adabu mimi ningeiona katika kauli
yako.
Wewe unasema mimi naandika hekaya.
Umenitukana kwa kuwa mimi si mwandishi wa hekaya na nimezunguka duniani kwingi
nikahadhiri historia ya Tanganyika katika vyuo vya kutajika na nimekuwekea usome.
Ungekuwa na akili na adabu ingekutosha kujua kuwa umekosea na ngalau hata kama
usingenitaka radhi basi ungerudi na adabu zako kamili.
Unazidi kudhihirisha umbumbu wako licha ya kukuelekeza kuwa hilo suala lako la rais
Mkristo Zanzibar ni kichekesho, ungekuwa na akili ungefanya utafiti niliokushauri.
Lakini nitakujibu swali lako kwa kuwa wewe huna uwezo wa kujua jibu la swali ulikouliza.
Rais wa nchi na jamii katika nchi yeyote iliyokuwa koloni inachukua uongozi katika nchi
kwa kushiriki katika siasa za ukombozi.
Umepata kuona au kusoma popote pale au angalau kusikia kuwa katika vyama vya
ukombozi Zanzibar, Hizbu, ASP na baadae Umma Party kama kulikuwa na Wakristo
wanapigania uhuru wa visiwa hivyo?
Au umepata kumuona Mkristo yeyote Zanzibar aliyekuwa na nguvu za kisiasa kiasi
aweze kugombea kuingoza nchi?
Mwisho kumbe lililokuchoma ni historia ya
Ali Msham na duka la mafuta la
Mama
Maria Nyerere.
Kwani wewe ulipata kumsikia
Mshume Kiyate katika historia ya TANU na historia ya
Nyerere kabla mimi sijamtaja?
Mshume Kiyate na Nyerere 1964
Tuseme kwa kuwa hakupata kutajwa popote ndiyo
Mshume Kiyate hakuwepo?
Mshume Kiyate alikuwapo na alikuwa rafiki mkubwa sana wa familia ya
Nyerere.
Halikadhalika
Mama Maria katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na yeye
alishiriki kama walivyoshiriki wazalendo wengine na akakumbnana na dhiki kama
zilizowapata wazalendo wengi katika TANU.
Hii biashara ya mafuta
Mama Maria Nyerere aliifanya pia Mtaa wa Mchikichi karibu na
nyumba ya
Mwalimu Bahia.
Huyu
Mwalimu Bahia mimi ni shangazi yangu.
Mshume Kiyate, Ali Msham na
Mwalimu Bahia si ''hekaya.''
Hawa walikuwapo na walishirikiana na
Mwalimu Nyerere bega kwa bega katika kupigania
uhuru wa Tanganyika.
Kulia
Ali Msham aliyekaa ni
Mwalimu Julius Nyerere 1955