Mfahamu Jenny ,, Paka pekee aliyekuwa akiishi ndani ya meli ya Titanic

Mfahamu Jenny ,, Paka pekee aliyekuwa akiishi ndani ya meli ya Titanic

Wangekuwa wanatuambia sasa,😚on a Jimmy katuachia janga la meli,usikute siku ya ajali alikuwa anacheka na watoto wake tu😀
Paka jenny alishajua kinachoenda kutokea maana si rahisi paka kuhama sehemu anayopewa vyakula kama samaki na maziwa bure,, afu ondoke
 
Yapata miaka 113 toka meli hii ya Titanic ilipozama katika bahari ya Atlantic ikiwa katika safari yake ya kwanza ikitokea Southampton kuelekea New york baada ya kugonda iceberg na kuzama huku ikisababisha vifo vinavgokadiliwa kuwa zaida ya 1500 . Mengi yameongelewa juu ya meli hii na ajari yake

Lakini leo ,, ningependa tumuongelee Paka ,, yes !! paka pekee aliyewahi kuishi ndani ya meli hii ya kifahari ya Titanic .

Paka huyu anakwenda kwa jina la Jenny . Jenny hakuwa tu paka wa kawaida kama wengi tunavyodhani bali alikuwa ni paka maalumu ambaye uwepo wake ndani ya meli hii ulitambulika na kampuni ya what star line .


Uwepo wa paka huyu kwa jina la Jenny ulikuwa ni kudhibiti uzalianaji wa panya ndani ya meli ya Titanic . Wakati wa majaribio ya meli hii ya Titanic . Jenny alifanikiwa kuzaa watoto watu na kuwa paka pekee iliyeweza kuweka record ya kuishi na kuweza kuzaa ndani ya meli ya kifahari ya Titanic .

Ndani ya meli hii Jenny alikuwa chini ya uangalizi maalumu wa bwana Jim MulHolland . Mmoja wa wafanyakazi wa meli hii ya kihistoria ya Titanic . Bwana jim alimtengenezea sehemu maalumu ya kuisha paka huyu ,, na kutokana na hali ya baridi katika bahari ya Atlantic basi bwana jimmy alihakikisha sehemu ya kuishi paka huyu inakuwa karibu na sehemu za kuzalishia joto zilizopo ndani ya meli ya Titanic yani ( boilers ) ili kuweza kumsaidia paka huyu asipate shida wakati wa baridi kali wawapo safarini .. nje na hilo bwana jim ndiyo alikuwa in - charge juu ya paka huyu yeye ndiyo alitakiwa kuhakikisha paka huyu anakula na anakuwa katika hali salama muda wote ndani ya meli hii ya Titanic..


Lakini kitu cha kushangaza kinatokea ,,,,,,,,

Siku chache kabla meli ya Titanic haijaanza rasmi safari yake ya kwanza ikitokea Southampton kuelekea New york . Tabia ya paka huyu (Jenny ) inabadilika ghafla. Ndani ya meli Jenny anaonekana kuwa bize asiyepumzika akienda huku na huko baada ya muda fulani Jenny alionekana kuamisha watoto wake mmoja mmoja akiwa kawang'ata sehemu ya shingoni ,, ikitumia sehemu ya ngazi iliyopo kwenye meli ,,Janny alishuka toka kwenye meli ya Titanic na kuwahamishia watoto wake nchi kavu ..

Jambo hili lilimshangaza sana bwana ,, Jim Mulholland na kuzalisha maswali mengi ndani ya kichwa cha bwana jimmy na kutokea hapo kuna jambo likawa wazi , jambo ambalo wengi hawakulijua . Jimmy kwa kuamini mawazo ya ndani yalioneshwa na paka kwa jina la Jane . Taratibu akaamua kupakia vitu vyake na kuamua kuondoka taratibu ndani ya meli hii ya Titanic na tokea hapo bwana jimmy anasema hakuwai kurudi tena ndani ya meli hii ya Titanic ..

Hivyo siku ya Tarehe 14 /4 /1912. TITANIC ilianza safari bila uwepo wa Jimmy . Na wote bila shaka tunajua nini kiliikuta meli hii masaa machache baadae

Miaka kadhaa baadae Jimmy ambaye kwa wakati huo alikuwa tayari ameshakuwa mzee ,, aliamua kumsimulia stori hii kwa mmoja wa waandishi wa habari wa wakati huo , ambaye alimsifia Jimmy kwa kuokoa maisha yake kwa kuzingatia hisia /mawazo ya ndani yalionesha na mnyama paka maarufu kwa jina la Jenny

View attachment 3317379
Inashangaza sana kwa mitikasi ile yote kapona😂
 
Hii ni kweli ,, sema binadamu wengi hupuzia ishara zinazotolewa na wanyama
Mfano
Bundi ,, yeye huweza kutabili mauti yanayomkabili mtu hasa akiwa mgonjwa maana wanadai bundi anauwezo wa kunusa seli zilizokufa katika mwili wa binadamu ..

Hivyo awapo angani na kupata harufu ya seli za binadamu zilizokufa uifuata hiyo harufu mpaka karibu na nyumba husika ambayo mtu huyo anapoishi ..

Na ndiyo wengi wetu hudhani bundi husababisha kifo
Hizi porojo hazijawahi kuthibitishwa popote
 
Halafu meli ya TITANIC haikuwa kubwa kiviile. Sema kwa wakati huo ndio ilikuwa meli kubwa kuliko zote. Ila pengine kwasasahv ingelinganishwa na meli kama mv victoria
Hata hizi unazozioma kunwa kwa sasa miaka 300 mbele zitakua ni ndogo tu
 
Na wewe fuga paka siku akilala nje na wewe lala nje
 
Halafu meli ya TITANIC haikuwa kubwa kiviile. Sema kwa wakati huo ndio ilikuwa meli kubwa kuliko zote. Ila pengine kwasasahv ingelinganishwa na meli kama mv victoria
hebu acha kuchekesha, likua kubwa ndio, usiifana na ki mv viktoria kachoingia mala 5 kwa titanic. Ngoja nikup calcuulations ndogo then upige hesabu mwenyewe.

Angalia
ilikua na uwezo wa kubeba watu wangapi?
ilikua na vyumba vingapi vya kulala?
ilikuwa na wafanyakazi wangapi?
ilikua na restaurants ngapi?
iliingiza magari mangapi?
ilibeba mizigo ya watu tani ngapi?
ilibeba mizingo ya mli husika kama vyakula vinywaji nk tani ngapi?


achana na mengine takuchoshwa, tafuta hizo details tu then utapata jibu, alafu eti unaifananisha na mv viktoria are you even serious? ndio sasa hivi ziko meli kubwa kuizidi titanic lakini usiifananishe na hiko ki mv viktoria chenu.
 
hebu acha kuchekesha, likua kubwa ndio, usiifana na ki mv viktoria kachoingia mala 5 kwa titanic. Ngoja nikup calcuulations ndogo then upige hesabu mwenyewe.

Angalia
ilikua na uwezo wa kubeba watu wangapi?
ilikua na vyumba vingapi vya kulala?
ilikuwa na wafanyakazi wangapi?
ilikua na restaurants ngapi?
iliingiza magari mangapi?
ilibeba mizigo ya watu tani ngapi?
ilibeba mizingo ya mli husika kama vyakula vinywaji nk tani ngapi?


achana na mengine takuchoshwa, tafuta hizo details tu then utapata jibu, alafu eti unaifananisha na mv viktoria are you even serious? ndio sasa hivi ziko meli kubwa kuizidi titanic lakini usiifananishe na hiko ki mv viktoria chenu.
Ufahamu wake ndipo ulipoishia haina haha ya kuumiza kichwa 😂😂😂😉
 
Back
Top Bottom