Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Kumtambulisha “Babiloni Mkubwa”

KITABU cha Ufunuo kina majina ambayo yana maana ya mfano. (Ufunuo 1:1) Kwa mfano, kinataja mwanamke ambaye jina “Babiloni Mkubwa” limeandikwa katika paji la uso wake. Kinasema kwamba mwanamke huyo ameketi juu ya “umati na mataifa.” (Ufunuo 17:1, 5, 15) Kwa kuwa hakuna mwanamke halisi anayeweza kufanya hivyo, lazima Babiloni Mkubwa awe mwanamke wa mfano. Kwa hiyo, kahaba huyo wa mfano anawakilisha nini?

Kwenye Ufunuo 17:18, mwanamke huyohuyo wa mfano anatajwa kuwa “lile jiji kubwa lililo na ufalme juu ya wafalme wa dunia.” Jina “jiji” linarejelea kikundi cha watu. Kwa kuwa ‘jiji hilo kubwa’ linaongoza “wafalme wa dunia,” lazima yule mwanamke anayeitwa Babiloni Mkubwa awe shirika lenye uvutano ulimwenguni pote. Linaweza kuitwa milki ya ulimwengu. Milki ya aina gani? Ya kidini. Ona jinsi maandiko mengine katika kitabu cha Ufunuo yanavyotusaidia kufikia uamuzi huo.

Milki inaweza kuwa ya kisiasa, ya kibiashara, au ya kidini. Mwanamke anayeitwa Babiloni Mkubwa si milki ya kisiasa kwa sababu Neno la Mungu linasema kwamba “wafalme wa dunia,” au wanasiasa wa ulimwengu huu, “walifanya uasherati” naye. Uasherati wake ni mapatano ambayo amefanya na watawala wa dunia na ndiyo sababu anaitwa “kahaba mkubwa.”—Ufunuo 17:1, 2; Yakobo 4:4.

Babiloni Mkubwa hawezi kuwa milki ya kibiashara kwa sababu “wanabiashara wa dunia,” watamlilia atakapoharibiwa. Isitoshe, wafalme na wanabiashara watamwangalia Babiloni Mkubwa wakiwa “mbali.” (Ufunuo 18:3, 9, 10, 15-17) Kwa hiyo, ni wazi kwamba Babiloni Mkubwa, si milki ya kisiasa wala ya kibiashara, bali ni milki ya kidini.

Hilo linathibitishwa na ile taarifa ya kwamba Babiloni Mkubwa anapotosha mataifa yote kwa ‘mazoea yake ya kuwasiliana na pepo.’ (Ufunuo 18:23) Kwa kuwa mazoea yote ya kuwasiliana na pepo hutokana na dini na roho waovu, haishangazi kwamba Biblia inamwita Babiloni Mkubwa “makao ya roho waovu.” (Ufunuo 18:2; Kumbukumbu la Torati 18:10-12) Pia, milki hiyo inapinga vikali dini ya kweli, ikiwatesa “manabii” na “watakatifu.” (Ufunuo 18:24) Kwa kweli, Babiloni Mkubwa anachukia sana dini ya kweli hivi kwamba anawatesa kikatili na hata kuwaua “mashahidi wa Yesu.” (Ufunuo 17:6) Hivyo, ni wazi kwamba mwanamke huyo anayeitwa Babiloni Mkubwa anawakilisha milki ya ulimwenguni pote ya dini ya uwongo, inayotia ndani dini zote zinazompinga Yehova Mungu


Rejea

Biblia inafundisha nini hasa? @ jw.org chini ya kichwa machapisho>vtabu
Kwanini mnapenda sana kupindisha maandiko ninyi?

Dhambi hii itawatafuna nawaambieni...

Ufunuo inatoa fasiri ya mwanamke ni nani na imesema wazi kuwa ni mji mkuu,wewe unakuja na maana yako kuwa ni milki ya kidini,unatoa wapi hii? Unataka kusema kuwa malaika hakuwa anajua alichokuwa akisema? Tena alikuwa anatoa TAFSIRI siyo kwamba alikuwa anazungumza kwa mafumbo kwasababu tayari Yohana alikuwa ameshapewa mafumbo na alikuwa anataka ufafanuzi.....

Hii dhana ya mwanamke kuwa kanisa au milki ya kidini haikubaliani kabisa na unabii huu.Siyo kila mahali anapotamkwa mwanamke kwenye unabii ni kanisa.....

Kanuni ya kufasiri unabii inaeleweka,kuna maeneo Mungu ametoa ufafanuzi wa mafumbo na kuna sehemu hajatoa,kule alikotoa kwanini mnakataa maana hiyo na kutafuta yenu?

Sijui ni kwanini mnaendelea kujidanmganya....
 
Moderator nafikiri ni wakati muafaka wakuondoa hizi post za kidini kwenye hii forum naona maada za kidini zimeibuka kwa kasi sana kwenye jamii forum,nafikiri sio vizuri hizi mada kuendelea kutamalaki.
 
Kwaiyo tufanyeje
Tokeni kwake msishiriki dhambi zake, kwani huyo mwanamke kahaba ameandaliwa ghadhabu na Mungu na atakinywea katika kikombe cha ghadhabu ya uasherati wake pasipo kuchangnywa na maji. Ufunuo 18:4-6
 
Hapo ni kuomba Mungu maana OMANI ingawa mh!!!!
 
Moderator nafikiri ni wakati muafaka wakuondoa hizi post za kidini kwenye hii forum naona maada za kidini zimeibuka kwa kasi sana kwenye jamii forum,nafikiri sio vizuri hizi mada kuendelea kutamalaki.
naona unata na moderator afute pia na dhana ya kuwako kwa Mungu duniani. ukiona hivyo ujue watu wanataka kufahamu haya mambo ya Mungu vizuri.usipoyajua haya mambo ya Mungu mapema utazeeka vibaya,utakuja kuwa mchawi uzeeni au mganga wakienyeji
 
Pole sana ila inabid umpate kiongoz wa kanisa anaweza akawa na majibu mazur sana
 
Mimi ni roman catholic
kwa mroma mwenzangu
atakayeweza kunielewesha, kiunagaubaga zile sanamu kanisani ni za nini? Kwanini maandiko yamepinga na still bado zipo? vp kwenye salama Maria kuna sehemu tunatamka mama wa Mungu je ni halali?. Ntaendelea kuuliza zaidi
Nb hayo maswali hasa la sanamu limenifanya niwe mgumu wa kwenda kanisani kabisa.
Pole sana inabid upate mtaalam haswa
 
Unataka copy and paste ipi ili ukae kimya? Mleta uzi hajatoa maelezo.
Copy and paste kutoka makao makuu ya Jehova's Witness Brooklyn New York. Unajifanya hujui ulikoitoa hii uliyoweka hapo juu?
 
Mtashindana na Vatican lakini hamtashinda.
 
huenda ukawa "sahihi" na mapokeo uliyopokea toka kwa wanazuoni wa kikundi chako cha kisabato nawe kuendelea kuwahadaa walimwengu wasio na elimu ya dini na ya imani ya kikatoliki, ila swali langu, je Mungu huwaacha wenye haki wapotee..?? kama siyo, "haki" ipo katika "usabato" (kwa mujibu wa mafundisho yenu), na usabato una karibia miaka 200, je kwanini kikundi hiki cha wenye "haki" mbali na kutumia maarifa yao kueneza "haki" kwa "wasio na haki"?... kwanini utawala wa "kishetani" (kanisa katoliki/waprotestitanti) halijawahi kuadhibiwa na Mungu kwa Mungu kuwaonesha "wenye haki" njia sahihi???
Kaka una hoja nzito..
 
Tanzania haina Dini hila watu wake wana Imani wanazo Amini.Hivyo mtu kuja na mafundiyosho ya kushambulia dhehebu moja tu siyo kitu kizuri.In short I know very well the History of the Church.Hivyo kuzungumzia upande mmoja wa shilingi sio sawa,mfano mtu anaweza kuwa anamini kunywa chai ya rangi au kula baadi ya chakula ni dhambi kutokana na uelewa wa kifungu fulani cha maandiko,lakini kuna sehemu maandiko yana ruhusu kula vitu vyakula vyote na visiitwe najisi kwani kinacho mtoka mtu ndio kitiacho najisi.
 
Hujaelewa swali langu, soma tena.
Ngoja nikuache mkuu. Ila tu tambua kuwa hapa JF kuna watu wa kila aina. Unapo-copy na ku-paste habari basi uwe tayari kuitetea hasa kama umeitoa kwenye source yenye mauzauza na isiyo na hadhi ya kuchangia lolote kuhusu mada husika. Happy New Year !
 
Vatican ndiko palipo na kiti cha enzi cha ibilisi!

Si mnasema yule mnyama kakaa mahali patakatifu. Kwa ninilei hii vatcan kiwe kiti cha ibilisi? Pia mnapoandika mavi yenu mwe mnatumia akili angalau kidogo zilizoko matakoni, biblia ina sema shetani huzunguka huku na huku iweje mseme ana kiti? Hopeless!
 
Mwanamke (yule Babeli) wa Ufunuo 17 anaelezwa kuwa

“alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, Siri [2 The. 2:7], Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba” [Ufu. 17:5, KJV].

Asema hivi yule Nabii:

“Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu.” Babeli anatangazwa tena kuwa ni “mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wa nchi.” Ufunuo 17:4-6,18.
ae7a1c4de023bbda2da0a25e30e725f6.jpg

Tyndale aliuliwa na utawala wa kipapa kwa kutafsiri biblia...



Mamlaka ile iliyodumisha utawala wake wa kidikteta juu ya wafalme wa Ulimwengu ule wa Kikristo kwa karne nyingi ni Roma. Rangi ile ya zambarau na nyekundu, dhahabu na kito cha thamani, na lulu, huonyesha waziwazi picha ya utukufu wake na fahari yake iliyozidi ile ya kifalme [angalia pia rangi za sare za viongozi na mapambo yao],
da95cf61b762f5a8bb3ffa13c0e24c5f.jpg

b601c77df03518a6574d5fdbdf97b1ea.jpg


mambo ambayo jimbo lile la Roma ( Vatikani), lenye majivuno makuu, lilijigamba kuwa nayo. Wala hakuna mamlaka [serikali] nyingine ambayo kweli ingetangazwa kuwa ilikuwa imelewa kwa damu ya watakatifu,” kama ya kanisa lile ambalo kwa ukatili mbaya sana limewatesa wafuasi wake Kristo.

Babeli pia anashtakiwa kwa dhambi ya kuungana isivyo halali [kuzini] na “wafalme wa nchi.” Ilikuwa ni kwa njia ya kujitenga mbali na Bwana, na kuungana na washenzi [wapagani], ndipo kanisa lile la Kiyahudi likageuka na kuwa kahaba [Soma Ezekieli 23]; naye Roma [kama kanisa], akifanya uasherati [ukahaba] unaolandana kabisa na ule na kutafuta msaada [kuungwa mkono] toka kwa mamlaka [serikali] zile za kidunia, anapata lawama iyo hiyo.

014c67cfdb1f454cb6ffad5c5931e2e5.jpg

2d74043e7497ad8b2d6a027cbaa597c5.jpg
hayo ni mawazo yako,

hayahusiani na maono ya Yohana aliyoyaandika katika kitabu chake cha Ufunuo

maono hayo aliyaona yeye mwenyewe akiwa peke yake

akasema hivi, Mtu awaye yote asiongeze neno wala asipunguze neno

ulikuwapo wakati Yohana akiona hayo Maono?

Je ni Yohana amekutokea na kukutafasiri hiyo?

km hajakutokea hii tafasiri unaitoa wapi?

usimlishe maneno
 
hivi mnafikiri Roman Catolic ni wajinga kiasi gani?,

wamekaa na bibilia hii kwa miaka 1500 kabla haijatoka nje wakiihariri,

wao ni wajinga kiasi gani mpaka waache maneno ya kuwakashifu wao?

kwa sababu Bibilia hii ilikuwa ni katiba ya utawala wao (Roman Empire )

mnaobadilisha maandiko ninyi ndio wajinga na si Kanisa Katoliki
 
Here we go again. Seventh Adventists (Wasabato) at work. Yaani bila Papa na ukatoliki hamna dini. Hata hiyo misingi ya Usabato huwa mnaihubiri saa ngapi kama kazi yenu kuu ni kupambana na Papa na ukatoliki 24/7? Nyinyi mnaamini nini? Wokovu unapatikanaje? Kwa kusoma na kufuata mafundisho ya Bibi Ellen G. White? Kwa kutokula samaki wenye magamba, wanyama wasio na kwato zilizogawanyika na wale wasiocheua? Ni kwa kuabudu Jumamosi? Ni kwa kutokunywa chai, kahawa na soft drinks? Ni kwa kukurupuka na kuwa na kiherehere cha kuhusisha kila tukio na unabii wa vitabu vya Daniel na Ufunuo? Usabato ni nini? Mtu atakwenda mbinguni kwa sababu ni Msabato?

Inawezekana kweli Papa ni ajenti wa shetani na kahaba mkuu wa Ufunuo lakini je, hili linawasaidiaje nyinyi kama Wasabato? Mbona mko so obsessed na Papa na Wakatoliki? Dini na madhehebu mengine yote yako sawa isipokuwa Wakatoliki? Mbona siwaoni mkiwachimba mf. Mormons au Jehova's Witness? Why Catholics only? Au mna bifu la kihistoria na Papa na ukatoliki?

Samahani kwa maswali mengi na natumaini kwamba hutatoa povu na badala yake utajaribu kutuelimisha kuhusu kikundi hiki cha kifarisayo (washika sheria za Musa) kiitwacho Seventh Adventists, kiundi chenye mauzauza mengi yasiyofungamana na mafundisho ya Biblia.

Anyway, Happy New Year mkuu (kama mnasherehekea mwaka mpya)! Naona mwaka mpya Wasabato mmeuanza vizuri na Wakatoliki aisee mpaka waombe poo [emoji23][emoji23][emoji23]. Post zaidi ya 7 hivi za kuanika ushetani wa Papa na ukatoliki tangu 2017 uanze. Ingekuwa mnashambulia let's say Uislamu naamini threads zenu zingekuwa zinafutwa. Komaeni na "mashetani" na "makahaba" wa kikatoliki mpaka kieleweke ila tu hakikisheni kuwa na nyie mko sawa kiimani!
Mie ni Mlutheran, ila umeongea points sana mkuu, big up sana[emoji109] [emoji106] [emoji4]
 
Back
Top Bottom