Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Mfahamu kahaba mkuu wa Ufunuo 17

Unamfahamu mfalme Nimrod aliyekaa babeli na kuleta kuabudu miungu...au hujui kma ibada zte za miungu zlianzia babeli?au hujui Israeli yakaa ikizungukwa na mataifa ya babeli yaliyokua yakiabudu miungu...au hata upagan wa warumi na mashariki ya kati yte hujui ulitokea wap?au bx hujui hata miji iliyokua inatengeneza ufalme wa babeli(babeli ya nebukadreza)
Huyo ni dumb head...ana copy na ku-paste...hivyo hawezi kutetea alichoandika....Atakusumbua....utapoteza muda...mimi najua jindi ya ku-deal naye
 
Ukisema karne ya 15 unamaanisha miaka ya 1400-1499 ss je marthin luther alikuepo kipin hiki au unataka kutudanganya pia...mna unajaribu kuleta kila unachoweza il kujarbu kuwin na hoja ishakukataa ss...maswal yngu hujbu unakimbia

Anakuambia Roma Vatican...daah..
 
Nawasaidia walio na mashaka Maria kuitwa mama wa MUNGU. Twende pamoja kwa busara wala sio kwa hasira.
Mfano hai. Eliza amezaa mtoto wa kiume jina lake John. Ni jambo lisilopingika kuwa Eliza ataitwa mama John. Au kuna kwenye ukakasi ktk hilo????

Swali la msingi la kujiuliza ni;
1. Ni Kweli Maria alimzaa Yesu??
2. Kama ni kweli. Kwanin asiitwe mama Yesu?
3. Je, Yesu ni MUNGU?
Tuanzie hapo kwanza ntarudi kimaandiko zaidi

Sent from my TECNO-Y6 using JamiiForums mobile app
 
BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NI NANI AU NI NINI?
Biblia inamfunua..
1. Kwanza tunaona BABELI MKUU huyu ameonyeshwa kuwa ni mwanamke, maana anaitwa "mama" sote tunaelewa sifa ya mama ni ya jinsi ya kike.
Je, kwa mujibu wa Biblia mwanamke hutumika kuwakilisha nini anapotumika kama kielelezo?
- Katika Biblia "mwanamke" hutumika kuwakilisha "JAMII YA WATU WA MUNGU" ambao katika agano la kale watu hao walikuwa ni taifa la "ISRAELI"
Tunaona katika Hosea Mungu akiongea na watu wake kama aongeae na mwanamke
Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
HOSEA 2 : 19
"Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
YEREMIA 3 : 14.
Katika zama za agani jipya, ambapo hakuna tofauti tena kati ya Myahudi na asiye Myahudi, mwanamke anawakilisha watu wa Mungu kwa maana ya "KANISA"
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
2 KORINTHO 11 : 2
Kwa sababu BABELI MKUU atatokea wakati wa Agano jipya, basi BABELI huyo ATAJITOJEZA KATIKA SURA YA KANISA!
Tumejua sasa KAHABA MKUU ni kanisa kumbe.
Mijadala bora huendeshwa kwa namna njema na ya kila mmoja kujitahidi kuelewa ni wapi mwingine ana tatizo kisha wote kwa pamoja kushirikiana kulitatua tatizo hilo kisha mnasonga mbele,naona jambo hili kwenye mjadala wangu na wewe limekuwa gumu....

Tatizo langu la kwanza kwenye mjadala huu ni hili na fasiri ya mwanamke kwenye unabii wa Ufunuo 17.Nimekueleza tatizo hili na nimekuonesha vile ambavyo maandiko yanaonesha kuwa mwanamkekwenye unabii huu hana maana kama unayoiweka wewe na nimekupa ushahidi...

Badala ya kushughulika na tatizo hilo naona unaelekea kwenye mambo mengine kabisa na unaendelea kurudia maelezo yale yale ambayo mimi nimeshayapinga kwa hoja na ushahidi,sasa mkuu tutaweza kuelewana hapa kweli?

Nilikuambia kuwa kwenye unabii huu mwanamke siyo kanisa ni mji lakini bado tu naona unaendelea kurudia kauli yako ya kusema mwanamke ni kanisa bila ya kueleza ni wapi kwenye unabii huu mwanamke ameelezwa kama kanisa....

Umenukuu maelezo kwenye maeneo mengine ya biblia kuonesha kuwa mwanamke ni kanisa,hili ni kosa kubwa.Nasema ni kosa kwasababu kiutaratibu,unapokuta unabii na kuna mafumbo kwanza unachopaswa kuanza nacho ili uelewe unabii ule ni kuangalia kwenye huo unabii kama mafumbo yale yamefafanuliwa.....

Ukikuta hilo halipo unaangalia maana ya jumla kimantiki kwenye unabii huo kama utaweza kuelewa maana ya mafumbo yale,ukikosa unakwenda kwenye maeneo mengine kwenye biblia kwenye unabii unaorandana na huo ili kuona kama kuna maneno yale yale yameelezwa na kama yamefasiriwa iliupate maana ya mafumbo husika....

Ukikosa unaelekea kwenye nabii zingine kuangalia kama kuna maneno hayo na kama yamefafanuliwa na ukikosa unaangalia maeneo mengine kwenye biblia bila kujali kama ni ya unabii au la ili kuweza kupata maana ya mafumbo hayo na ukikosa basi unaangalia vyanzo vingine nje ya Biblia ili kukusaidia kuelewa maana ya mafumbo au maneno yaliyotumika kwenye unabii huo....

Nikiangalia kwenye unabii huu naona umeamua kabisa kuacha kuchukua hatua ya kwanza ambayo ndiyo bora kabisa na umekimbilia kwenye hatua ya tatu sijui ni kwanini.Kwenye unabii huu Mungu amesema mwanamke ni nani humo humo kwenye unabii huu,ni kwanini unahangaika na sijui Yeremia na akina Hosea?

Mkuu ndivyo tunaenda hivi kweli?

Tutaweza kuelewana namna ipi?
 
Msisahau kua dini ya kweli ni kuwajali yatima,wajane,wafungwa,walio na njaa ,wagonjwa n.k aya mambo mengine ni vyama tu . Na Yesu akawambia wanafunz wake nalikuja na njaa hamkunipa chakula,nalikua na kiu hamkunipa maji,nalikua ngonjwa hamkunitazama ,nalikua uchi hamkunipa nguo,Nao wakamjibu Bwana!Nilini tumekutendea hayo? Naye akawajibu,Amini nawambia yoyote amtendeaye mwanadamu kati ya haya atakua amenitendea Mimi.Kuna wengine wajiita wasabato wao ujiona wakamilifu sana binafs siwashangai Maana yesu baada ya kumponya mmama wa watu siku ya sabato wakamshambulia na kumjia juu wawezaje kufanya mambo haya sku ya Sabato? Yesu akawajibu Eenyi wanafiki Ngo'mbe wako akianguka shimoni sku ya sabato utashindwa kumuokoa? Kisa nisku ya sabato? Nawashangaa sana watu hawa mpaka wa leo bado hawakumuelewa Yesu,utakuta wanamaduka lakin sku ya sabato hawafungui NGO' kibaya zaid wengine wana maduka ya Madawa lakin hata ngonjwa wako awe na khali gani kamwe hawakuuzii dawa sku ya sabato yan wako tayar mgojwa apoteze maisha,Lakin utakuta wanatamba et ni dini ya kweli .Kimuingiacho mtu hakimtii najisi bali kimtokacho,mfano ukila kitimoto sio najsi lakin ukitoa tusi mdomon iyo ni najsi kwa maana umedhamilia na limetoka rohoni lakin jamaa zangu awakuelewi wanaona bola kudhini kuliko kula kiti moto!All in all din haimpeleki mtu mbinguni Bali matendo yake.

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Ni vema kujua malengo ya uanzishwaji wa dini fulani,mila za wakati husika na mabadiliko yake. Mfano,ukristo na uislam ulianzishwa enzi za kifalme,mitazamo yake yote pamoja na kuwa ya malengo ya Kimungu,imekuwa ya heshima za kifalme na kuheshimu tawala. Dini chache kama sabato zimeanzishwa kipindi cha mapinduzi ya viwanda na kupigania malighafi,hivyo zikawa zimeanzishwa pamoja na kuwa za Kimungu,lakini malengo makuu ilikuwa kupora raslmali kwa kuonyesha udhaifu wa ulaya kupitia njia iliyojificha kwa dini.Dini zilizoanza katika zama za habari kama ulokole nazo siku zote zitakuwa katika malengo,mila na taratibu zilizozianzisha. Malengo yanapokamilika watawala huachia kundi husika na minyukano kuanza. Ni bahati mbaya sana katika dini karibia zote malengo ya uanzishwaji hayawekwi wazi kwa waumini.

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Mijadala bora huendeshwa kwa namna njema na ya kila mmoja kujitahidi kuelewa ni wapi mwingine ana tatizo kisha wote kwa pamoja kushirikiana kulitatua tatizo hilo kisha mnasonga mbele,naona jambo hili kwenye mjadala wangu na wewe limekuwa gumu....

Tatizo langu la kwanza kwenye mjadala huu ni hili na fasiri ya mwanamke kwenye unabii wa Ufunuo 17.Nimekueleza tatizo hili na nimekuonesha vile ambavyo maandiko yanaonesha kuwa mwanamkekwenye unabii huu hana maana kama unayoiweka wewe na nimekupa ushahidi...

Badala ya kushughulika na tatizo hilo naona unaelekea kwenye mambo mengine kabisa na unaendelea kurudia maelezo yale yale ambayo mimi nimeshayapinga kwa hoja na ushahidi,sasa mkuu tutaweza kuelewana hapa kweli?

Nilikuambia kuwa kwenye unabii huu mwanamke siyo kanisa ni mji lakini bado tu naona unaendelea kurudia kauli yako ya kusema mwanamke ni kanisa bila ya kueleza ni wapi kwenye unabii huu mwanamke ameelezwa kama kanisa....

Umenukuu maelezo kwenye maeneo mengine ya biblia kuonesha kuwa mwanamke ni kanisa,hili ni kosa kubwa.Nasema ni kosa kwasababu kiutaratibu,unapokuta unabii na kuna mafumbo kwanza unachopaswa kuanza nacho ili uelewe unabii ule ni kuangalia kwenye huo unabii kama mafumbo yale yamefafanuliwa.....

Ukikuta hilo halipo unaangalia maana ya jumla kimantiki kwenye unabii huo kama utaweza kuelewa maana ya mafumbo yale,ukikosa unakwenda kwenye maeneo mengine kwenye biblia kwenye unabii unaorandana na huo ili kuona kama kuna maneno yale yale yameelezwa na kama yamefasiriwa iliupate maana ya mafumbo husika....

Ukikosa unaelekea kwenye nabii zingine kuangalia kama kuna maneno hayo na kama yamefafanuliwa na ukikosa unaangalia maeneo mengine kwenye biblia bila kujali kama ni ya unabii au la ili kuweza kupata maana ya mafumbo hayo na ukikosa basi unaangalia vyanzo vingine nje ya Biblia ili kukusaidia kuelewa maana ya mafumbo au maneno yaliyotumika kwenye unabii huo....

Nikiangalia kwenye unabii huu naona umeamua kabisa kuacha kuchukua hatua ya kwanza ambayo ndiyo bora kabisa na umekimbilia kwenye hatua ya tatu sijui ni kwanini.Kwenye unabii huu Mungu amesema mwanamke ni nani humo humo kwenye unabii huu,ni kwanini unahangaika na sijui Yeremia na akina Hosea?

Mkuu ndivyo tunaenda hivi kweli?

Tutaweza kuelewana namna ipi?
Nilitegemea ushushe ushahid kuhusu kahaba mkuu

Naona umeandika lawama tu

Ni kusema mjadala hauuwezi?

YHWH IS GOOD
 
Huyu anawapotezea muda tu ndugu sbb nlishamjengea hoja ambayo akakimbia na maswal hajajibu mpka leo pamoja na wenzie...leo kahaba katoka kua ukatoliki kawa mji wa vatican...hv unahisi wte n watoto kma ww kua unaeza kutuchanganyia maneno!hata hajui anatetea nini kaambiwa biblia inasema n mji kahama kutoka ukatolik kua mji...hya mbele ya mistari hyo kuna mistari inasema mji huo uko kati ya vilima saba yaani wafalme saba wamekaa...tukikwambia utaje utaweza..
Wewe hii mada huiwezi ,tulia ufundishwe

YHWH IS GOOD
 
Ukisema karne ya 15 unamaanisha miaka ya 1400-1499 ss je marthin luther alikuepo kipin hiki au unataka kutudanganya pia...mna unajaribu kuleta kila unachoweza il kujarbu kuwin na hoja ishakukataa ss...maswal yngu hujbu unakimbia
Wap nime generise luther alipinga ushetan wa roma karne ya 15?

Hivi kwann mnakurupuka hivo

Halafu unajifanya uliuliza swali

Mada na comments zangu nimeshajibu humu hadi HUKUMU YA KAHABA MKUU ROMA

YHWH IS GOOD
 
Trust me wewe unayejifanya kanisa lako ni la kweli kuliko Mengine..jehanamu inakusubiri acha mimi na rais Wang JPM tuendelee kuinyoosha nchi ili tukawe malaika hata huko mbinguni..nyie mnaotafuta wafuasi kwa nguvu endeleeni.

NB..USHAURI WA BURE
kaka kizuri chajitangaza kibaya chajiuza
fanyakazi acha kujifanya malaika na umekamirika. hakuna binadamu wa kumhukumu binadamu ni Mungu tu

Sent from my SM-J200H using JamiiForums mobile app
Kwanini mkiambiwa ukweli mnakuwa wakali hivo?

Mungu ametuasa tuonyane

YHWH IS GOOD
 
Kuabudu vinyago ni ukristo?

YHWH IS GOOD
Hilo somo LA Vinyago/Sanamu lilielezwa vzuri sana ktk thread zilizopita,hili la Kababa Mkuu wa Ufunuo 17 bado unarukaruka pasipo kujibu hoja.

In short uko affected na Mafundisho ya nabii mke EGW kwa anayejadili na wewe its a westage of time.

Kwanini hata cku moja cjasikia ukigusia zile tabiri zaidi ya nne kutoka kwa EGW/Miller/Bates kuhusu ujio wake Yesu.

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini mkiambiwa ukweli mnakuwa wakali hivo?

Mungu ametuasa tuonyane

YHWH IS GOOD
imani ni kitu kipana sana huwezi kukimaliza kwa hiyo muhimu ni kuamini na kuongelea zaidi kile kilichokuwa kwenye imana na dhehebu lako na kitu usichokijua hata nikikuelewesha utantolea tu macho...nnarudi kulekule kwamba kama unataka waumini upate sadaka huwezi kupata kwa kuongelea dini mwenzio so amini unachokiamini na ntaamini nnachokiamini kwa sababu huku niliko nnabarikiwa pia na usiforce tufanane.....
OVA

Kuna sehemu nimekuomba sadaka?

YHWH IS GOOD
 
Wewe hii mada huiwezi ,tulia ufundishwe

YHWH IS GOOD
Ungejibu hoja zangu ndo ungekua na ujasiri wa kunambia nkae kimya nachokiona umefika ukomo wa ulichokalilishwa ss unarudia rudia tu maneno yako
 
Back
Top Bottom