BABELI MKUU MAMA WA MAKAHABA NI NANI AU NI NINI?
Biblia inamfunua..
1. Kwanza tunaona BABELI MKUU huyu ameonyeshwa kuwa ni mwanamke, maana anaitwa "mama" sote tunaelewa sifa ya mama ni ya jinsi ya kike.
Je, kwa mujibu wa Biblia mwanamke hutumika kuwakilisha nini anapotumika kama kielelezo?
- Katika Biblia "mwanamke" hutumika kuwakilisha "JAMII YA WATU WA MUNGU" ambao katika agano la kale watu hao walikuwa ni taifa la "ISRAELI"
Tunaona katika Hosea Mungu akiongea na watu wake kama aongeae na mwanamke
Nami nitakuposa uwe wangu kwa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.
HOSEA 2 : 19
"Rudini, enyi watoto wenye kuasi, asema BWANA; maana mimi ni mume wenu; nami nitatwaa mtu mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta hata Sayuni;
YEREMIA 3 : 14.
Katika zama za agani jipya, ambapo hakuna tofauti tena kati ya Myahudi na asiye Myahudi, mwanamke anawakilisha watu wa Mungu kwa maana ya "KANISA"
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
2 KORINTHO 11 : 2
Kwa sababu BABELI MKUU atatokea wakati wa Agano jipya, basi BABELI huyo ATAJITOJEZA KATIKA SURA YA KANISA!
Tumejua sasa KAHABA MKUU ni kanisa kumbe.
Mijadala bora huendeshwa kwa namna njema na ya kila mmoja kujitahidi kuelewa ni wapi mwingine ana tatizo kisha wote kwa pamoja kushirikiana kulitatua tatizo hilo kisha mnasonga mbele,naona jambo hili kwenye mjadala wangu na wewe limekuwa gumu....
Tatizo langu la kwanza kwenye mjadala huu ni hili na fasiri ya mwanamke kwenye unabii wa Ufunuo 17.Nimekueleza tatizo hili na nimekuonesha vile ambavyo maandiko yanaonesha kuwa mwanamkekwenye unabii huu hana maana kama unayoiweka wewe na nimekupa ushahidi...
Badala ya kushughulika na tatizo hilo naona unaelekea kwenye mambo mengine kabisa na unaendelea kurudia maelezo yale yale ambayo mimi nimeshayapinga kwa hoja na ushahidi,sasa mkuu tutaweza kuelewana hapa kweli?
Nilikuambia kuwa kwenye unabii huu mwanamke siyo kanisa ni mji lakini bado tu naona unaendelea kurudia kauli yako ya kusema mwanamke ni kanisa bila ya kueleza ni wapi kwenye unabii huu mwanamke ameelezwa kama kanisa....
Umenukuu maelezo kwenye maeneo mengine ya biblia kuonesha kuwa mwanamke ni kanisa,hili ni kosa kubwa.Nasema ni kosa kwasababu kiutaratibu,unapokuta unabii na kuna mafumbo kwanza unachopaswa kuanza nacho ili uelewe unabii ule ni kuangalia kwenye huo unabii kama mafumbo yale yamefafanuliwa.....
Ukikuta hilo halipo unaangalia maana ya jumla kimantiki kwenye unabii huo kama utaweza kuelewa maana ya mafumbo yale,ukikosa unakwenda kwenye maeneo mengine kwenye biblia kwenye unabii unaorandana na huo ili kuona kama kuna maneno yale yale yameelezwa na kama yamefasiriwa iliupate maana ya mafumbo husika....
Ukikosa unaelekea kwenye nabii zingine kuangalia kama kuna maneno hayo na kama yamefafanuliwa na ukikosa unaangalia maeneo mengine kwenye biblia bila kujali kama ni ya unabii au la ili kuweza kupata maana ya mafumbo hayo na ukikosa basi unaangalia vyanzo vingine nje ya Biblia ili kukusaidia kuelewa maana ya mafumbo au maneno yaliyotumika kwenye unabii huo....
Nikiangalia kwenye unabii huu naona umeamua kabisa kuacha kuchukua hatua ya kwanza ambayo ndiyo bora kabisa na umekimbilia kwenye hatua ya tatu sijui ni kwanini.Kwenye unabii huu Mungu amesema mwanamke ni nani humo humo kwenye unabii huu,ni kwanini unahangaika na sijui Yeremia na akina Hosea?
Mkuu ndivyo tunaenda hivi kweli?
Tutaweza kuelewana namna ipi?