TATIZO UNA MIX MAMBO
KAA UTULIE UFUNZWE,haya mambo tatizo mapadri hawezi kuwaambia maana watawapoteza wakose sadaka
Falme hizo zinawakilishwa na Pembe 10 (Dan. 7:8). "Pembe"
ni "Wafalme" au "Falme" (Dan. 7:24). Falme 10 zilijikomboa toka
ukoloni wa Kirumi ulipoangushwa mwaka 476 B.K. na mataifa ya
kipagani ya Ulaya Kaskazini. Falme 10 ni Uingereza, Ufaransa,
Ujerumani, Uswisi (Switzerland), Ureno, Hispania, Italia,
Heruli, Wavandali (Vandals), na Waostrogothi (Ostrogoths).
Katika Danieli 2 zimewakilishwa na Vidole 10 vya Nyayo (Dan.
2:41,42). Kuhusu ukatili wao soma historia. Zilimsaidia, tena
zitamsaidia papa kuua watakatifu (Ufu.17:12-14).
HAYA MATAIFA YATAKAYOMSAIDIA , NADHANI UNAYAJUA SASA , NADHANI UNAONA HARAKATI ZA PAPA KUZURU HAYO MATAIFA
YHWH IS GOOD
Na katika hizo pembe kumi, ndipo inaibuka pembe ndogo na kuzinagusha pembe tatu yaani falme tatu ambazo ni Ostrogoths, heruli na vandals. Daniel 7: 24. "Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu." Hii pembe ndogo ndiye pia mnyama wa ufunuo 13:1 " Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru".
Tazama mfanano uuliopo kati ya Daniel na ufunuo.
Daniel 7:25. "Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati."
Ufunuo 13:6-8 "Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia".
Ufafanuzi
1.Kunena kinyume chake alieye juu ni pale kanisa katoliki lilipobadili amri za Mungu.
2. Jina la Makufuru ni VACARIUS FILII DEI yaani mwakilishi wa Mwana wa Mungu kama ajiitavyo papa. Makufuru!hakuna mtu awezaye kulinganishwa na Mungu.
3. Biblia inasema kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha mwanakondoo atamsujudia mnyama huyu. hata mijadala humu inaonyesha watu wengi wanmsujudia huyu mnyama. wengine kwa kufahamu kabisa wengine kwa kufuata mkumbo tu.
4. Mwisho wa wakati dunia itagawanywa mafungu mawili; aidha umwabudu mnyama na sanamu yake (Jumapili) ama umwabudu Mungu wa Mbinguni kwa kutii amri zake kama zilivyo katika kitabu cha kutoka 20 na sabato ya siku ya saba, jumamosi ikiwemo katika amri hizo.