Mfahamu marehemu Sheikh Ali Muhsin Barwani (1919 - 2006)

Mohamed katika maandishi yako kuhusu wapigani uhuru wa nchi hii wasiotajwa,umetilia mkazo sana watu
wa pwani.Huko bara kuna watu walifanya makubwa kumuwezesha Nyerere.Kwa kuanzia tafiti juu ya mabibi hawa,Fatna binti Mursali wa Arusha na dada yake Hawa binti Feruzi wa Singida uone ukweli uliofichwa.

Kivava,
Hakika mie nawajua zaidi wazee wangu wa hapa Dar es Salaam na ndiyo
niloweza kuhifadhi historia yao.

Ningefurahi sana mtu kama wewe unaowajua wazee wetu wengine kama
hao ungefanya utafiti na ukaandika habari zao.
 
Zamiluni Zamiluni,
Umri unakwenda na kadar.

Ondoa hofu.
Allah anasema hata ukijificha kwenye ngome mauti yatakufika.
Kweli MS, hata tukijenga mlingoti(Tower) wakenda juu !! nishaondoa khofu....
Wamaa Qadar Allah, haq Qaderihi !!
 
Zamiluni labda nikuulize. Niuliwe kwa uovu upi au kwa kulipiziwa yupi mie niliyemuua au kwa ubaya upi mkubwa niliofanya?
 
Mohamed katika maandishi yako kuhusu wapigani uhuru wa nchi hii wasiotajwa,umetilia mkazo sana watu
wa pwani.Huko bara kuna watu walifanya makubwa kumuwezesha Nyerere.Kwa kuanzia tafiti juu ya mabibi hawa,Fatna binti Mursali wa Arusha na dada yake Hawa binti Feruzi wa Singida uone ukweli uliofichwa.

Nnamjuwa sana huyu bi Hawa bint Feruzi wa Singida, niliwahi kumtaja katika mijadala humu JF zamani sana. Alikuwa ni rafiki mpenzi wa Marehemu bibi ya mume wangu nae pia akiitwa Bi Hawa.

Bibi huyu wa Singida nnamkumbuka sana sauti yake nyembamba na ya upole, huku akitetema tetema uzeeni na meno yake ya mdaa.

Naam, alikuwa ni mwana harakati wa Singida toka enzi ya mkoloni.

Mwenyeezi Mungu amghufirie na ampe rehma zake na amuingize peponi Bibi yetu huyu.

Machozi yanantoka.

Umenipeleka mbali sana.
 
ukweli uliofichwa? nani anauficha? sema ukweli ambao wenyewe hawataki kuandika
 
jMali,
Sidhani kama hilo swali umeuliza ukitegemea upate jibu kutoka kwetu.

Nasema hivyo kwa kuwa jibu lake liko wazi mno.
 
ukweli umefichwa na nani? kuna mtu yoyote aliandika kitabu kwa mfano juu ya huyo bi Mursali wa Arusha, halafu ikatokea mamlaka ikapiga marufuku kitabu?
 
Inaelekea wewe si mweledi katika tatizo hili la historia ya uhuru wa Tanganyika.

Hebu ingia hapa uone ''ladha,'' ya mjadala huu jinsi ulivyokuwa mkali miaka
michache iliyopita ikichagiwa na akina Mwanakijiji, Faiza Fox, Ritz, na wengine wengi:
KUTOKA JF: AFRICA EVENTS LILIPOCHAPA KUMBUKUMBU YA ABDUL SYKES 1988 - Mohamed Said

Labda huenda ukapata mwanga kidogo.
Ukitaka taatifa zaidi ingia:

mohammedsaid.com
 
Nnamjuwa sana huyu bi Hawa bint Feruzi wa Singida, niliwahi kumtaja katika mijadala humu JF zamani sana. Alikuwa ni rafiki mpenzi wa Marehemu bibi ya mume wangu nae pia akiitwa Bi Hawa.

Bibi huyu wa Singida nnamkumbuka sana sauti yake nyembamba na ya upole, huku akitetema tetema uzeeni na meno yake ya mdaa.

Naam, alikuwa ni mwana harakati wa Singida toka enzi ya mkoloni.

Mwenyeezi Mungu amghufirie na ampe rehma zake na amuingize peponi Bibi yetu huyu.

Machozi yanantoka.

Umenipeleka mbali sana.
Dada yangu wa imani, bi Hawa na mswaki wake wa mdaa ni mdogo wake nyanya 'angu 'mzaa baba yangu,hatma yake nitaileta punde
 
Amma kwa hakika dunia ni ndogo, naam, nikimfaham sana Bi Hawa kutokana na Bibi mkwe wangu nae pia akiitwa Bi Hawa, na Bi Hawa katika uhai wake nimemuona mara mbili aliwahi kuja Dar akifikia hapo kwa Bi Hawa mwenzake Kariakoo na pia nilimuona Singida mara mbili kwa kumsindikiza Bibi mkwe wangu alipomlazimisha mjukuu wake (mume wangu) ampeleke Singida kwa gari maana "mabasi siyawezi" (akideka kwa mjukuu wake) na mjukuu wake alikuwa hamvunji akampeleka. Nnakumbuka tupo njani kwenye gari tumekaa kimya, mara bibi ananambia, sasa hivi zamu yako kukaa mbele na dereva, tukirudi zamu yangu.

Biti Feruzi, akinitania "mie ndiyo wa awali, wewe mtunze tu lakini kaa ukijuwa nipo mwenyewe tulotoka mbali". Na kweli anamjuwa toka anazaliwa.

Nasubiri kwa hamu kubwa sana habari za Biti Feruzi. Nami ntatia yangu japo kiduchu nnayoyajuwa kuhusu Bibi yetu huyu.
 
Waislam leo tunajivunia wazee wetu kuwemo kwenye Historia ya nchi hii sama na Al Alama Mohamed Said aliyetupa mengi mno ya kujivunia, kwanini Waislam tusijivunie kuliko mwengine yeyote yule. Mwenyeezi Mungu akuzidishie kila la kheri Alama wetu na akupe umri mrefu tuzidi kufaidika na uliyonayo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom