Mfahamu mdudu Kantangaze (Tuta absoluta)

Mfahamu mdudu Kantangaze (Tuta absoluta)

Tin guy

Member
Joined
Nov 16, 2017
Posts
27
Reaction score
21
MDUDU KANTANGAZE ( Tuta absoluta) AZIDI KUUA KILIMO CHA NYANYA TANZANIA.


Leo nimeona habari iliyotolewa na ITV kuhusu zaidi za ekari mianane za Nyanya katika kijiji cha Ngarenanyuki wilaya ya Arumeru mkoani Arusha kuteketezwa na Kantangaze na hivyo nimeamua kuandika machache kuhusu huyu mdudu wenda yakawasaidia wengi.

CHIMBUKO
Chimbuko la Kantangaze ni America ya Kusini miaka ya 80's. Kutoka huko alienea sehemu za Ulaya hususani Spain na katika hali ya Kimediterania. Mpaka sasa mataifa yaliyo Kaskazini mwa Africa mfano Tunisia yameshashambuliwa vikali. Nchi Tanzani mdudu huyu kwa mara ya kwanza aliripotiwa mwaka 2014 ambapo kati ya mwaka 2014 - 2015 na maeneo ya kwanza kuathirika sana ambayo ni Ngabobo, Ngarenanyuki na King'ori wilayani Arumeru ambayo ni maarufu kwa uzalishaji nyanya yalipata hasara kubwa.Mdudu huyu husambazwa kwa kasi sana hususani kupitia mazao yaliyoharibiwa sokoni na kutumia mbegu zenye masalia.Hivyo hupaswi akufikie ndo umfahamu.

MUONEKANO
Tuta absoluta hutaga mayai kati ya 250 mpaka 300 katika kipindi cha uhai wake ambao ni kati ya siku 28-30.Akiwa mkubwa- huonekana katika umbo la kipepeo ( moth) mdogo mwenye ukubwa wa mm 6 hivi. Kipepeo huyo huwa na rangi ya Kijivu chenye Ukahawia ( grey-brown).

Akiwa Kiwavi ( Caterpillar)- Kiwavi mchanga sana huwa na rangi ya Njano ( Yellowish).Kadiri anavyokuwa hubadilika na rangi ya njano yenye ukijani ( yellow-green) na michirizi myeusi ( black bands) huota nyuma ya kichwa. Akikua huwa na rangi ya waridi ( pink).

Pupa:- Pupa wake ana rangi ya kahawia isiyokolea ( light brown).

UHARIBIFU
Hushambilia sana nyanya.Pia ana uwezo wa kuharibu viazi mviringo.Hatua ya ukuaji ya Tuta absoluta inayoshambia mmea ni KIWAVI ( Caterpillar) .Kiwavi huchimba majani, mashina na sehemu ya taji la tunda la nyanya. Pia huchimbua matunda ya nyanya yaliyo na ukijani na kufanya uingiaji wa vijidudu wengine kama fangasi na bakteria uwe rahisi. Kiwahi husababisha madoadoa yaliyokauka ( blotches ) katika majani ya mnyanya ambapo huwa anaishi. Lakini pia kiwavi anaweza kuishi nje ya majani na mashina mfano aridhini kwa muda. Maambukizi yakizidi jani hufa kabisa na mmea kunyauka.Pia huharibu mashina.


JINSI YA KUMZUIA
-Kilimo cha mzunguko ( crop rotation) kwa kutumia mazao yasiyo shambuliwa( mazao yasiyo jamii ya nyanya au viazi mviringo ). Mfano msimu huu ukilima nyanya/viazi msimu ujao unalima mahindi. Masalia ya wadudu hao yatakosa chakula na kufa kabisa maana hayana uwezo wa kula mahindi).
-Kuondoa mazao yote shambani kipindi cha kuvuna.
-Kuondoa na kuteketeza kabisa mimea iliyoathiriwa shambani
( Hizi njia zikitumiwa sehemu iliyo closed mfano greenhouse huwamaliza kabisa. Lakini sehemu iliyo wazi hizi njia huwapunguza kiasi cha kutosababisha hasara ( economic loss). Pia kama pembeni kuna mimea ya Solanaceae family itoe isije kuwa hifadhi.
Njia nyinginezo ni:Kulima vizuri, umwagiliaji mzuri na matumizi mazuri ya mbolea.


KUTUMIA KEMIKALI ( Insectides)
Japo zinatofautiana uwezo kemikali hizi ukizipa zaweda kuwa msaada mkubwa.
Cypermethrin, duduall-yenye mchanganyiko wa Cypermethrin na Profenofos au Chloropyrphos. Hizi ndizo zimeonekana kuwa na uwezo wa kuwaua.

Pia Deltamethrin na Pyrethroids zaweza kutumiwa japo uwezo wake umethibi
kuwa mdogo.

Nyinginezo ni Mwarubaini, spinosin,indoxacarb, methamidophos, abamectin, emamectin benzoate na cryomazin.

Pia unaweza kutumia mtego ( bait). Huwa na sex hormone iliyotengenezwa , harufu yake huvutia vidume. Vikija kwenye huo mtego hufa maana huwa na dawa. Hivyo unapunguza wingi wao na kasi ya kuzaliana.
 
Sambaza elimu Kwa wakulima huko kijijin mtaalum Wa udongo kutoka SUA
 
Mwaka jana wakati nyanya zangu zikiwa zinatoa maua, niliona vipepeo wadogo wa kijivu, baada ya wiki 2-3 nikaona nyanya zinashambuliwa na zimekwanguliwa majani yote. Napiga dawa wala hawaisikii
 
Hawa wadudu wanatabia ya kutengeneza usugu (resistance) kwa viuatilifu mno, unawezakupiga dawa mara ya kwanza ikafanikiwa kuwapunguza lakini ukapiga tena msimu huo huo ikashindwa kuwaua hapa sasa utashangaa kama hukua na taarifa ya tabia ya mdudu..kwasababu utakua ulishajiaminisha dawa flan ndio inafaa.
Unatakiwa kubadilisha kiutilifu unachopiga yaani usipige hiyo hiyo kila mara kwenye msimu mmoja au na misimu mingine ya ulimaji. Tumia kiuatilifu kingine chenye sifa ya kupambana na Tuta absoluta maana kufanya hivi itasaidia angalau kupunguza wingi wake na usugu.
 
Mwaka jana wakati nyanya zangu zikiwa zinatoa maua, niliona vipepeo wadogo wa kijivu, baada ya wiki 2-3 nikaona nyanya zinashambuliwa na zimekwanguliwa majani yote. Napiga dawa wala hawaisikii
Pole sana mkuu,kwahiyo mwishowe ilikuaje kiongozi?
 
Km tenga 22 ya nyanya iliharibiwa kwakutobolewa na wadudu hao, shamba ilioza kwa nyanya tulizotupa
 
Ukipata mojawapo kati ya hizi umemaliza

1.belt

2.wiltigo

Ziwe orijino,maana juzi nilikuwa kin'gori watu wanatumia feki nyingi ,maana wakulima hupenda vya bei chee
 
Tuta absoluta sio shida siku hizi ,sema wakulima na wataalamu baadhi hutumia wrong or counterfeit active ingredients
 
Kuna kitu nataka kujua kuhusu huyu mdudu kantangaze.. Je nikiwa niko katikati ya msitu sijazungukwa na mkulima mwingine yeyote yaan ful pori alafu hapo katikati ya pori ndio mm nalima heka zangu za nyanya je huyu mdudu anaweza nipata??
 
Kuna kitu nataka kujua kuhusu huyu mdudu kantangaze.. Je nikiwa niko katikati ya msitu sijazungukwa na mkulima mwingine yeyote yaan ful pori alafu hapo katikati ya pori ndio mm nalima heka zangu za nyanya je huyu mdudu anaweza nipata??
Swali zuri na fikirishi
 
TAASISI ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, mkoani Arusha imegundua mbinu mbadala ya kutokomeza mdudu ajulikanaye kama ‘kanitangaze’ ambaye ni jamii ya viwavijeshi, baada ya kemikali kushindwa kufanya kazi.

Mtafiti Never Mwambela amesema mdudu huyo ni tishio hivi sasa, kwa kutoboa nyanya na viazi mviringo.

Amesema wao walitafiti dawa ya vimelea vya asili kwa ajili ya kumdhibiti mdudu huyo, ambayo ni ya kimiminika na nyingine ya unga ambayo hunyunyizwa kwenye udongo pamoja na mazao shambani zikiwemo, nyanya, viazi, mahindi na mengineyo.

Amesema dawa hiyo imepata mafanikio makubwa wa wakulima walioitumia wa maeneo ya Ilula mkoani Iringa, Ngara na Nyuki mkoani Arusha, Babati mkoani Manyara na Kilosa mkoani Morogoro.

Amesema wao kama taasisi, dawa hiyo haijaanza kuuzwa ila wanasubiri vibali kutoka kwenye taasisi husika, na kwamba utafiti huo wameufanya kwa miaka mitatu.

Amesema Kanitangaze ni jamii ya viwavi jeshi ambaye ni mharibufu kwa mazao. Wakulima wamejitahidi kutumia kemikali mbalimbali bila mafanikio, na mwisho mdudu huyo anakuwa sugu wa dawa.

Amesema mdudu huyo aliingia nchini mwaka 2014 akitoka Amerika ya Kusini.
 
Mamayoyoo kwanza karibu sana JamiiForums.

Pili unapotaka kuanzisha mada angalia inahusu nini halaf ufungue jukwaa husika linalohisiana na mada yako.

Hii hukutakiwa kuiweka kwenye jukwaa la siasa my dear.

Karibu sana.
 
images.jpeg
Naomba kumuona huyo mdudu anaeitwa kanitangaze anafananaje?
images.jpeg
 
Back
Top Bottom