pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Hii ni kwa waafrika wote wafia dini za kuja kwa meli na manabii wa uongo, ambao hadi leo hii hawajatabiri jambo lolote la kweli kuhusu Afrika.
Mugo wa Kíbirú alikuwa nabii aliyeishi kabla na wakati mkoloni alipowasili Kenya. Nabii Mugo alitabiri ujio wa mkoloni Afrika Mashariki, miaka mingi kabla ya tukio lenyewe.
Utabiri wa Mugo wa Kíbirú ulikuwa hivi; Kwamba kutawasili watu wenye ngozi inayofanana na chura mweupe, 'kiengere' kwa kikikuyu.
Kwamba kwa kuwatazama tu watu watakuwa wanaona damu kwenye mishipa miilini mwao. Vyura hivyo vitakuwa vimevalia nguo zenye rangi nyingi, mithili ya vipepeo(kííuhuruta) na itakuwa upumbavu kuwashambulia kwa mikuki.
Kwasababu watakuja na vijiti vya ajabu(bunduki), ambavyo vitakuwa vinatoa moto(risasi).
Kisha akatabiri ujio wa reli na treni ya mkoloni. Akasema watakuja na joka kubwa la chuma, ambalo litakuwa linatembea kwenye barabara ya chuma. Likitema watu kila mara linaposimama, huku likiongozwa na kichwa kinachotoa moshi.
http://shujaastories.com/stories/mugo-wa-kibiru/