Mfahamu Mugo wa Kibiru au Chege(Cege) wa Kibiru, Nabii aliyetabiri ujio wa mzungu/mkoloni Afrika Mashariki

Mfahamu Mugo wa Kibiru au Chege(Cege) wa Kibiru, Nabii aliyetabiri ujio wa mzungu/mkoloni Afrika Mashariki

mkuu bila dini hao watawala wasingeweza kushawishi vita...achana na viongozi kuna watu binafsiwanajilipua,wanajiunga na makundi ya ugaidi kwasababu dini imekolea...kama ni kitu kizuri kwanini hiyo abrahamic religion ilivyoingia middle east isingeleta amani?it is always muslims vs Jews and Christians. kwahyo bila dini hayo yasingekuwepo.

Na kuhusu miaka 500 ijayo trust me dunia itakuwepo labda ungesema miaka millioni500 ijayo...umeangalia movie sana zimekuharibu.


Hivi kuna mtu aliyekudanganya kuwa Kabla ya ukoloni kuja Afrika watu walikua wanaishi kwa amani.

Achana na hiyo dhana ya wanasiasa ya kudanganya kuwa Tulikua wamoja kabla ya ukoloni.
Kwa taarifa yako Mkoloni ndiye aliyetuunganisha .
Tanganyika ina makabila 128 makubwa yenye l
Lugha tofauti . Na koo nyingi sana . Kabla ya Mkoloni Kila Kabila lilikua ni kama nchi na utawala wake yaani kila kabila lilikua na Chifu wake. Hata dini zilikua hazifanani. Ubaguzi ulikua ni mkubwa sana. Mkoloni alipokuja ndiye aliyeweka mipaka ya kuwatambua watu wa makabila 128 kuwa ni Taifa moja na wanafuata sheria za nchi moja chini ya kiongozi mmoja, mahakama na Jeshi moja.

Vita zilikua ni za kunyanganyana mifugo na ardhi na kugombania madaraka. Kwa hiyo vita haijanzishwa na dini bali zilikuwepo kila mahali.

Amani haiwezi kuja kwa watu wasioheshimu Uhuru wa wengine. Kwa muda mrefu ya Ibrahimu imekua ikipigwa vita na mataifa mengine. Kwa hiyo wanajihami kama yalivgo kalundi mengine yanavyojiham wanapoonewa.
Watu wanaoitwa watani kwa makabila ni watu waliowahi kupigana sana vita kwa karne nyingi kabla ya mkoloni kuja. Mkoloni alipokuja ikawekwa swa sheria ya kuzuia vikundi vya makabila kuwa na majeshi.Ukawa mwanzo wa kuisha kwa vita za kikabila.


Kifupi kila jambo lina wakati wake na makusudi yake ili dunia itoke kwenye hatua moja kwenda nyingine katika maendeleo.
 
Hii ni kwa waafrika wote wafia dini za kuja kwa meli na manabii wa uongo, ambao hadi leo hii hawajatabiri jambo lolote la kweli kuhusu Afrika.

Mugo wa Kíbirú alikuwa nabii aliyeishi kabla na wakati mkoloni alipowasili Kenya. Nabii Mugo alitabiri ujio wa mkoloni Afrika Mashariki, miaka mingi kabla ya tukio lenyewe.

Utabiri wa Mugo wa Kíbirú ulikuwa hivi; Kwamba kutawasili watu wenye ngozi inayofanana na chura mweupe, 'kiengere' kwa kikikuyu.

Kwamba kwa kuwatazama tu watu watakuwa wanaona damu kwenye mishipa miilini mwao. Vyura hivyo vitakuwa vimevalia nguo zenye rangi nyingi, mithili ya vipepeo(kííuhuruta) na itakuwa upumbavu kuwashambulia kwa mikuki.

Kwasababu watakuja na vijiti vya ajabu(bunduki), ambavyo vitakuwa vinatoa moto(risasi).

Kisha akatabiri ujio wa reli na treni ya mkoloni. Akasema watakuja na joka kubwa la chuma, ambalo litakuwa linatembea kwenye barabara ya chuma. Likitema watu kila mara linaposimama, huku likiongozwa na kichwa kinachotoa moshi.

http://shujaastories.com/stories/mugo-wa-kibiru/
Ukimaliza kumwelezea huyu pia utuletee utabiri wa nabii wa mwisho huko Kenya aliyeitwa "Jehovah Nyonyi"
 
Ukimaliza kumwelezea huyu pia utuletee utabiri wa nabii wa mwisho huko Kenya aliyeitwa "Jehovah Nyonyi"
Jehovah Wanyonyi alikuwa tapeli mwenzenu, mtafuna sadaka pamoja na kitoweo cha kondoo. Hakuwa na tofauti yeyote na yule mwanachama mwenzenu askofu. Sijui huwa mnamwitaje, Gwajima?
 
Back
Top Bottom