Mfahamu mwana dada aliyedondoka umbali mrefu toka kwenye ndege bila parachuti na kupona

Mfahamu mwana dada aliyedondoka umbali mrefu toka kwenye ndege bila parachuti na kupona

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Mpaka leo hakuna rekodi wala kutokea kwa binadamu kutoka kwenye ndege na kuanguka ardhini na kupona.

Historia hii ina muangukia mwadada Vesna Vulović.mpaka kumuingiza kwenye kitabu cha maajabu ya dunia.

Mnamo tarehe 26 Januari 1972, Vesna Vulović alikuwa mhudumu wa ndege kwenye ndege ya JAT Yugoslav Airlines Flight 367. Safari zilizofanyika kati ya Stockholm nchini Uswidi na Belgrade nchini Serbia.

Ndege hiyo ilipokuwa juu maeneo ya Czechoslovakia - sasa Jamhuri ya Czech - na hapo ndipo ndege ililipuka vipande vitatu. Mlipuko na ajali hiyo iliua kila mtu kwenye bodi. Kila mtu isipokuwa Vesna, ambaye alinusurika kuanguka toka kwenye ndege umbali uliopo juu wa futi 33,333 (mita 10,160; maili 6.31).

Naweza kusima ni miujiza
images%20(13).jpg
images%20(14).jpg
images%20(15).jpg
 
Mwenye kushikiria rekodi anayemfata ni bwana Ivan Chisov.

Chisov alikuwa Luteni wa Jeshi la Wanahewa la Soviet ambaye alianguka futi 22,000 wakati mshambuliaji wake wa Ilyushin II-4 alipopigwa na wapiganaji wa Ujerumani. Huku vita vikiendelea kupamba moto karibu na mshambuliaji wake aliyekuwa akishuka kwa kasi, aliamua kutofungua parashuti yake mara moja - badala yake akasubiri hadi aanguke chini ya macho ya Wajerumani. Kwa bahati mbaya alipoteza fahamu mara tu baada ya kuruka na hakuweza kuvuta kamba ya mpasuko. Chisov alinusurika kimiujiza.

Akianguka kati ya 120 na 150 mph, aligonga ukingo wa bonde lenye theluji na kubingiria chini hadi chini. Alivunjika mguu, fupanyonga, na baadhi ya majeraha ya uti wa mgongo lakini hatimaye aliweza kupona kabisa. Miezi mitatu tu baadaye alikuwa akiruka tena.
chisov.jpg
 
Hivi futi 30000 unazijua?ukitandaza ni km kumi,kutoka posta mpaka ubungo
Hii ni chai ya wazungu
Sasa umeshaelezwa ulitaka nini ? Kutizama.sio kila jambo dunia ulifahamu ndio maana ukuwa mganga wa kienyeji wala mchungaji au mwanasayansi.
Mengine yanaitwa maajabu. Ushawai kuwa na urefu kama wa hashimu
 
Narudia tena,wazungu wametudanganya vingi sana,usiwaamini kivile,rekodi zote za dunia wanataka ziwe zao.
 
Kashindane na wanaothibitisha wamesoma na kufundisha wanazuoni kuwa wewe ni mjuaji kuliko wao.View attachment 2527630
Narudia wazungu wana chai sana usiwaamini sana.
Kuna mtu anaitwa cassanova mgoogle alitembea na wanawake 132 maishani mwake ila wamemuweka kwenye rekodi za womanizer,wakati mimi na umri huu nimeshafikisha 300+ na sijulikani .wazungu wana chai sanq
 
Narudia tena,wazungu wametudanganya vingi sana,usiwaamini kivile,rekodi zote za dunia wanataka ziwe zao.
Eti wametudanganya ulivokuwa mjinga.kwa hiyo hizi app,kompyuta,kutibiwa,umeme na magari unatumia ukiwa unadanganywa
 
Narudia wazungu wana chai sana usiwaamini sana.
Kuna mtu anaitwa cassanova mgoogle alitembea na wanawake 132 maishani mwake ila wamemuweka kwenye rekodi za womanizer,wakati mimi na umri huu nimeshafikisha 300+ na sijulikani .wazungu wana chai sanq
Una hoja unajiabisha tu
 
Hujafika 300+ emu nipasie hio tangawizi hapo,
 
Eti wametudanganya ulivokuwa mjinga.kwa hiyo hizi app,kompyuta,kutibiwa,umeme na magari unatumia ukiwa unadanganywa
Siongelei technology naongelea hivi vistory vya rekodi,wanajipendelea sana ,si ajabu mnaamini ziwa victoria na mlima kilimanjaro waligundua wao
 
Back
Top Bottom