Mfahamu Saida Karoli, Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili

Mfahamu Saida Karoli, Mwanamuziki mkongwe wa nyimbo za asili

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
43
Reaction score
61
Saida Karoli Amezaliwa mkoani Kagera tarehe 4 Aprili 1976 ni mwanamuziki wa nyimbo za asili ya Kihaya Saida alipata elimu ya msingi mwisho darasa la tano tu, ambapo ilibidi aache shule kutokana na kukosa msaada kutoka kwa baba yake ambaye hakuwa anaitazama sana elimu ya mtoto wake, hivyo hakuweza kuendelezwa

Saida alikulia katika kijiji cha Rwongwe mkoani Kagera na kutokana na mila za ukoo wake wasichana walikuwa hawaruhusiwi kushiriki katika shughuli za kimuziki. Hata hivyo kwa vile mama yake alikuwa na kipaji cha muziki alimpa moyo na kumfundisha masuala mbalimbali ya kimuziki

Akiwa na miaka 20 mama yake mzazi alifariki dunia lakini Saida aliendelea kujijengea kipaji chake cha uimbaji na upigaji ngoma

Kukua kwake kimuziki Kipaji cha usanii wa muziki kwa Saida kilijitokeza ghafla baada ya kujikuta akichukuliwa na kudhaminiwa na FM Productions Ltd waliokuwa mkoani Kagera wakitafuta wasanii wenye vipaji kwa ajili ya kuwaendeleza

FM ilimchukua Karoli wiki tatu tu kurekodi nyimbo yake ya kwanza ilotoka na kuishitua Dar es Salaam mzima pamoja na nchi za jirani za Afrika Mashariki

Albamu yake ya kwanza ilizinduliwa tarehe 2 Septemba mwaka 2001 .
Albamu hiyo ilipata mafanikio makubwa na kupata umaarufu mkubwa sana kwakuwa albamu hiyo ilikuwa na vionjo vingi vya kabila la Kihaya

Albamu hiyo ilijulikana kama Maria Salome. Japokuwa mashabiki wake waliibatiza jina la Chambua kama Karanga kutokana na maneno aliokuwa anaimba katika nyimbo ya Maria Salome nyimbo iliobeba jina la Albamu

Albamu hiyo ilifuatiwa na ziara kubwa alizokuwa anafanya katika nchi za jirani kama vile Burundi , Rwanda,Uganda na Kenya ambapo alipata mafanikio makubwa na Saida kujikuta akibatizwa na kupewa jina la malkia wa nyimbo za asili

Kutokana na uwezo alionao na kipaji katika masuala ya muziki ni rahisi kugundua kuwa
mwanamuziki huyo ana kiwango cha kuweza kupata mashabiki wa muziki wake mbali na
Tanzania na Afrika ya Mashariki.

Facian Muta promota na meneja maarufu miaka ya 2000 Huyu ndie mmiliki halali wa Album na Nyimbo za Saida Karoli. Yeye ndie alimleta mjini Saida na kumsaini (FM Studios) Producer Mikka Mwamba. Nyimbo zake zilibamba si Tanzania pekee bali Africa Mashariki na Africa nzima .

( PICHA YA KWANZA NI FACIAN MUTA PROMOTA WA SAIDA KAROLI)
( PICHA YA PILI NI PRODUCER MIKKA MWAMBA)

List ya Album za Saida karoli.

1. Chambua kama Karanga (Maria Salome) (2001)
2. Mapenzi kizunguzungu (2003)
3. Harusi (2004)
4. Mimi Nakupenda (2005)
5. Nelly (2008)
6. Akatambala Ft. Baliruno K. Hanson (2018)

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
1771349888383.jpg
1771349883408.jpg
1771349875028.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Saida karoli na Rose muhando hawa ndo wasanii bora wa muda wote ila unfortunately walikutana na WEZI wasiothamini jasho lao.
 
Back
Top Bottom