Charles Mandela
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 2,752
- 2,282
Kuwa mwanafunzi bora kitaifa sio jambo dogo hata kidogo na sio kitu chepesi, kinahitaji maandalizi ya kujitoa kama mwanafunzi ili kufikia adhma hiyo.Sasa mkuu kutangazwaa Kuwa T.O sio kwamba Itaandikwa kwenye Cheti chako mzeee[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Zaidi zaidi utapewa certificate inayokutambulisha kuwa ulikuwa Best if kipo au inawezekana hakuna kabisaaa hicho cheti just Wanatangaza tu na kuweka kwenye kumbukumbu zao huko Necta. Lipumba alikuwa T.O kwa Comb ya EGM kitu ambacho hakijawahi tokea sasa just imagine toka enzi lipumba anasoma mpaka leo hii historia ipo means system ilianza zamani ila sio kama unavyodhani wewe kuwa lazima upewe cheti sijui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Na nikupe siri nyingine ambayo watu wengi hawafahamu, kwa kila mtihani wa taifa kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa kuna orodha ya matokeo ya wanafunzi kuanzia wakwanza mpaka wamwisho kitaifa.
Lakini matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanauzito kwa sababu yanakuwa ni ngazi ya kwenda hatua nyingine.
Na serikali huwa inaamua kutangaza wanafunzi kumi [10 bora] waliofanya vizuri kitaifa tu lakini ilikuwa na uwezo wa kutangaza hata [20 bora] au hata [50 bora] kama ikitaka, kwa sababu orodha ya watahiniwa wote ipo - wakwanza mpaka wamwisho.
Sasa kwa miaka ya nyuma, serikali ilikuwa haitoi hizi orodha kama inavyotoka wakati huu. Ndio maana kulikuwa na ulaghai na udanganyifu wa kutisha kwenye kuwasilisha matokeo kwa nakala ya vyeti.
Kwa kesi ya Elias Kihombo, hakuongoza yeye na hauwezi kusema ana wastani wa 98 kwa sababu hiyo orodha haipo na haikutangazwa hadharani. Na mimi siwezi kuitoa hadharani kwa sababu hizo orodha huwa ni nyaraka za serikali, zisipotangazwa zinabaki kuwa ni siri za serikali.
Inabidi yeye mwenyewe Elias Kihombo atuambie au wale wanaosema aliongoza kidato cha sita watuoneshe hiyo orodha na sio tofauti na hapo.