Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Kuwa mwanafunzi bora kitaifa sio jambo dogo hata kidogo na sio kitu chepesi, kinahitaji maandalizi ya kujitoa kama mwanafunzi ili kufikia adhma hiyo.

Na nikupe siri nyingine ambayo watu wengi hawafahamu, kwa kila mtihani wa taifa kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa kuna orodha ya matokeo ya wanafunzi kuanzia wakwanza mpaka wamwisho kitaifa.

Lakini matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanauzito kwa sababu yanakuwa ni ngazi ya kwenda hatua nyingine.

Na serikali huwa inaamua kutangaza wanafunzi kumi [10 bora] waliofanya vizuri kitaifa tu lakini ilikuwa na uwezo wa kutangaza hata [20 bora] au hata [50 bora] kama ikitaka, kwa sababu orodha ya watahiniwa wote ipo - wakwanza mpaka wamwisho.

Sasa kwa miaka ya nyuma, serikali ilikuwa haitoi hizi orodha kama inavyotoka wakati huu. Ndio maana kulikuwa na ulaghai na udanganyifu wa kutisha kwenye kuwasilisha matokeo kwa nakala ya vyeti.

Kwa kesi ya Elias Kihombo, hakuongoza yeye na hauwezi kusema ana wastani wa 98 kwa sababu hiyo orodha haipo na haikutangazwa hadharani. Na mimi siwezi kuitoa hadharani kwa sababu hizo orodha huwa ni nyaraka za serikali, zisipotangazwa zinabaki kuwa ni siri za serikali.

Inabidi yeye mwenyewe Elias Kihombo atuambie au wale wanaosema aliongoza kidato cha sita watuoneshe hiyo orodha na sio tofauti na hapo.
 
Je kama alipewa alama zake, kisha akatafuta Wastani wa alama hizo na kupa Wastani wa 98. Huo Wastani unakuwa siyo mpaka utangaziwe ?

Au yeye anaposema amepata wastani wa 98,huwa anasema ameambiwa hivyo baraza ?
Hakuna kitu kama hicho!
 
Kwa nini hakusomea ualimu sasa?
 
Hata mimi sijawahi kusikia huo upuuzi anaosema.
Na nilishawahi kufanya kazi nje ya nchi ila sijawahi kuulizwa hayo makolokolo anayotaja hapa sasa sijui huko nje ni wapi alipodaiwa hivyo vitu.
 
Hata mimi sijawahi kusikia huo upuuzi anaosema.
Na nilishawahi kufanya kazi nje ya nchi ila sijawahi kuulizwa hayo makolokolo anayotaja hapa sasa sijui huko nje ni wapi alipodaiwa hivyo vitu.
Fala tu mmoja hafu yupi active kweli na huu uzi atakuja muda si mrefu hapa.
 
Tuwekee ushahidi wa haya uliyo yaandika. Kisha utuambie ulijuaje kama wewe umeongoza ?
 

Kushindwa kuandika sentensi kwa usahihi ndiyo kigezo cha mtu kushindwa kufaulu ?

Mlitakiwa nfundishwe Elimu ni nini kwanza kabla ya kuzisoma.
 
Fungua hizo screen shots utapata list Ya wanafunzi waliofanya vizuri kidato cha nne mwaka 2005
 
Ni maigizo hakika! Hivi kwani hata wewe ulishawahi kuiona hiyo orodha ya wanafunzi bora inayoonyesha Elias Kihombo aliongoza kidato cha sita mwaka 2006? Kama ipo mnakwama wapi na sisi wengine tuione?
Nenda necta mkuu

Acha ubishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…