MA_mandela
KU_ kubwa jinga
Sijui tunachobishana ni nini, kwa sababu kila kitu kipo wazi! Tatizo sio wahitimu, tatizo ni NECTA.
Maana taarifa za NECTA zingekuwa wazi kusingekuwa na haya malumbano.
Wahitimu wanapata shida sana kwenye vetting kwa sababu matokeo yaliyopo kwenye cheti yanakuwa ni tofauti na matokeo yanayosoma kwenye TSM9.
Ifahamike kuwa mbali na TSM9, huwa kuna kitabu cha wahitimu ambacho kinaonesha mwanafunzi wa kwanza mpaka wa mwisho kitaifa.
Kitabu hiki huwa kinatoka kila mwaka kwa madarasa husika - yaani darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita.
Huwa pia kuna kitabu cha wahitimu wa darasa la nne na kidato cha pili, sema hivi vitabu huwa vinaorodha ya wanafunzi waliofanya mitihani na matokeo yao kupangwa kimikoa tu.
Na hivi vitabu huwa havipatikani Baraza la Mitihani [ NECTA ] pekee yake, bali huwa vinapatikana pia Wizara ya TAMISEMI kwa sababu elimu ya msingi huwa ipo chini ya hii wizara, Wizara ya ELIMU, Wizara ya MUUNGANO na ofisi ya RAIS yaani IKULU.
Kwahiyo sio kitu cha kubeza, ifahamike kuwa matokeo halisi ndio yamebeba uhai wa wahitimu na ikitokea matokeo halisi yapo tofauti na matokeo ya kwenye cheti ndio haya matatizo yanayotokea wahitimu wengi kukosa ajira ingali ajira zipo!
Kwahiyo tatizo sio wahitimu, tatizo ni NECTA kwa sababu ukiingia kwenye sekta ya ajira, muajiri hawezi kuaminika na matokeo ya kwenye karatasi tu lazima uhakiki uwepo ili kuhakikisha yale yaliyomo kwenye cheti ndio matokeo halisi?
Ikitokea ni tofauti, kwa lugha ya kitaaluma wasema vetting disclosure yaani hamna kitu hapo. Sasa hapa tatizo sio wahitimu, tatizo ni NECTA.
Na huko tunapoenda, upishi wa matokeo ukiendelea hivi, ajira nyingi za Watanzania zitachukuliwa na wageni hasa kutoka KENYA na UGANDA.
Sasa hii tabia ya NECTA inabidi ikemewe vikali kwa masilahi ya wahitimu kwanza na taifa kwa ujumla maana tunapata wahitimu wabovu kwa sababu ya rushwa!. Na kuacha wale waliokuwa wanafaa kihalali tangu shule ya msingi mpaka kidato cha sita.
Chuo Kikuu huwa hatutazamii sana kwa sababu kila chuo huwa kina silabasi zake na kila chuo kina GPA zake. Kwahiyo nauwezo wa kuchukua LOWER SECOND ya UDOM au MZUMBE nikaacha FIRST CLASS ya TUMAINI au SAUT.
Turudi kwenye mada husika sasa! Matokeo ya wanafunzi bora ni muhimu sana hata kwa miaka ya nyuma kwa sababu na wao pia wapo kwenye soko la ajira.
Ni hayo tu kwa leo!