Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Mfahamu T.O Kihombo 2006 aliyepata Degree yake ya Kwanza baada ya Miaka 11

Hata kuandika sentensi ya kiingereza inakushinda! Ilikuaje ukapata shahada yako?

Ndio haya tunayosema, elimu ya Tanzania ilikuwa ni soko huria.

Pesa ilikuwa inamaliza kila kitu, na sio uwezo wa mwanafunzi husika. Ndio maana hata kimataifa watanzania hawapo!

Nchi jirani za Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Msumbiji na hata Malawi zimetupita mbali sana kielimu.
Kwani Elimu ni nini kaka mkubwa ? Kujua kuandika Kiingereza ndiyo unakuwa mjinga au hujaelewa au inakuwaje ? Na nani anapaswa ajue Kiingereza katika nchi kama yetu ?
 
Hmm! Mimi binafsi namfahamu kwa sababu alinifundisha masomo ya dhiada [ tuition ] ya Physics na Mathematics mwaka 2009.

Kusema ukweli, Elias Kihombo yuko vizuri kwenye kufundisha masomo ya Physics na Mathematics.

Lakini hii isiwe sababu ya yeye kujitangaza kuwa aliongoza kidato cha sita mwaka 2006 na kupata wastani wa 98!

Hivi kwani siku hizi baraza la mitihani [ NECTA ] wanatoa hadi wastani? Jibu ni hakuna!

Sasa kama hiyo orodha ipo ya yeye kuongoza kidato cha sita tunaomba tuione! Jibu ni haipo!
Je kama alipewa alama zake, kisha akatafuta Wastani wa alama hizo na kupa Wastani wa 98. Huo Wastani unakuwa siyo mpaka utangaziwe ?

Au yeye anaposema amepata wastani wa 98,huwa anasema ameambiwa hivyo baraza ?
 
TSM9 ni taarifa za kitaaluma za mwanafunzi husika, tangu chekechea mpaka chuo kikuu.

Chochote utakachokifanya kwenye maendeleo ya kitaaluma kinaorodheshwa kwenye hii fomu.

Hata zile barau za utovu wa nidhamu ambapo mwanafunzi huandika kipindi ambapo yupo shule au chuo kikuu zinaorodheshwa kwenye faili lako.

Kwa hiyo matokeo halisi ya wanafunzi husika yapo kwenye faili la kitaaluma, popote pale litakufuata.
Kuwa makini!

Hmm! Hivi unaona jinsi matokeo ya wanafunzi bora yanavyotangazwa sasa hivi?

Leta matokeo ya wanafunzi bora ya kidato cha sita ya mwaka wa 2006 ampabo Elias Kihombo ameongoza [emoji23][emoji23]
Sasa mkuu kutangazwaa Kuwa T.O sio kwamba Itaandikwa kwenye Cheti chako mzeee[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Zaidi zaidi utapewa certificate inayokutambulisha kuwa ulikuwa Best if kipo au inawezekana hakuna kabisaaa hicho cheti just Wanatangaza tu na kuweka kwenye kumbukumbu zao huko Necta. Lipumba alikuwa T.O kwa Comb ya EGM kitu ambacho hakijawahi tokea sasa just imagine toka enzi lipumba anasoma mpaka leo hii historia ipo means system ilianza zamani ila sio kama unavyodhani wewe kuwa lazima upewe cheti sijui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hivi yule jamaa anayeongoza kwa kusolve millenium problems anaitwa nan nmemsahau
Yametatuliwa na wanataaluma mbalimbali. Ila alifanya jambo la ajabu ni huyu aliyesolve Poincare conjecture ). Mrusi ( Grigor Perelman) aliyekataa dola milioni moja kama zawadi ya kazi yake problem. Halafu hii njemba inaishi kwao kwa mama ake. Hawa jamaa wenye akilinyingi sijui wakoje.
 
Wee jamaa TSM9 na kutangazwa kwa TO vinahusianaje????[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani unatumiq nguvu kubwa kubisha alafu badala ya kubisha unasupport wanachosema wengine. Kutangazwa T.O tanzania imeanza kitambo sanaa yani sanaa sasa wewe unasema 2016 sijui umeitoa wapi??
Huyu jamaa naona kaamua kujimwambafy anatuchafulia Uzi[emoji44]
 
Imepita miaka takribani 12 sasa, tangia Tanzania ilipapata kumshuhudia mwanafunzi aliyeshindikana katika maswala ya Elimu hapa namzungumzia,Tanzania One (2006) Elias Kihombo katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2006 akitokea shule ya sekondari Tosamaganga wengi wanapenda kuiita Tosa Boy's

Mwaka 2006, Necta ilimtangaza mwanafunzi Elias Kihombo kutoka Tosamaganga Secondary School kuwa ndo kipanga wa mwaka huo akiwapita wanafunzi wenye akili zaidi waliovuma toka shule kongwe na special schools kama kibaha, ilboru, mzumbe, kilakala, Tabora boys etc ukweli ni kwamba Elias Kihombo hakuwa maarufu kwa kipindi hiko na wengi walisikia tu story zake haswa kwa wanafunzi wa Mzumbe Boys ambao Mara nyingi walipata kumuona katika mazingira yao.

Kumbuka kwamba Elias Kihombo hakupewa Priority kubwa sana ya kuwa T.O wa Advance Level kutokana pia na matokeo yake ya Kidato cha Nne (4) kuonekana kuwa ya kawaida sana, Kihombo alifanikiwa kupata Division One (1.14) akiwa na Physics-A Chemisrty-A Biology na Mathematics-B, Ndipo mwaka huo 2003 alipata kuchaguliwa Tanga Technical school iliyopo mkoa wa Tanga (tetesi), lakini baadae aliamua kurudi tena katika shule yake ya zamani yaani Tosamaganga secondary kuendelea na masomo yake ya Advance level. Alimaliza hapo hapo akifanikiwa kuwa mwanafunzi wa kwanza toka Tosamaganga kwa Advance Level kuwa mwanafunzi bora kitaifa, Alifanikiwa kupata maksi za juu sana na kupata Division One (1.3)
Physics-A
Chemistry-A
Advanced Mathematics-A

October 2006 Alichaguliwa kujiunga na University of Dar Es Salaam (UDSM) akiwa kama T.O kusoma Bachelor of Science In Telecommunication Engineering (4years) na tetesi zinasema alifanikiwa kupata ufadhili wa masomo yake chini ya kampuni ya Airtel.
Siku zilienda na alikuwa karibu kumaliza Elimu yake ya chuo kikuu, huku akipata madili mengi ya kufundisha Tuition maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam na shule nyingi za sekondari ndani ya Tanzania hasa shule za Advance.

Lakini baada ya Miaka 4 kupita ikiwa miezi michache tu imebaki ya kumaliza chuo Tanzania One Kihombo alidisco chuo na hivyo kumfanya asifanikiwe kupata degree yake ya kwanza mwaka huo 2010, lakini wengi wanasema hakupaswa kudisco chuo lakini ndivyo ambavyo Hatima yake ilipoishia hapo. (tetesi [emoji6] [emoji6]).

Moja kati ya maneno ambayo wengi wanamnukuu aliyopata kuyasema ndani ya Miaka hiyo, alisema "Duniani walionipita kwa akili ni watu wawili tuu wa kwanza Mola, wa pili ni Mzungu" hapa ndipo hatima yake inavyosemekana ikafungwa na wakuu wake lakini wengine wanasema vingine.

Elias hakutaka kwenda chuo chochote kile na ndani ya Miaka hiyo mitatu baada ya kudisco chuo, yaani 2011,2012 na 2013 alikuwa anazunguka shule mbalimbali za sekondari Tanzania kupiga mapindi ya Physics na Chemistry na kwelii huyu jamaa alikuwa ni Invisible katika masomo hayo mawili, Japo Pure Mathematics alikuwa hafundishi kabisa kwasababu alikuwa anasema "Siwezi kufundisha Somo rahisi duniani kama Pure Mathematics, Mimi nafundisha Physics na Chemistry tu"

Ndipo baada ya Miaka mitatu kupita (3) T.O aliyetukuka zaidi katika vinywa vingi vya wanafunzi wa Tanzania, kutokana na ufundishaji wake na kuwaita wanafunzi wake nyumbu na kuwa na jeuri zaidi ya akili zaidi ya watu wengine, alifanikiwa kurudi tena ndani ya University of Dar Es Salaam safari hii akiwa ameamua na amedhamiria kuchagua kozi nyingine Mpya kabisa iliyoanzishwa mwaka huo 2013 hapohapo Udsm iliyoitwa (Bachelor of Science In Petroleum Engineering). Hii kozi ilikuwa inachukua wanafunzi 20 pekee Tanzania nzima tena wale waliosoma PCM tu (Physics, Chemistry na Advanced Mathematics) na waliopata Marks za juu kabisaa.

Baada ya Miaka 4 kupita, ndipo July 2017, T.O Elias Kihombo alifanikiwa kumaliza Degree yake ya kwanza (Bachelor of Science In Petroleum Engineering) na mnamo November 2017 Elias Kihombo alifanikiwa kutunukiwa Degree yake ya kwanza akiwa ndani ya University of Dar Es salaam baada ya Miaka 11 kupita.

Hapa imepita Miaka mingi tangia, 2006 Engineer Elias Kihombo alivyotangazwa kuwa Tanzania One lakini ilimchukua Miaka mingine 11 mpaka kutunukiwa Degree yake ya kwanza. Huyu ndiye The Best Of The Best, Eng Elias Kihombo Mwanafunzi aliyepata kutokea Tanzania na kuwaonesha wengine uwezo wake katika nyanja nzima ya Elimu.

Wapo wengi wanaojiuliza Eng Elias Kihombo yupo wapi kwa sasa, Lakini mpaka sasa Kihombo yupo chini ya Himaya ya Mkoa wa Geita Nyumbani kwa Mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuri, huku akiendeleza harakati zake na akiwa na vitabu vyake vingi alivyoviandika kuwasaidia vijana wa Tanzania ikiwa pamoja na Physics Books na Chemistry Books.


Written by Eng EVANS RICHARD.

*We Always Live To Fight Another Day*




View attachment 818214View attachment 818215View attachment 818222
Dah kweli akil tu haikufany ufanikiwe nidhsm pia ni mhm
 
Anakwamaa sanaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
ndio maana social network nyingine unapotaka kujiunga Kuna short survey ya kugundua Kama wewe unaetaka kujiunga ni binadamu au ni robot kuepuka outomatic reply ambayo itakupotezea muda au kukuletea shida nyingine ata kukupelekea kutapeliwa, maana huyu jamaa anaubishi Si wa kibinadamu.
JF mfike uko Sasa maana Kuna viumbe waajabu washaanza kuvamia huu mtandao.
 
Sema wewe Ndo unajua alikuwa T. O maana wewe ndio umeyasema hapa hakuna mwingine aliyesema hao watu unaowasingizia kuwa wanajua alikuwa T. O Ni wewe na watu wa aina yako
By the way msalimie Mzee Kisandu hapo Rock City
Naam! Sasa watu wengi wanafahamu kuwa huyu mwanafunzi nayeye aliongoza, kumbe hamna kitu kama hicho! Hopeless kabisa!
 
Invisible = unseen (esp. By naked eyes)
Invincible = undefeated

Sijui kwanini tusiwe tunaandika kwa Kiswahili tu
 
Sema wewe Ndo unajua alikuwa T. O maana wewe ndio umeyasema hapa hakuna mwingine aliyesema hao watu unaowasingizia kuwa wanajua alikuwa T. O Ni wewe na watu wa aina yako
By the way msalimie Mzee Kisandu hapo Rock City
Mimi sipo Mwanza na hata Mzee Kisandu simfahamu!
 
Hahahah unachekesha wewe [emoji2][emoji2][emoji1787] [emoji1787][emoji1787]
Ni maigizo hakika! Hivi kwani hata wewe ulishawahi kuiona hiyo orodha ya wanafunzi bora inayoonyesha Elias Kihombo aliongoza kidato cha sita mwaka 2006? Kama ipo mnakwama wapi na sisi wengine tuione?
 
Back
Top Bottom