Kuwa mwanafunzi bora kitaifa sio jambo dogo hata kidogo na sio kitu chepesi, kinahitaji maandalizi ya kujitoa kama mwanafunzi ili kufikia adhma hiyo.
Na nikupe siri nyingine ambayo watu wengi hawafahamu, kwa kila mtihani wa taifa kuanzia darasa la nne, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha nne na kidato cha sita huwa kuna orodha ya matokeo ya wanafunzi kuanzia wakwanza mpaka wamwisho kitaifa.
Lakini matokeo ya darasa la saba, kidato cha nne na kidato cha sita huwa yanauzito kwa sababu yanakuwa ni ngazi ya kwenda hatua nyingine.
Na serikali huwa inaamua kutangaza wanafunzi kumi [10 bora] waliofanya vizuri kitaifa tu lakini ilikuwa na uwezo wa kutangaza hata [20 bora] au hata [50 bora] kama ikitaka, kwa sababu orodha ya watahiniwa wote ipo - wakwanza mpaka wamwisho.
Sasa kwa miaka ya nyuma, serikali ilikuwa haitoi hizi orodha kama inavyotoka wakati huu. Ndio maana kulikuwa na ulaghai na udanganyifu wa kutisha kwenye kuwasilisha matokeo kwa nakala ya vyeti.
Kwa kesi ya Elias Kihombo, hakuongoza yeye na hauwezi kusema ana wastani wa 98 kwa sababu hiyo orodha haipo na haikutangazwa hadharani. Na mimi siwezi kuitoa hadharani kwa sababu hizo orodha huwa ni nyaraka za serikali, zisipotangazwa zinabaki kuwa ni siri za serikali.
Inabidi yeye mwenyewe Elias Kihombo atuambie au wale wanaosema aliongoza kidato cha sita watuoneshe hiyo orodha na sio tofauti na hapo.