Mfahamu Wilfred Mwabulambo, aliyecharazwa bakora na Mwl. Julius K Nyerere

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU WILFRED MWABULAMBO ALICHARAZWA VIBOKO KWA KUMGOMEA RAIS NYERERE!

Wanafunzi wanapogoma au kufanya maandamano, dola hujibu mapigo kwa njia anuai. Ipo mifano ya wanafunzi waliosimamisha au kufukuzwa chuo, kuswekwa korokoroni na kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kujihusisha kwao na maandamano yasiyo na kibali cha dola.

Ni vigumu mtu kuamini kwamba kati ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kuwadhibiti wanafunzi wa chuo kikuu wanaoonekana kuwa watukutu ni kuwaadabisha kwa bakora! Amini usiamini, hapa nchini imewahi kufika pahala serikali, tena chini ya Mwalimu Nyerere kuwatandika viboko wanafunzi waliokosa utiifu kwa viongozi wa serikali.

Mfano wa hili ni kwenye mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam dhidi ya tamko la uhuru wa walowezi wa Zimbabwe (Unilateral Declaration of Independence-UDI) la mwaka 1965 chini ya Ian Smith.

Ikumbukwe kuwa baada ya Ian Smith na genge lake la walowezi kujitangazia uhuru na kutwaa mamlaka ya kuiongoza Rhodesia ya Kusini (Sasa Zimbabwe), Umoja wa Afrika uliitisha kikao cha dharura , ambapo viongozi wa nchi za Kiafrika waliafikiana kwa kauli moja kuipa shinikizo Uingereza (Waliokuwa wakoloni wa Rhodesia ya Kusini kabla ya kuwaachia walowezi) kubatilisha utawala wa Smith na kuukabidhi uhuru kwa wazalendo.

Azimio la Umoja wa Nchi Huru za Afrika liliweka bayana kwamba kama Uingereza haikutekeleza matakwa hayo ifikapo 15 Disemba 1965 basi nchi zote za Kiafrika zingefuta mahusiano ya kidiplomasia na nchi hiyo.

Uingereza ilipochelea kutekeleza azimio la OAU, Tanzania ilikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa za Kiafrika kufanya uamuzi mzito wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Uingereza. Kwenye hotuba yake Bungeni kuhusu suala hili, Mwalimu Nyerere aliweka wazi msimamo wa Tanzania. “Sera za Tanzania na Afrika kuhusiana na suala la Rhodesia ya Kusini mara zote zimekuwa na zitaendelea kuwa na lengo moja tu. Lengo hilo lilikuwa na litaendelea kuwa kupatikana kwa uhuru wa wengi. Kuhusu hili, kila hatua tuliyochukua na kila hotuba tuliyotoa vimelenga kulifanikisha lengo hilo. Hatuna zaidi ya hilo” alisema Mwalimu.

Kwa upande wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kama yalivyofanya makundi mbalimbali barani Afrika, wao waliamua kufanya maandamano makubwa kuipinga serikali ya kimabavu ya UDI chini ya Ian Smith ili kuonyesha mshikamano na wapigania uhuru wa Zimbabwe.

Joseph Sinde Warioba aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Wanafunzi Tanzania (National Union of Tanzania Students ) na mmoja wa vinara wa mgomo huo wa mwaka 1965 anatujuza yaliyotokea; “Walowezi wa Zimbabwe walipojitangazia uhuru tuliamua kufanya maandamano kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam bila kibali. Mwalimu aliagiza tukamatwe na wengi tuliwekwa mahabusu makao makuu ya polisi. Baadaye tulipelekwa Ikulu kuonana naye”.

“Kwenye mkutano wetu alitueleza kwa upole kwamba hatukukamatwa kwa sababu ya kuipinga serikali ya Walowezi wa Zimbabwe bali ni kwa sababu tumevunja sheria kwa kuandamana bila kibali na kwamba tumefanya uharibifu”
“Alisema hakuna hatua zaidi zitazochukuliwa dhidi yetu lakini akatutaka tuiombe msamaha serikali ya Uingereza kwa uharibifu wa mali tulioufanya (Wanafunzi waandamanaji walikwenda ubalozi wa Uingereza na kuharibu mali za ubalozi).

Alisema kuomba msamaha ni utaratibu uliopaswa kutekelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje lakini kwa sababu kwa wakati huo yeye aliishikilia nafasi hiyo, angeomba msamaha, ingetafsiriwa kwamba ni Rais aliyeomba msamaha na si Waziri wa Mambo ya Nje. Hivyo, akatutaka tuombe msamaha kwa niaba yake”

“Baada ya hapo Mwalimu akauliza kama yupo mwenye pingamizi. Mwanafunzi mmoja akasema kwamba analo pingamizi na papohapo Mwalimu akamuamuru kamishna wa polisi amchukue na kumcharaza bakora sita. Ni katika hatua hiyo tuligundua kwamba alikuwa na hasira na sisi. Mazungumzo yote yale ya upole yalikuwa ni njia ya kuficha hasira zake dhidi ya tulichokifanya”

“Baadaye Mwalimu alimuita tena Ikulu yule kijana aliyecharazwa bakora na kumfafanulia kwamba alikuwa ametenda yale kutokana na msukumo wa hasira. Alisema alikuwa ametenda kwa misingi ya ualimu”

“Kama tulivyo wengi, Mwalimu aliweza kupandwa na hasira na kufanya makosa. Lakini moja ya sifa zake ilikuwa ni kwamba hakuona soni kuyakubali mapungufu yake”.

Kijana aliyecharazwa bakora alikuwa ni Wilfred N. J. Mwabulambo. Yeye na Jaji Joseph Warioba, miaka kadhaa baadaye walikuja kuwa viongozi wakubwa serikalini. Wilfred Mwabulambo ambaye sasa ni marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za Uongozi, zikiwemo ukatibu mkuu kwenye Wizara mbalimbali na pia kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ameshawahi shika nafasi mbalimbali Kama vile Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.

Pichani ni Rais Nyerere akiwa na Wilfred Mwabulambo, Picha hii inatajwa kupigwa mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati Mwabulambo akiwa Kiongozi Serikalini.

1001526_699319653446404_771184154_n.jpg

Picha na Maelezo husika ni kwa Hisani ya Ndugu Ado Shaibu Ado wa Watanzania Mashuhuri.​
 
kuna gazeti linawekaga picha za kumbukumbu niliwahi muona mnene hivi wa wastan.
 
Kwa wasiomfahamu Mwambulambo, ni huyo jamaa mwenye nusu kipara aliyekuwa akijipima ubavu na Mohammed Ali wakati akiwa katibu mkuu wa wizara ya vijana na utamaduni mwaka 1977 au 1978 hivi. Alimwambia Ali usiniletee ujinga hapa; mimi siyo Joe Frazier wala George Foreman, nitakuzaba hapa hapa airport kavukavu.

1591777320957.png
 
Kwamba Jaji Joseph Sinde Warioba kwa sasa ni mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Katiba mpya.....
 
Hata kina Samuel sitta walilambwa viboko baadae wakaja kuwa viongozi lakini wao ilikuwa sababu ya kugomea jkt
 
Kwa wasiomfahamu Mwambulambo, ni huyo jamaa mwenye nusu kipara aliyekuwa akijipima ubavu na Mohammed Ali wakati akiwa katibu mkuu wa wizara ya vijana na utamaduni mwaka 1977 au 1978 hivi. Alimwambia Ali usiniletee ujinga hapa; mimi siyo Joe Frazier wala George Foreman, nitakuzaba hapa hapa airport kavukavu.

View attachment 1474029
Hahaha.....kwahiyo siku hiyo jamaa walizichapa live bila chenga?.....zamani raha sana
 
Ilikuwaje hiyo? Hebu tupe stori.
Ninachojua ni kwamba JKT walikuwa wanajiunga baada ya kumaliza kidato cha sita.
Pia jeshini kitu kinachoitwa mgomo hakipo kwani kule ni amri na utii.
Pia Mambo ya jeshi humalizwa kijeda
Mgogoro ulianza pale serikali ilipotangaza ni lazima wanafunzi wa kidato cha sita na vyuo waende kwa lazima jkt baadae vyuo havikuhusika kwa sababu waliomaliza kidato cha sita walienda moja kwa moja chuo kikuu na walienda vyuoni kama vyuo vya ufundi au ualimu walienda jkt.Mpango huu haukupokelewa vizuri na wanafunzi wa chuo kikuu ambao walijua wakimaliza wanaenda kupokea mshahara waliandamana wakamwona rais hiyo ilikuwa mwaka 1966 wakamsomea risala akawajibu risala yao ikiwemo kupunguza mshahara wake kwa asilimi 20 maana moja ya madai ilikuwa viongozi wana mishahara mikubwa yeye alikuwa anapata mshahara wa shilingi 5000 ambao mwalimu alisema ni sawa na pato la mkulima kwa miaka 25 baadae akawafukuza wote na akahakikisha wanarudi kwenye vijiji walivyotoka hii ilichangiwa na kauli yao miili yao inaweza kuwa kule lakini sio mioyo yao baada ya misamaha ya muda mrefu aliamua kuwarudisha lakini aliwaramba bakora kila.mmoja ni story ndefu nimeifupisha lakini kuna watu wanaijua hata ukigoogle utaipata
 
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU WILFRED MWABULAMBO ALICHARAZWA VIBOKO KWA KUMGOMEA RAIS NYERERE!

Wanafunzi wanapogoma au kufanya maandamano, dola hujibu mapigo kwa njia anuai. Ipo mifano ya wanafunzi waliosimamisha au kufukuzwa chuo, kuswekwa korokoroni na kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kujihusisha kwao na maandamano yasiyo na kibali cha dola.

Ni vigumu mtu kuamini kwamba kati ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kuwadhibiti wanafunzi wa chuo kikuu wanaoonekana kuwa watukutu ni kuwaadabisha kwa bakora! Amini usiamini, hapa nchini imewahi kufika pahala serikali, tena chini ya Mwalimu Nyerere kuwatandika viboko wanafunzi waliokosa utiifu kwa viongozi wa serikali.

Mfano wa hili ni kwenye mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam dhidi ya tamko la uhuru wa walowezi wa Zimbabwe (Unilateral Declaration of Independence-UDI) la mwaka 1965 chini ya Ian Smith.

Ikumbukwe kuwa baada ya Ian Smith na genge lake la walowezi kujitangazia uhuru na kutwaa mamlaka ya kuiongoza Rhodesia ya Kusini (Sasa Zimbabwe), Umoja wa Afrika uliitisha kikao cha dharura , ambapo viongozi wa nchi za Kiafrika waliafikiana kwa kauli moja kuipa shinikizo Uingereza (Waliokuwa wakoloni wa Rhodesia ya Kusini kabla ya kuwaachia walowezi) kubatilisha utawala wa Smith na kuukabidhi uhuru kwa wazalendo.

Azimio la Umoja wa Nchi Huru za Afrika liliweka bayana kwamba kama Uingereza haikutekeleza matakwa hayo ifikapo 15 Disemba 1965 basi nchi zote za Kiafrika zingefuta mahusiano ya kidiplomasia na nchi hiyo.

Uingereza ilipochelea kutekeleza azimio la OAU, Tanzania ilikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa za Kiafrika kufanya uamuzi mzito wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Uingereza. Kwenye hotuba yake Bungeni kuhusu suala hili, Mwalimu Nyerere aliweka wazi msimamo wa Tanzania. “Sera za Tanzania na Afrika kuhusiana na suala la Rhodesia ya Kusini mara zote zimekuwa na zitaendelea kuwa na lengo moja tu. Lengo hilo lilikuwa na litaendelea kuwa kupatikana kwa uhuru wa wengi. Kuhusu hili, kila hatua tuliyochukua na kila hotuba tuliyotoa vimelenga kulifanikisha lengo hilo. Hatuna zaidi ya hilo” alisema Mwalimu.

Kwa upande wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kama yalivyofanya makundi mbalimbali barani Afrika, wao waliamua kufanya maandamano makubwa kuipinga serikali ya kimabavu ya UDI chini ya Ian Smith ili kuonyesha mshikamano na wapigania uhuru wa Zimbabwe.

Joseph Sinde Warioba aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Wanafunzi Tanzania (National Union of Tanzania Students ) na mmoja wa vinara wa mgomo huo wa mwaka 1965 anatujuza yaliyotokea; “Walowezi wa Zimbabwe walipojitangazia uhuru tuliamua kufanya maandamano kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam bila kibali. Mwalimu aliagiza tukamatwe na wengi tuliwekwa mahabusu makao makuu ya polisi. Baadaye tulipelekwa Ikulu kuonana naye”.

“Kwenye mkutano wetu alitueleza kwa upole kwamba hatukukamatwa kwa sababu ya kuipinga serikali ya Walowezi wa Zimbabwe bali ni kwa sababu tumevunja sheria kwa kuandamana bila kibali na kwamba tumefanya uharibifu”
“Alisema hakuna hatua zaidi zitazochukuliwa dhidi yetu lakini akatutaka tuiombe msamaha serikali ya Uingereza kwa uharibifu wa mali tulioufanya (Wanafunzi waandamanaji walikwenda ubalozi wa Uingereza na kuharibu mali za ubalozi).

Alisema kuomba msamaha ni utaratibu uliopaswa kutekelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje lakini kwa sababu kwa wakati huo yeye aliishikilia nafasi hiyo, angeomba msamaha, ingetafsiriwa kwamba ni Rais aliyeomba msamaha na si Waziri wa Mambo ya Nje. Hivyo, akatutaka tuombe msamaha kwa niaba yake”

“Baada ya hapo Mwalimu akauliza kama yupo mwenye pingamizi. Mwanafunzi mmoja akasema kwamba analo pingamizi na papohapo Mwalimu akamuamuru kamishna wa polisi amchukue na kumcharaza bakora sita. Ni katika hatua hiyo tuligundua kwamba alikuwa na hasira na sisi. Mazungumzo yote yale ya upole yalikuwa ni njia ya kuficha hasira zake dhidi ya tulichokifanya”

“Baadaye Mwalimu alimuita tena Ikulu yule kijana aliyecharazwa bakora na kumfafanulia kwamba alikuwa ametenda yale kutokana na msukumo wa hasira. Alisema alikuwa ametenda kwa misingi ya ualimu”

“Kama tulivyo wengi, Mwalimu aliweza kupandwa na hasira na kufanya makosa. Lakini moja ya sifa zake ilikuwa ni kwamba hakuona soni kuyakubali mapungufu yake”.

Kijana aliyecharazwa bakora alikuwa ni Wilfred N. J. Mwabulambo. Yeye na Jaji Joseph Warioba, miaka kadhaa baadaye walikuja kuwa viongozi wakubwa serikalini. Wilfred Mwabulambo ambaye sasa ni marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za Uongozi, zikiwemo ukatibu mkuu kwenye Wizara mbalimbali na pia kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ameshawahi shika nafasi mbalimbali Kama vile Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.

Pichani ni Rais Nyerere akiwa na Wilfred Mwabulambo, Picha hii inatajwa kupigwa mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati Mwabulambo akiwa Kiongozi Serikalini.

1001526_699319653446404_771184154_n.jpg

Picha na Maelezo husika ni kwa Hisani ya Ndugu Ado Shaibu Ado wa Watanzania Mashuhuri.​
Huyu Mwabulambo ndo yule marehemu baba yake Wasiwasi Mwabulambo?
 
Pamoja na migogoro yao hawa watu na Mwalimu Nyerere, mimi nilichokiona hapa ni uzalendo wa hali ya juu sana ulioambatana na tabia za usomi wa hali ya juu sana. Mwalimu hakufanya makosa kumcharaza viboko Mwabulambo kwa sababu hawa wanafunzi hawakutakiwa kufanya huo uharibifu kwenye Ubalozi wa Uingereza. Zaidi ni kwamba Mwabulambo yeye alitakiwa ajiongeze kichwani. Mkuu wa Nchi anapowaita Ikulu kwa sababu mmefanya kitu ambacho hakijamfurahisha, bila kujali mood mtakayomkuta nayo, hutakiwi kuanza kubwabwaja maneno yako na wewe pale, kwa sababu anakuwa amewaita kwa ajili ya MAELEKEZO na si majadilano.Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kusikiliza na kuondoka. Ikulu panaogopesha, hata kama unaitwa kwa ajli ya jambo ambalo ni jema sana, ili mradi tu uwe hujaambiwa kuwa unaitiwa nini. Sasa ije iwe kwa swala ambalo lilikuwa linajulikana kuwa ni tuhuma? Alitakiwa akae kimya. I liked Mwalimu's style of leadership. Hata hivyo sifa ya juu kabisa ninayoina kwa Mwabulambo ni kwamba alikuwa jasiri sana.... and I like JASIRI people. Wote nimewapenda kwa matendo yao, Mwalimu na Mwabulambo pia
 
Back
Top Bottom