Mfahamu Wilfred Mwabulambo, aliyecharazwa bakora na Mwl. Julius K Nyerere

Komesha rushwa ni mapungufu? wanaume wenge kasoro! wanawake ni wapole, waaminifu na wachapakazi!

Nasema kasoro za mwalimu ndiyo kusema kwamba; mwenye hatia ya rushwa apigwe fimbo 12 anapoingia gerezani na 12 atokapo akamuonyeshe mkewe, --- Hapo maana yake walarushwa ni wanaume tu. Je hakukuwa na hawapo wanawake walarushwa???
 
Narudia wanawake ni wapole sasa mtu mwaminifu ale rushwa ya nini? soma tena
 
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU WILFRED MWABULAMBO ALICHARAZWA VIBOKO KWA KUMGOMEA RAIS NYERERE!

Wanafunzi wanapogoma au kufanya maandamano, dola hujibu mapigo kwa njia anuai. Ipo mifano ya wanafunzi waliosimamisha au kufukuzwa chuo, kuswekwa korokoroni na kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kujihusisha kwao na maandamano yasiyo na kibali cha dola.

Ni vigumu mtu kuamini kwamba kati ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kuwadhibiti wanafunzi wa chuo kikuu wanaoonekana kuwa watukutu ni kuwaadabisha kwa bakora! Amini usiamini, hapa nchini imewahi kufika pahala serikali, tena chini ya Mwalimu Nyerere kuwatandika viboko wanafunzi waliokosa utiifu kwa viongozi wa serikali.

Mfano wa hili ni kwenye mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam dhidi ya tamko la uhuru wa walowezi wa Zimbabwe (Unilateral Declaration of Independence-UDI) la mwaka 1965 chini ya Ian Smith.

Ikumbukwe kuwa baada ya Ian Smith na genge lake la walowezi kujitangazia uhuru na kutwaa mamlaka ya kuiongoza Rhodesia ya Kusini (Sasa Zimbabwe), Umoja wa Afrika uliitisha kikao cha dharura , ambapo viongozi wa nchi za Kiafrika waliafikiana kwa kauli moja kuipa shinikizo Uingereza (Waliokuwa wakoloni wa Rhodesia ya Kusini kabla ya kuwaachia walowezi) kubatilisha utawala wa Smith na kuukabidhi uhuru kwa wazalendo.

Azimio la Umoja wa Nchi Huru za Afrika liliweka bayana kwamba kama Uingereza haikutekeleza matakwa hayo ifikapo 15 Disemba 1965 basi nchi zote za Kiafrika zingefuta mahusiano ya kidiplomasia na nchi hiyo.

Uingereza ilipochelea kutekeleza azimio la OAU, Tanzania ilikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa za Kiafrika kufanya uamuzi mzito wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Uingereza. Kwenye hotuba yake Bungeni kuhusu suala hili, Mwalimu Nyerere aliweka wazi msimamo wa Tanzania. “Sera za Tanzania na Afrika kuhusiana na suala la Rhodesia ya Kusini mara zote zimekuwa na zitaendelea kuwa na lengo moja tu. Lengo hilo lilikuwa na litaendelea kuwa kupatikana kwa uhuru wa wengi. Kuhusu hili, kila hatua tuliyochukua na kila hotuba tuliyotoa vimelenga kulifanikisha lengo hilo. Hatuna zaidi ya hilo” alisema Mwalimu.

Kwa upande wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kama yalivyofanya makundi mbalimbali barani Afrika, wao waliamua kufanya maandamano makubwa kuipinga serikali ya kimabavu ya UDI chini ya Ian Smith ili kuonyesha mshikamano na wapigania uhuru wa Zimbabwe.

Joseph Sinde Warioba aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Wanafunzi Tanzania (National Union of Tanzania Students ) na mmoja wa vinara wa mgomo huo wa mwaka 1965 anatujuza yaliyotokea; “Walowezi wa Zimbabwe walipojitangazia uhuru tuliamua kufanya maandamano kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam bila kibali. Mwalimu aliagiza tukamatwe na wengi tuliwekwa mahabusu makao makuu ya polisi. Baadaye tulipelekwa Ikulu kuonana naye”.

“Kwenye mkutano wetu alitueleza kwa upole kwamba hatukukamatwa kwa sababu ya kuipinga serikali ya Walowezi wa Zimbabwe bali ni kwa sababu tumevunja sheria kwa kuandamana bila kibali na kwamba tumefanya uharibifu”
“Alisema hakuna hatua zaidi zitazochukuliwa dhidi yetu lakini akatutaka tuiombe msamaha serikali ya Uingereza kwa uharibifu wa mali tulioufanya (Wanafunzi waandamanaji walikwenda ubalozi wa Uingereza na kuharibu mali za ubalozi).

Alisema kuomba msamaha ni utaratibu uliopaswa kutekelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje lakini kwa sababu kwa wakati huo yeye aliishikilia nafasi hiyo, angeomba msamaha, ingetafsiriwa kwamba ni Rais aliyeomba msamaha na si Waziri wa Mambo ya Nje. Hivyo, akatutaka tuombe msamaha kwa niaba yake”

“Baada ya hapo Mwalimu akauliza kama yupo mwenye pingamizi. Mwanafunzi mmoja akasema kwamba analo pingamizi na papohapo Mwalimu akamuamuru kamishna wa polisi amchukue na kumcharaza bakora sita. Ni katika hatua hiyo tuligundua kwamba alikuwa na hasira na sisi. Mazungumzo yote yale ya upole yalikuwa ni njia ya kuficha hasira zake dhidi ya tulichokifanya”

“Baadaye Mwalimu alimuita tena Ikulu yule kijana aliyecharazwa bakora na kumfafanulia kwamba alikuwa ametenda yale kutokana na msukumo wa hasira. Alisema alikuwa ametenda kwa misingi ya ualimu”

“Kama tulivyo wengi, Mwalimu aliweza kupandwa na hasira na kufanya makosa. Lakini moja ya sifa zake ilikuwa ni kwamba hakuona soni kuyakubali mapungufu yake”.

Kijana aliyecharazwa bakora alikuwa ni Wilfred N. J. Mwabulambo. Yeye na Jaji Joseph Warioba, miaka kadhaa baadaye walikuja kuwa viongozi wakubwa serikalini. Wilfred Mwabulambo ambaye sasa ni marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za Uongozi, zikiwemo ukatibu mkuu kwenye Wizara mbalimbali na pia kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ameshawahi shika nafasi mbalimbali Kama vile Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.

Pichani ni Rais Nyerere akiwa na Wilfred Mwabulambo, Picha hii inatajwa kupigwa mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati Mwabulambo akiwa Kiongozi Serikalini.

1001526_699319653446404_771184154_n.jpg

Picha na Maelezo husika ni kwa Hisani ya Ndugu Ado Shaibu Ado wa Watanzania Mashuhuri.​
Kweli watoto hurithi Mambo ya wazazi wao!
Kuna mtoto wa Mwabulambo tulisoma naye ...Yeye alicharazwa viboka shuleni mbele ya kadamnasi kwa uzinzi! Sasa naona urithi wa mtoto kwa Baba ulipotoka kidogo!
 
watu wakampachika jina la "haambiliki" fikra zake zilikua hazikosolewi mpaka ikaanzishwa slogan ya "zidumu fikra za mwenyekiti" na wengi waliomkosoa walikua wanaishia matatizoni kama sio uhamishoni.
Mwenyekiti aliweka mazingira ya kuogopwa zaidi, watu hawakuthubutu hata kukaa pamoja na kuzungumzia mustakbali wa mambo kama yalikua yanaenda ndivyo sivyo, kila mtu alikua na wasiwasi na mwenzie kwa jinsi mzee alivyowatengezea watu uoga kutokana na vitisho vyake.
Labda ndio maana kwa wajihi anashabihiana na PK mtusi.
To some extent rais anatakiwa awe dictector, maana kuna watu wavurugaji tu wa makusudi kwa jina la demokrasia.
 
Mgogoro ulianza pale serikali ilipotangaza ni lazima wanafunzi wa kidato cha sita na vyuo waende kwa lazima jkt baadae vyuo havikuhusika kwa sababu waliomaliza kidato cha sita walienda moja kwa moja chuo kikuu na walienda vyuoni kama vyuo vya ufundi au ualimu walienda jkt.Mpango huu haukupokelewa vizuri na wanafunzi wa chuo kikuu ambao walijua wakimaliza wanaenda kupokea mshahara waliandamana wakamwona rais hiyo ilikuwa mwaka 1966 wakamsomea risala akawajibu risala yao ikiwemo kupunguza mshahara wake kwa asilimi 20 maana moja ya madai ilikuwa viongozi wana mishahara mikubwa yeye alikuwa anapata mshahara wa shilingi 5000 ambao mwalimu alisema ni sawa na pato la mkulima kwa miaka 25 baadae akawafukuza wote na akahakikisha wanarudi kwenye vijiji walivyotoka hii ilichangiwa na kauli yao miili yao inaweza kuwa kule lakini sio mioyo yao baada ya misamaha ya muda mrefu aliamua kuwarudisha lakini aliwaramba bakora kila.mmoja ni story ndefu nimeifupisha lakini kuna watu wanaijua hata ukigoogle utaipata
Enzi za kina warioba kulikuwa na Form Six kweli??Nauliza lakini au ndo middle School Enzi hizo
 
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU WILFRED MWABULAMBO ALICHARAZWA VIBOKO KWA KUMGOMEA RAIS NYERERE!

Wanafunzi wanapogoma au kufanya maandamano, dola hujibu mapigo kwa njia anuai. Ipo mifano ya wanafunzi waliosimamisha au kufukuzwa chuo, kuswekwa korokoroni na kuchukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu kwa kujihusisha kwao na maandamano yasiyo na kibali cha dola.

Ni vigumu mtu kuamini kwamba kati ya hatua zinazoweza kuchukuliwa kuwadhibiti wanafunzi wa chuo kikuu wanaoonekana kuwa watukutu ni kuwaadabisha kwa bakora! Amini usiamini, hapa nchini imewahi kufika pahala serikali, tena chini ya Mwalimu Nyerere kuwatandika viboko wanafunzi waliokosa utiifu kwa viongozi wa serikali.

Mfano wa hili ni kwenye mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam dhidi ya tamko la uhuru wa walowezi wa Zimbabwe (Unilateral Declaration of Independence-UDI) la mwaka 1965 chini ya Ian Smith.

Ikumbukwe kuwa baada ya Ian Smith na genge lake la walowezi kujitangazia uhuru na kutwaa mamlaka ya kuiongoza Rhodesia ya Kusini (Sasa Zimbabwe), Umoja wa Afrika uliitisha kikao cha dharura , ambapo viongozi wa nchi za Kiafrika waliafikiana kwa kauli moja kuipa shinikizo Uingereza (Waliokuwa wakoloni wa Rhodesia ya Kusini kabla ya kuwaachia walowezi) kubatilisha utawala wa Smith na kuukabidhi uhuru kwa wazalendo.

Azimio la Umoja wa Nchi Huru za Afrika liliweka bayana kwamba kama Uingereza haikutekeleza matakwa hayo ifikapo 15 Disemba 1965 basi nchi zote za Kiafrika zingefuta mahusiano ya kidiplomasia na nchi hiyo.

Uingereza ilipochelea kutekeleza azimio la OAU, Tanzania ilikuwa kati ya nchi za mwanzo kabisa za Kiafrika kufanya uamuzi mzito wa kuvunja mahusiano ya kidiplomasia na Uingereza. Kwenye hotuba yake Bungeni kuhusu suala hili, Mwalimu Nyerere aliweka wazi msimamo wa Tanzania. “Sera za Tanzania na Afrika kuhusiana na suala la Rhodesia ya Kusini mara zote zimekuwa na zitaendelea kuwa na lengo moja tu. Lengo hilo lilikuwa na litaendelea kuwa kupatikana kwa uhuru wa wengi. Kuhusu hili, kila hatua tuliyochukua na kila hotuba tuliyotoa vimelenga kulifanikisha lengo hilo. Hatuna zaidi ya hilo” alisema Mwalimu.

Kwa upande wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kama yalivyofanya makundi mbalimbali barani Afrika, wao waliamua kufanya maandamano makubwa kuipinga serikali ya kimabavu ya UDI chini ya Ian Smith ili kuonyesha mshikamano na wapigania uhuru wa Zimbabwe.

Joseph Sinde Warioba aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Wanafunzi Tanzania (National Union of Tanzania Students ) na mmoja wa vinara wa mgomo huo wa mwaka 1965 anatujuza yaliyotokea; “Walowezi wa Zimbabwe walipojitangazia uhuru tuliamua kufanya maandamano kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam bila kibali. Mwalimu aliagiza tukamatwe na wengi tuliwekwa mahabusu makao makuu ya polisi. Baadaye tulipelekwa Ikulu kuonana naye”.

“Kwenye mkutano wetu alitueleza kwa upole kwamba hatukukamatwa kwa sababu ya kuipinga serikali ya Walowezi wa Zimbabwe bali ni kwa sababu tumevunja sheria kwa kuandamana bila kibali na kwamba tumefanya uharibifu”
“Alisema hakuna hatua zaidi zitazochukuliwa dhidi yetu lakini akatutaka tuiombe msamaha serikali ya Uingereza kwa uharibifu wa mali tulioufanya (Wanafunzi waandamanaji walikwenda ubalozi wa Uingereza na kuharibu mali za ubalozi).

Alisema kuomba msamaha ni utaratibu uliopaswa kutekelezwa na Waziri wa Mambo ya Nje lakini kwa sababu kwa wakati huo yeye aliishikilia nafasi hiyo, angeomba msamaha, ingetafsiriwa kwamba ni Rais aliyeomba msamaha na si Waziri wa Mambo ya Nje. Hivyo, akatutaka tuombe msamaha kwa niaba yake”

“Baada ya hapo Mwalimu akauliza kama yupo mwenye pingamizi. Mwanafunzi mmoja akasema kwamba analo pingamizi na papohapo Mwalimu akamuamuru kamishna wa polisi amchukue na kumcharaza bakora sita. Ni katika hatua hiyo tuligundua kwamba alikuwa na hasira na sisi. Mazungumzo yote yale ya upole yalikuwa ni njia ya kuficha hasira zake dhidi ya tulichokifanya”

“Baadaye Mwalimu alimuita tena Ikulu yule kijana aliyecharazwa bakora na kumfafanulia kwamba alikuwa ametenda yale kutokana na msukumo wa hasira. Alisema alikuwa ametenda kwa misingi ya ualimu”

“Kama tulivyo wengi, Mwalimu aliweza kupandwa na hasira na kufanya makosa. Lakini moja ya sifa zake ilikuwa ni kwamba hakuona soni kuyakubali mapungufu yake”.

Kijana aliyecharazwa bakora alikuwa ni Wilfred N. J. Mwabulambo. Yeye na Jaji Joseph Warioba, miaka kadhaa baadaye walikuja kuwa viongozi wakubwa serikalini. Wilfred Mwabulambo ambaye sasa ni marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za Uongozi, zikiwemo ukatibu mkuu kwenye Wizara mbalimbali na pia kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Jaji Joseph Sinde Warioba ambaye ameshawahi shika nafasi mbalimbali Kama vile Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.

Pichani ni Rais Nyerere akiwa na Wilfred Mwabulambo, Picha hii inatajwa kupigwa mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati Mwabulambo akiwa Kiongozi Serikalini.

1001526_699319653446404_771184154_n.jpg

Picha na Maelezo husika ni kwa Hisani ya Ndugu Ado Shaibu Ado wa Watanzania Mashuhuri.​
Asante sana kwa taarifa yako ambayo ni sahihi kwa asilimia 99. Kitu kimoja nilichokiona ambacho si sahihi ni kule kusema Wilfred Mwabulambo aliwahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Marehemu Mwabulambo hakuwahi kushika wadhifa huo. Aliishia kwenye uKatibu Mkuu kwenye wizara zingine tu, ya mwisho ikiwa Wizara ya Afya. Ukatibu Mkuu wake wa kwanza ulikuwa SCOPO, baada ya kupandishwa cheo kutoka Mkurugenzi wa Idara moja hapo UTUMISHI. Ni kweli alicharazwa viboko na Mwalimu na yeye mwenyewe alikuwa akijisifia kwa hilo. Miaka ya 70 na 80 alikuwa akichangia makala kwenye 'Daily News' na katika toleo mojawapo ya gazeti hilo aliandika habari hiyo; si kwa kumlaumu Mwalimu bali kwa kuashiria kujisifia. Kitu cha pili ambacho sina uhakika wa usahihi wake kutokana na maelezo yako ni kusema Mwalimu alimuagiza polisi amchape hivyo viboko. Kufuatana na maelezo yake Marehemu, Mwalimu alishika fimbo na kumcharaza yeye mwenyewe, na hicho ndiyo kikawa kitu cha kujisifia. Kitu cha tatu ambacho kinabidi kudhihirishwa ni tarehe ya picha ya Marehemu akiwa na Mwalimu. Nadhani lazima iwe kabla ya miaka ya 90. Sikumbuki alifariki lini lakini nadhani miaka ya 80 mwishoni au mwanzoni mwa miaka ya 90.
 
Yote uliyosema ni sahihi kwa 100%. Pia nakumbuka aliwahi kuwa RDD, hawa saivi wanaitwa katibu tawala (RAS). Pia marehem alikuwa na mwisho mgumu.
 
Inaonekana wanafunzi wa vyuo wa zaman walikua na uelewa sana na mambo ya kimataifa....wa sa hivi hata ramani yenyewe ya dunia sidhani kama wanaielewa vizuri!
Watayajuaje wkt wanakesha instagram na fesibuku kuangalia diamond ametoka na nani[emoji23][emoji23][emoji23]

Wakigoma ujue wamenyimwa boom fullstop.
 
Asante sana kwa taarifa yako ambayo ni sahihi kwa asilimia 99. Kitu kimoja nilichokiona ambacho si sahihi ni kule kusema Wilfred Mwabulambo aliwahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Marehemu Mwabulambo hakuwahi kushika wadhifa huo. Aliishia kwenye uKatibu Mkuu kwenye wizara zingine tu, ya mwisho ikiwa Wizara ya Afya. Ukatibu Mkuu wake wa kwanza ulikuwa SCOPO, baada ya kupandishwa cheo kutoka Mkurugenzi wa Idara moja hapo UTUMISHI. Ni kweli alicharazwa viboko na Mwalimu na yeye mwenyewe alikuwa akijisifia kwa hilo. Miaka ya 70 na 80 alikuwa akichangia makala kwenye 'Daily News' na katika toleo mojawapo ya gazeti hilo aliandika habari hiyo; si kwa kumlaumu Mwalimu bali kwa kuashiria kujisifia. Kitu cha pili ambacho sina uhakika wa usahihi wake kutokana na maelezo yako ni kusema Mwalimu alimuagiza polisi amchape hivyo viboko. Kufuatana na maelezo yake Marehemu, Mwalimu alishika fimbo na kumcharaza yeye mwenyewe, na hicho ndiyo kikawa kitu cha kujisifia. Kitu cha tatu ambacho kinabidi kudhihirishwa ni tarehe ya picha ya Marehemu akiwa na Mwalimu. Nadhani lazima iwe kabla ya miaka ya 90. Sikumbuki alifariki lini lakini nadhani miaka ya 80 mwishoni au mwanzoni mwa miaka ya 90.
Mzee Mwabulambo amefariki mwanzoni mwa miaka ya 90
 
Watayajuaje wkt wanakesha instagram na fesibuku kuangalia diamond ametoka na nani[emoji23][emoji23][emoji23]

Wakigoma ujue wamenyimwa boom fullstop.
Dah......wanasikitisha kwakweli wasomi wetu!
 
Back
Top Bottom