Mfahamu Wilfred Mwabulambo, aliyecharazwa bakora na Mwl. Julius K Nyerere

Komesha rushwa ni mapungufu? wanaume wenge kasoro! wanawake ni wapole, waaminifu na wachapakazi!


Nasema kasoro za mwalimu ndiyo kusema kwamba; mwenye hatia ya rushwa apigwe fimbo 12 anapoingia gerezani na 12 atokapo akamuonyeshe mkewe, --- Hapo maana yake walarushwa ni wanaume tu. Je hakukuwa na hawapo wanawake walarushwa???
 
Nasema kasoro za mwalimu ndiyo kusema kwamba; mwenye hatia ya rushwa apigwe fimbo 12 anapoingia gerezani na 12 atokapo akamuonyeshe mkewe, --- Hapo maana yake walarushwa ni wanaume tu. Je hakukuwa na hawapo wanawake walarushwa???
Narudia wanawake ni wapole sasa mtu mwaminifu ale rushwa ya nini? soma tena
 
Kweli watoto hurithi Mambo ya wazazi wao!
Kuna mtoto wa Mwabulambo tulisoma naye ...Yeye alicharazwa viboka shuleni mbele ya kadamnasi kwa uzinzi! Sasa naona urithi wa mtoto kwa Baba ulipotoka kidogo!
 
Labda ndio maana kwa wajihi anashabihiana na PK mtusi.
To some extent rais anatakiwa awe dictector, maana kuna watu wavurugaji tu wa makusudi kwa jina la demokrasia.
 
Enzi za kina warioba kulikuwa na Form Six kweli??Nauliza lakini au ndo middle School Enzi hizo
 
Asante sana kwa taarifa yako ambayo ni sahihi kwa asilimia 99. Kitu kimoja nilichokiona ambacho si sahihi ni kule kusema Wilfred Mwabulambo aliwahi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Marehemu Mwabulambo hakuwahi kushika wadhifa huo. Aliishia kwenye uKatibu Mkuu kwenye wizara zingine tu, ya mwisho ikiwa Wizara ya Afya. Ukatibu Mkuu wake wa kwanza ulikuwa SCOPO, baada ya kupandishwa cheo kutoka Mkurugenzi wa Idara moja hapo UTUMISHI. Ni kweli alicharazwa viboko na Mwalimu na yeye mwenyewe alikuwa akijisifia kwa hilo. Miaka ya 70 na 80 alikuwa akichangia makala kwenye 'Daily News' na katika toleo mojawapo ya gazeti hilo aliandika habari hiyo; si kwa kumlaumu Mwalimu bali kwa kuashiria kujisifia. Kitu cha pili ambacho sina uhakika wa usahihi wake kutokana na maelezo yako ni kusema Mwalimu alimuagiza polisi amchape hivyo viboko. Kufuatana na maelezo yake Marehemu, Mwalimu alishika fimbo na kumcharaza yeye mwenyewe, na hicho ndiyo kikawa kitu cha kujisifia. Kitu cha tatu ambacho kinabidi kudhihirishwa ni tarehe ya picha ya Marehemu akiwa na Mwalimu. Nadhani lazima iwe kabla ya miaka ya 90. Sikumbuki alifariki lini lakini nadhani miaka ya 80 mwishoni au mwanzoni mwa miaka ya 90.
 
Yote uliyosema ni sahihi kwa 100%. Pia nakumbuka aliwahi kuwa RDD, hawa saivi wanaitwa katibu tawala (RAS). Pia marehem alikuwa na mwisho mgumu.
 
Inaonekana wanafunzi wa vyuo wa zaman walikua na uelewa sana na mambo ya kimataifa....wa sa hivi hata ramani yenyewe ya dunia sidhani kama wanaielewa vizuri!
Watayajuaje wkt wanakesha instagram na fesibuku kuangalia diamond ametoka na nani[emoji23][emoji23][emoji23]

Wakigoma ujue wamenyimwa boom fullstop.
 
Mzee Mwabulambo amefariki mwanzoni mwa miaka ya 90
 
Watayajuaje wkt wanakesha instagram na fesibuku kuangalia diamond ametoka na nani[emoji23][emoji23][emoji23]

Wakigoma ujue wamenyimwa boom fullstop.
Dah......wanasikitisha kwakweli wasomi wetu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…