Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 16,583
- 42,992
J
Japo damu ya B's inakulilia unaanza kuwa na akiliAmeongea mambo ya msingi sana ingawaje huwa nakuwa muangalifu sana ninapotaka kujadili issues za ktu kinachoitwa usalama wa taifa kutokana na mada inayoletwa na mtu kama TumainiEl !!
Kwa mataifa aliyotolea mfano (US na Israel) na intelligence agencies zao(CIA na Mossad), wakikuambia someone is a traitor or the enemy of state basi ni traitor na enemy of state kweli kweli! Unfortunately, kwa mtu kama TumainiEl, watu kama akina Ben Saanane, Azory Gwanda, Zitto Kabwe, Tundu Lissu, and the like, kwake hawa ni traitors and/or enemy of state!!
Ukimtoa Gwanda ambae ni Mwandishi, wengine wote wanaoonekana kwamba ni traitors and/or enemy of state kimsingi wao ni critics... and even most important, wao ni politicians ambao no matter what, lazima wai-challenge administration!
Lakini TumainiEl kaongea jambo lingine zito kweli kweli, kwamba:-I doubt kwamba Tumain anaiishi hii kauli, na hapo ndipo lilipo tatizo la msingi! Hata wale wanaodhani kwamba kwao ni "taifa kwanza" kimsingi wanachokiishi sio "taifa kwanza" bali ni "serikali kwanza!"
Taifa kama Israel au US hakuna Enemy of the Government bali kuna Enemy of the State! Tanzania karibu wote wanaoitwa Enemy of the State sio Enemy of State bali Enemy of the Government!
Tena bora hata ya hao wanaoamini katika "serikali kwanza" manake kuna wengine wengi tu, wao "Magufuli kwanza!" Ukimsikia mtu kama Musiba, yule unajua kabisa kwamba kwake ni "Magufuli Kwanza" na wala sio "..Serikali Kwanza" let alone "Taifa Kwanza!"
Ni kutokana na ukweli huo ndio maana wala si ajabu kusikia watu wa aina yake wakishambulia baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa serikali ile ile wanayodhani wanaitetea!!
Kwahiyo nakaa kitako kufuatilia mwendelezo TumainiEl kwa uangalifu mkubwa!!!
Hata hivyo, kuna jambo moja la msingi sana amelitaja ambalo nadhani ndio hasa linatakiwa kutawala mjadala huu kwamba:-Kwa hakika, ni jambo muhimu sana kwa Decision Makers, na sio Rais peke yake kuzungukwa na watu "wenye akili"
Neno "wenye akili" nimeliweka kwenye kifunga na kifungua semi kwa kuzingatia muktadha wa Tanzania na uongozi tulionao! JPM kuwa na watendaji wakuu na mawaziri wenye PhD ndo anadhani amezungukwa na wenye akili kwa sababu tunapima akili kwa idadi ya vyeti with vertical growth: Mwenye Bachelor Degree>>> Master Degree>>>Doctorate>>>Professor!
Kwa mifumo yenu, na inayoshadadiwa zaidi na JPM, hapo mwenye akili kuliko wote ni Profesa na Kilaza kuliko wote ni mwenye Bachelor!
Lakini kama serikali na decision makers wanazungukwa na wenye akili kwa maana ya akili, hakika hilo ndilo linahitajika sana! Hawa watu wakiwamo kwenye sekta ya usalama, watakuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya Enemy of the State na Enemy of the Government, ambae hata hivyo kimsingi wala sio Enemy of the Government bali ni Critic of the Government!
Isitoshe, unapokuwa na Vichwa pale Eagle House, na wenyewe wanaweza kuwa na impact kubwa sana kiuchumi hata kama indirectly! Ni hivi vichwa vya Eagle House ndivyo vinavyoweza kutuongoza kwenye masuala ya international cooperation, and of course, international relations.
Aidha, hao Tumaini aliowaita wenye akili wakiwamo kwenye sekta ya uchumi, pia watakuwa na uwezo wa kunyambua kwa makini na kuweka bayana ina maana gani inaposemwa kuangalia mambo kwa miaka 50-100 ijayo!!
Leo hii mtu anaweza kukuambia JPM anaangalia mbele kwa miaka 50 ijayo ndo maana, for instance, anatumia trilions ku-finance Stiegler's Gorge hata kama kwa uchumi wa sasa inaweza kuwa underutilized, na badala yake kuwa economically viable in the next 5-10 years!
Wataongea hayo huku wakisahau dhana ya optimal utilization of our limited resources!!
Kwamba kwanini tutumie our limited resource kwa ajili ya investment itakayokuja kuwa materialized in the next 5-10 years wakati kuna opportunities kibao bado hazijawa exploited, na zenye uwezo wa kuleta impact kubwa zaidi ya kiuchumi muda mfupi tu baada ya investment kuwa imeshafanyika na hatimae project husika ikawa ndie "financier" wa projects zingine!
Tanzania sio kama China yenye Ghost Cities kwa sababu China hawana shida ya capital!